I KILLED MY LOVER 26

 


SCENE 26: -

KESHO YAKE JIONI: -

(Rafiki na binamu zake Liliana wamekusanyika pamoja kwenye ukumbi mmoja ambao umeambatana na sehemu ya mgahawa, watu wanapata chakula wakati huohuo kuna sherehe ya kumpongeza Liliana kwa kufikia miaka ishirini na tatu)

Linda :( mmoja wa rafiki za Liliana) sikilizeni hii ni surprise party ya rafiki yetu najua jana hatukuweza kufanya hii pati mama yake alikataa maana alikuwa amemuandalia sherehe nyumbani na tayari tulikuwa tumeshanchanga ndo tukaona isiwe kesi tuifanye hata leo

Mabel :( rafiki mwingine) haina shida najua bado ana mood ya birthday… (Anacheka kidogo) maana yeye Kwa kusherekea

Anna: acha asherekee amepitia mambo mengi Sana katika maisha yake

Lucy :( rafiki yake mwingine) guys… (Anachungulia anaangalia simu yake) Liliana anapiga simu

Mabel: pokea sasa unashangaa nini?

Lucy :( anapokea) Lily…tupo ukumbini Kama utaweza njoo tumekaa huku tunakunywa

Liliana: okay nakuja (anakata simu na kuanza kuelekea ukumbini baada ya hatua chache anafika ukumbini hapo)

(Rafiki zake wanapiga kelele surprise, na kumpa zawadi kedekede)

Liliana: jamani asanteni Jana mmenipa zawadi na leo mnanipa zawadi

Mabel: hii sherehe ilikuwa ya Jana sema tu Aunt Bianca alitukatalia…

Liliana: jamani asanteni Sana…mbarikiwe Zaidi na Zaidi jamani

(Wakati huo kuna mwanaume mtu mzima Kama mzee hivi umri wake ni miaka 55-60 anaingia mgahawani hapo, anapoangaza angaza anatupa macho kwa Liliana, anabaki anamuangalia sana)

Mwanaume: wow…she is so beautiful (anang’ata midomo) I want her...ila nitampataje huku hapa wanaonekana kuwa na sherehe na hawaruhusu yeyote kuingia…nitakaa mpaka mwisho nipate hata namba zake

(Upande wa kina Liliana bado wanasherekea sherehe hiyo)

Liliana: People…guys ngoja nakuja naenda kupokea simu mama ananipigia…

Lucy: okay

Liliana :( anatoka nje akipitia mgahawani)

Mwanamume :( anamfuata nyuma) samahani

Liliana :( anamgeukia kisha anampa ishara kuwa anaongea na simu)

Mwanaume :( anakaa kimya huku anamuangalia Sana Liliana)

Liliana: okay mama baadae naenjoi Sana…baadae (anakata simu kisha anamsikiliza mwanaume huyo) yes…shikamoo?

Mwanaume: marahaba… (Anampa mkono)

Liliana :( anamuangalia usoni sura ya mwanaume huyo inamrudisha miaka 16 nyuma usiku mmoja akiwa anakimbia kutoka kwa shangazi na mjomba wake alimuomba msaada mmoja mlinzi mmoja nae akamfanyia unyama kwa kumbaka) ha!!!

Mwanaume :( anatabasamu) nini? Mrembo?

Liliana: labda nakufananisha…

Mwanaume: Na nani?

Liliana: Na mtu mmoja aliwahi kunifanyia unyama wakati bado nipo mdogo

Mwanamume :( anarudisha kumbukumbu nyuma na anakumbuka tukio lile) hapana sijawahi (anakumbuka na kujisemea moyoni) huyu ndo yule mtoto niliyevaa mpira na kumbaka…Mungu wangu nimeumbuka leo

Liliana: anyway, labda nimekufananisha maana wanasema kuwa binadamu ni wawili wawili

Mwanaume: anyway…hiyo ni kweli…by the way mimi naitwa Robert

Liliana: sawa… (Anataka kuondoka)

Robert: mbona una haraka wewe unaitwa nani?

Liliana: Liliana… (Anaondoka)

Robert: subiri…

Liliana: (anasubiri)

Robert: unaonekana una haraka Sana basi naaomba namba yako nitakutafuta

Liliana: (anamuangalia tena usoni) ila ni wewe yaani ni wewe kabisa…

Robert: naomba namba yako tutazungumza

Liliana :( anaondoka bila kusema kitu)

Robert: nitapata tu namba zako…dah katoto kamekuwa katamu haka…Ah (anashusha pumzi) wazungu wanasema destiny…baada ya miaka mingi kupita hatimaye nimekutana nae tena, kipindi hiki simuachii… (Anakaa na kuendelea na mambo yake)

(Upande wa Liliana anasherekea ila akili yake inamfikiria Robert)

Liliana: ila ni yeye kabisa sijui lakini labda kisema chake binadamu wawili wawili ila nikimuangalia ni yeye kabisa sema tu amezeeka ila ni yeye…anyway haina shida kwa vyovyote sitaki anaizoee (anageuka na kuangalia alipokaa Robert)

Robert: (anamkonyeza)

Liliana (anafyonza) sijui lipoje?

(Anaendelea kusherekea sherehe aliyoandaliwa na afiki zake ila tayari akili yake imeshavurugika)

Robert: she will be mine (Anatabasamu)

Post a Comment

1 Comments