SCENE 46: -
USIKU HUOHUO:
NYUMBANI KWA BIANCA: -
(Liliana anafika nyumbani akiwa
ameambatana na binamu zake, wanapofika wanapigwa na butwaa kuona nyumba yao
imeteketea kwa moto, anahisi miguu inaishiwa nguvu)
Anna:
(anamshika bega) mdogo wangu jikaze
Lupemba:
(anakuja anamkumbatia Liliana)
Liliana:
(anatoka machozi) mama yangu yuko
wapi?
Lupemba:
Liliana… (Analia)
Liliana:
nini?
Bella:
(Analia)
Lupemba:
kila mtu
Liliana:
nini? (anaanza kuchanganyikiwa)
Lupemba:
amekufa…wamefariki
Liliana:
(anapiga kelele)
maaaaaammaaaaaaaaaa…uwiiiiiiiiii (anaweka
mikono kichwani)
Jirani:
maskini huyu mtoto
Liliana:
mama yangu mimi… (machozi yanamtoka)
Anna:
(Analia sana) babaaaaaaa
Bella:
baabaaaaaaaa
Lupemba:
(Analia sana)
Liliana:
(anachanganyikiwa)
Polisi:
tunaomba utulivu…miili haipo yaani ni majivu moto ulikuwa mkali sana
Liliana:
(Analia sana)
Polisi:
(kwa Lupemba) wewe ndo shahidi
tunaomba kama hautajali twende wote kituoni
Lupemba:
sawa
Liliana:
(kwa hasira) Lupemba
Lupemba:
naam…
Liliana:
njoo
Lupemba:
(anarudi alipo Liliana)
Liliana:
nani ameunguza nyumba ya mama yangu na kumuulia mama yangu ndani?
Lupemba:
Liliana tulia kwanza
Liliana:
(kwa hasira) nani?
Lupemba:
Robert
Liliana:
(anapiga magoti) Robert… (anapiga chini kwa hasira) lazima ufe
sitasubiri sheria mimi nitakuua kwa mikono yangu miwili Robert I swear you will
pay dearly…I swear... (kwa Lupemba)
usihangaike kwenda wapi wala wapi hii shoo niachie mimi nitaisimamia
Polisi:
binti acha sheria ichukue mkondo
Liliana:
sina muda wa kusubiri sheria… (anaanza
kulia tena) mama yangu amekufa mwezi mmoja kabla ya ndoa yake mama yangu
alikuwa ana furaha sana leo hii amekufa mama yangu mimi na mnaniambia nisubiri
sheria? Siwezi
Lupemba:
punguza hasira Liliana
Liliana:
hasira zangu zitaisha pale nitakapomuua Robert…lazima afe I swear lazima afee
Anna:
(Analia sana)
Bella:
(Analia)
Liliana:
msijali dada zangu huyu Robert kwangu mchache sana nitamuonyesha joto ya jiwe
mjinga sana huyu baba
Polisi:
(anaona aondoke zake)
Lupemba:
nipo na wewe Husna amefia humo…kipenzi changu amefia humo…siwezi kumsamehe Robert
halafu baada ya kuchoma nyumba akaondoka kwa madaha na dharau hata hakujutia
Liliana:
ninaenda kumuona
Anna:
huwezi kwenda ukiwa na hali hii
Liliana:
hii hali ndo nzuri sasa nikienda nimepoa sitamuonyesha upande wangu wa pili (anapanda gari na kuliondoa)
Bella:
Liliana
Liliana:
(analiondoa kwa fujo sana, baada ya
mwendo wa muda kidogo anafika katika jumba safi na la kifahari la Robert)
nimefika sijui ataniambia nini mimi… (anashuka
na moja kwa moja anaingia ndani)
Robert:
(anamuona anacheka kwa dharau)
nilijua tu utakuja…una ujasiri…vipi kafa au kaokoka kwenye ule moto?
Liliana:
wewe ni mpumbavu tena mpumbavu mkubwa
Robert:
I don’t care…Bianca kama hakuwa wangu ni bora nilivyomuua kuliko kumuona na
mwanaume mwingine hiyo ni adhabu yake kwa kunikataa mimi...kwani mimi nina
kasoro gani kwani hukumwambia uzuri wangu?
Liliana:
nitakuua Robert… I swear to you nitakumaliza kama ulivyomuua mama yangu na mimi
nitakuua Robert
Robert:
(anacheka kwa kejeli) maskini anaota
ndoto za saa nne usiku...huwezi hata kunisogelea sasa hivi unaongelea kuniua?
Liliana:
wanaume mna roho mbaya sana
Robert:
sana…hata Mungu alijua ndo maana hakutupa jukumu la kubeba mimba maana kama
tungebeba hao watoto wasingekuwa wanafikisha miezi tisa ingekuwa wanatusumbua
kidogo tunawaua… (anamalizia na kicheko
cha dharau)
Liliana:
I will kill you…
Robert:
rubbish (anacheka kwa kejeli)
Liliana:
you killed my mama… I will kill you
Robert:
whatever…I don’t care
Liliana:
mwezi mmoja baadae tarehe kama leo nitakuua Robert
Robert:
(anacheka kwa dharau) huniwezi halafu
kwa taarifa yako nimeona nimuue Bianca ili nafsi yangu iridhike…nilimpenda sana
Bianca nilikuwa tayari kumuacha mama Gabriel ili nimuoe Bianca lakini kila mara
nikimuangalia alikuwa hanitaki na pia alikuwa ananichukia sana…nikaona isiwe
kesi afe tu
Liliana:
nitakuua
Robert:
(anacheka) huniwezi Liliana…huniwezi
kiserikali huniwezi kichawi wala vyovyote hata ukienda polisi huniwezi Liliana
Liliana:
nani amekuambia naenda polisi? Wewe nacheza na wewe mwenyewe umeniulia mwanamke
aliyeyapa maisha yangu nafasi ya pili mwanamke pamoja na kujua mimi sio mwanae
wa kuzaa alinibeba na kunipenda kwa dhati
Robert:
embu toa blah blah zako hapa yaani hata kunisogelea unshindwa unawaza kuniua (anacheka kwa dharau) usinichekeshe bwana
Lilian:
time will tell
Robert:
mimi nikwambie tu kuwa pole sana kwa msiba ndugu yangu (anacheka kwa dharau)
Liliana:
wa kwako unakuja usubiri
Robert:
tutaona
Liliana:
we will see about that
Robert:
okay dogo... (anacheka kwa dharau)
Liliana:
(anafura kwa hasira) nitakuua I swear
Robert:
huwezi…tupinge na usiponiua nitakuua wewe
Liliana:
sawa…nitakuua mwezi mmoja baadae
Robert:
in your dreams baby
Liliana:
(anatoka kwa hasira)
Robert:
eti nitakuua… (anacheka sana) Mtu hata huwezi hata kunisogelea unaanzaje
kuniua?
Liliana:
(akiwa nje) I will surely kill him….
Nitamuua haki ya Mungu (anaondoka)
Robert:
(anaendelea na shughuli zake)
1 Comments
Usiondoke mdau mpaka uone mwisho WA mkasa huu... Asanteni kwa kuendelea kunisapoti
ReplyDelete