MUNGU MKUU 7

 


SCENE 7: -

(Asubuhi nzuri na ya kupendeza tena ya siku nyingine na siku ya kwanza ya juma yaani Jumamosi, Ken na mkewe Keddy wanausubiri kwa hamu ugeni wa mchumba wa kupangiwa na wazazi wa Ariana)

Keddy: yaani nimefurahi jamani hii siku imefika mwanangu nae aolewe jamani…

Ken: kweli kabisa mke wangu na njia za Mungu hazichunguziki hata kidogo…Jeremy ni kijana mcha Mungu sana…baba yake aliponiambia kuwa kijana wake amemaliza masomo na kwa sasa anatafuta mke nikamtaja mwanangu na hapohapo baba yake Jeremy akaniunga mkono na kusema kuwa watafaa kuwa wanandoa na wataishi vizuri pia

Mary: kumbe watoto hawajawahi kuonana?

Keddy: ndio…baba Ariana na baba wa huyu kijana wanajuana na wanasali kanisa moja na wote ni wazee wa kanisa

Mary: sawasawa…

(Miriam anakuja walipo Ken, Keddy na Mary)

Mary: vipi wewe?

Miriam: wageni wanakuja

Ken: sawa… (kwa Mary) kaandae vinywaji na chakula Miriam atakusaidia…kwa Ariana asitoke kwanza...

Mary:(huku anatabasamu) sawa shem...

(Kengele ya mlangoni inalia)

Keddy:(haraka anafungua mlango) karibuni jamani

(Wageni ni pamoja na kijana mmoja mrefu, mtanashati tena anaonekana ni mstaraabu sana, kuna mzee na bila shaka ni baba wa kijana huyu mtanashati lakini pia kuna kijana mwingine ni mrefu ila wa wastani)

Mzee:(huku anaongoza njia) asante sana…na Amani iwe juu ya nyumba yenu

Ken: amina karibuni sana

(Wageni wanakaa)

Miriam:(anatokea akiwa amebeba vinywaji na anaonyesha tabasamu wakati wote)

Jeremy:(anamuangalia Miriam kwa umakini mkubwa sana) wow… (anamnong’oneza baba yake) baba je huyu ni mwanamke nayetarajia kumuoa?

Baba: hapana mwanangu, mkeo mtarajiwa hapa hayupo utamuona baadae mara baada ya kusikilizana pande zote mbili wewe tulia tu kila kitu kitakuwa sawa

Jeremy:(kimya huku anajisemea moyoni) huyu mwanamke ni mrembo sana…na nimetokea kumpenda sana…

Miriam:(hana habari anatabasamu tu)

Jeremy:(anapokea kinywaji kutoka kwa Miriam) unaitwa nani?

Miriam: naitwa Miriam…na ni mdogo wake Ariana…shemeji karibu kwenye familia

Jeremy:(anajisemea moyoni) nitakaribia kwa ajili yako…nimekupenda sana Miriam na nitakuoa wewe na sio Ariana sijui nimefanya nini kumkubali mwanamke ambae sikuwahi kumuona hata mara moja

Mzee:(kwa Miriam) unaonekana una heshima sana…unasoma au unafanya nini?

(Keddy na Ken wanatabasamu)

Miriam:(anajibu kwa ujasiri) nasoma chuo nipo mwaka wa kwanza…nasomea sheria…

Mzee: safi sana unataka kuwa muamuzi kama Debora?

Miriam: hapana baba nataka kuwa wakili

Mzee: safi sana…

(Wakati huo Ariana anawachungulia na hafurahishwi na jinsi watu wanavyomfurahia Miriam)

Ariana: yaani huyu mwanamke kila sehemu anataka kujionyesha yeye ndo mzuri…(anafyonza)ananikera kweli yaani (anamchungulia Jeremy) ila mwanamme mzuri huyu…anafaa kuwa mume wangu…he is so handsome

(Huku sebuleni, furaha na Amani zinaendelea kutawala)

Mzee: basi sawa… (anamuangalia Miriam) nimekufurahia sijui kwanini?

(Wanacheka sana)

Jeremy:(anajisemea moyoni) hunizidi mimi…nimemfurahia sana na hata kama unasoma nitakusubiri tu sina haraka ya kuoa sasa…nimempata mwanamke wa maisha yangu na sina mpango wa kukuacha…Miriam my love…

Miriam:(anaendelea kutabasamu kisha anaondoka na kwenda zake jikoni)

Jeremy:(kwa baba yake) dad… (anamnong’oneza baba yake) kwani leo ndo tunatoa mahari?

Mzee: hapana mwanangu au unaonaje?

Jeremy: isiwe leo lakini pia mi naona mtupe muda kidogo mimi na Ariana tujuane tuzoeana na Zaidi tuwe marafiki…

Mzee: sawa haina shida mwanagu sisi tunakusikiliza wewe na huyo mwenzio…

Jeremy: asante baba

Ken:(anaangalia mezani) oh naona chakula tayari lakini kabla ya hapo naomba nimlete kwenu binti yangu mkubwa mpendwa sana

Mzee: bila shaka…

Ken: mama Ariana nenda kamlete binti yetu mpenzi…

(Wageni wanaonyesha furaha)

Keddy:(ananyanyuka na kuingia ndani alipo Ariana na baada ya muda anatoka akiwa na Ariana)

Ariana:(anaonyesha tabasamu na aibu pia)

Mzee:(anaonyesha kumfurahia pia)

Ariana:(anamsalimia baba Jeremy kwa heshima zote)

Mzee: marahaba mama…

Ariana:(anamsalimia kaka aliyekuja na Jeremy kama mshenga wake)

Mshenga:(anaitikia na anaonekana ni kijana mwenye aibu sana)

Ariana:(anamsalimia Jeremy)

Jeremy:(anamuitikia na kuonyesha tabasamu ila anamuangalia Miriam)

Miriam:(hana kinyongo wala nini na anaonekana ana furaha kuliko mtu yeyote hapo)

Ken: basi baada ya hayo…tujongee mezani...

Mzee: asante sana

(Wenyeji wanawaongoza wageni na kwenda mezani kupata chakula cha mchana pamoja)

Jeremy:(anamuangalia sana Miriam)

Ariana:(anamuona Jeremy anavyomuangalia Miriam)

Miriam:(anakula na wala hana hata muda na mtu)

(Familia zote mbili wanaendelea kula huku kila mmoja wao anafurahia chakula kile, baada ya kula kwa muda mrefu kidogo hatimae wanamaliza kula)

Mzee:(ananyanyuka na kwenda kunawa) chakula kitamu sana

(Keddy na Mary wanafurahi)

Ariana :( anachukia Sana maana anajua kuwa aliyepika chakula kile ni Miriam)

(Wageni wengine nao wananawa na wao wanakisifu chakula)

Miriam :( anatoa vyombo na kuvipeleka jikoni)

Jeremy :( anamuangalia Ariana)

Ariana :( anaona aibu na kuanza kumsaidia kutoa vyombo)

(Wageni pamoja wenyeji wanarudi sebuleni kukaa kidogo kabla hawajaaga, wanakaa kwa muda kidogo kisha wanaaga)

Mzee: jamani tunashukuru Sana kwa kila kitu…tumefurahi sana

Keddy: tumefurahi pia karibuni Sana

Mzee: tutakuwa ni wakwe wazuri sana

Keddy: kabisa

Ariana :( anacheka)

Jeremy :( anamuangalia Miriam)

(Wageni wananyanyuka na kuondoka zao, wakisindikizwa na wenyeji)

Jeremy :( anamuaga Miriam) bye Miriam (anaondoka yeye na mzee pamoja na mshenga aliyekuja nae)

Post a Comment

1 Comments

  1. Love story is about to begin...what will happen next...don't go anywhere

    ReplyDelete