MUNGU MKUU 52


 

SCENE 52: -

KESHO YAKE ASUBUHI: -

NYUMBANI KWA WAZAZI WA MARY: -

(Vincent na Colton wanafika nyumbani kwa wazazi wa Mary)

Vincent: hodi humu ndani

Bibi: karibu baba

Vincent: shikamoo mama

Bibi: marahaba…

Dada yake Mary: karibu…

Vincent: habari yako

Dada: nzuri

Colton: shikamoo

(wanaitikia)

Vincent: Mary hajafika?

Bibi: ameenda kumuona mwanae jela yaani Analia tu …amekonda mwanangu yaani ila asante ni wewe ndo umesababisha tukamtafuta Mary

Vincent: nilitaka kumuona mwanangu

Colton: (amekaa kimya)

Bibi: na huyu ni mwanao?

Vincent: ndio…mtoto wangu wa kwanza kaka wa huyo bibie…ambae yupo jela au niende nikakutane na Mary

Colton: baba

Vincent: oh, okay nimekumbuka…

Dada: nini?

Vincent: hamna kitu

Dada: nimeona mnakonyezana

Vincent: usijali

Dada: niwaletee chai, maziwa au kahawa?

Vincent: usijali shem

Dada: hamnywi chochote?

Vincent: tumetoka tumekula kabisa… (anaangalia simu yake) Mary nae sijui yuko wapi

Dada: atakuja tu

Vincent: natakiwa kwenda kazini

Colton: msubiri tu dad atakuja

Vincent: (anakaa anatulia)

Mary: (anakuja) nimechelewa samahanini…za hapa jamani… (kwa mama yake) shikamoo mama

Bibi: marahaba mwanangu, mjukuu anaendeleaje?

Mary: yupo tu mwanangu...analia tu

Dada: hakuna jambo lililowahi kumshinda Mungu

Mary: hakika…asanteni sana kwa kunitia moyo (anakaa kwenye sofa nyuma ya kina Vincent) yule Vince?

Bibi: anakusubiri kaja na mwanae

Mary: (anawaendea) embu ngoja nikawaone

Colton: (anageuka kwa mshangao) aunt Mary

Vincent: unamjua?

Colton: namjua ndio...

Mary: (anawafikia na anamuona Colton) Colton???

Colton: ma mdogo

Vincent: mbona siwaelewi?

Mary: (anasikitika) kwanini umefanya hivi?

Vincent: eeh basi sina haja ya kuwatambulisha naona mnajuana

Colton: huyu ni mama yake Miriam binti niliyesababisha aende jela

Mary: unafanya nini hapa?

Vincent: jamani

Colton: nipo na baba yangu huyu hapa nimekuja kumuona mdogo wangu

Mary: Vincent ni baba yake Miriam

Colton: (anashangaa) kwa maana nyingine nimemkosea mdogo wangu?

Mary: yes...  kama wewe ni mtoto wa Vincent basi Miriam

Dada: makubwa…kwahiyo kaka kamsababishia dada makubwa?

Mary: ipo hivyo

Vincent: aisee hii dunia ndogo sana jana alipokuwa ananisimulia nikajua sijui nani yaani haya sikuwaza pamoja ya kwamba kulikuwa na uwiano kwenye hizi hadithi…mtoto wa Mary kwenda jela kwa kosa ambalo hakulitenda na Colton kumsingizia mtu na sasa yuko jela na kwamba zimepita wiki mbili pamoja na kufanana huko hata sikuwaza kama atakuwa mtu mmoja

Bibi: aisee…sasa wewe baba unamsaidiaje mdogo wako

Colton: (kwa Mary) naomba unisamehe mama

Mary: panga tu mipango ya kumsaidia baada yah apo ndo tutaanza kuongea

Colton: nitafanya ila nani atanisaidia?

Mary: Jeremy

Colton: mchumba wake Miriam?

Mary: ndio

Colton: ataniua akiniona

Mary: (anashusha pumzi)

Colton: ma mdogo kaongee kwanza na shemeji

Mary: hawezi kukufanya chochote…asante Mungu nimekuona Colton sasa mwanangu hatonyongwa asante sana Mungu wangu kweli umeonyesha UKUU wako jina lako litukuzwe

Vincent: (anawaangalia Colton na Mary kwa zamu)

Mary: nitamwambia Miriam

Vincent: tulia kwanza…yeye hatutamwambia kwanza...huu mpango tunapanga sisi sasa ni jeshi la kumsaidia binti yetu

Mary: asante Yesu

Vincent: tutapanga kwa ajili ya siku ya hukumu acha tuwaonyeshe kuwa tumeshindwa

Dada: hapo umenena shem

Vincent: (kwa Mary) mpigie mkwe tupange tunakutana wapi…

Mary: sawa

Colton: mimi sitaki kuonekana kwa dunia mimi tayari ni marehemu

Mary: tunakuhitaji lakini

Colton: najua na nipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha

Mary: asante sana...

Vincent: hilo limeisha

Bibi: Mungu hajawahi kushindwa

(wanaonekana kuwa na tumaini jipya)

Post a Comment

0 Comments