MUNGU MKUU 54


 

SCENE 54: -

END OF FLASHBACK: -

MAHAKAMANI KESI INAPOSIKILIZWA: -

(Colton anamaliza kusimulia ilivyokuwa mpaka amefika hapo)

Colton: ndo ilikuwa hivyo (kwa Miriam) naomba unisamehe na nipo tayari kwa adhabu yoyote itakayotolewa

Miriam: (anatikisa kichwa)

Colton: iam so sorry miriam...iam sorry my sister

Miriam: (Analia)

Mwanasheria 2: (anabaki anashangaa na haelewi yanayoendelea hapo)

Ariana: (anachanganyikiwa)

Keddy: (anamshangaa)

Ken: Ariana…

Ariana: (anacheka cheka)

Keddy: shida nini?

Ariana: kila nachofanya hakiwezekani kwa Miriam… (anapiga makofi) nilijua leo Miriam atahukumiwa kifo ila badala yake mimi ndo nimeumbuka mwenzenu…(anacheka) jamani nimeumbuka

Keddy: Ariana

Ariana: (kwa mama yake) nini? wewe si umefurahi?

Keddy: hapana mwanangu…najua natakiwa kukasirika kwa vitu ulivyomfanyia mwenzio

Ariana: sio mwenzangu na hawezi kuwa mwenzangu

Ken: Ariana Miriam ni mdogo wako

Ariana: sio ndugu yangu…wewe huwaoni ndugu zake? Baba na mama yake hao hapo na kaka yake huyo hapo wote wanampenda…mimi sijawahi kupendwa na mtu…tangu Mdogo nipo peke yangu kila mara mlikuwa mpo busy kumuomba Mungu awape mtoto mwingine…mlisahau kuwa na mimi nipo…baada ya Miriam kuja maishani mwetu mkasahau kuwa mimi ni mtoto wenu

Ken: Ariana sio kweli wewe ni mtoto wetu na tunakupenda sana

Ariana: sikuwahi kuona huo upendo…kila mara ilikuwa ni miriam yeye ndo alikuwa mtoto mzuri mwenye adabu na akili…

Keddy: sio kweli Ariana

Ariana: (Analia)

Ken: wewe umekuwa ni mtoto wetu mpendwa

Ariana: sio kweli baba na mama (Analia) nilifanya hayo sababu ya uchungu sana kila mara akili yangu ilijaa mawazo na moyo wangu ulijaa hasira

Keddy: uliamua kufanya hivyo ulisikia hasira mwanangu tulipomleta Miriam nyumbani hukumtaka tangu mwanzo ndo maana ulitengeneza chuki kwa Miriam…ungemkubali tu Miriam na pia tulikuwa tunasali maana tulikuwa tunakuona u mpweke sana kila kitu tulikuwa tunakuwaza na tulipomleta Miriam tulijua utafurahi kama ungempokea kwa upendo Miriam ungeona kila kitu kipo fair ni kwasababu uliweka ukuta ndo maana ulimchukia

Ariana: (anacheka kwa dharau) Zaidi ukaruhusu mapenzi ya Jeremy na Miriam

Ken: Jeremy na Miriam walikuwa wanapendana sana na hata kama ungeoana na Jeremy ndoa isingekuwa ya Amani

Ariana: tungependana tu

David: (anafika mahakamani hapo akiwa na mkewe)

Jeremy: (anawaona wazazi wake) njoo ukae hapa baba

David: kuna nini? Sikuja maana nilikuwa naona huruma sana

Jeremy: limeisha baba

David: afadhali

(wanaendelea kusikiliza)

Ariana: ni nyie wazazi wangu ndo mmesababisha nikawa hivi nimeishi kwa mateso sana na mwisho wangu ni mbaya sasa nini maana ya mimi kuwepo kwenye hii dunia?

Keddy: (Analia sana)

Ken: (Analia sana) mwanangu

Ariana: nachukia sana haya maisha nachukia jina langu najichukia hata mimi…hivi kwanini nilizaliwa? (Analia)

Watu: (wanamuangalia wengine kwa huzuni wengine kwa kumshangaa)

Miriam: dada (anamuendea Ariana) dada (anamkumbatia)

Ariana: (anamsukuma kwa nguvu) embu nitokee hapa nani dada yako? Mnafki mkubwa wewe

Jeremy: (anamdaka Miriam) are you okay?

Colton: (amekaa kimya)

Miriam: yes, iam fine

Ariana: sasa (anatoa bastola kwenye mkoba) nitajiua sasa hivi

Hakimu: (anagonga meza kuamuru utulivu)

Ariana: najiua hapa sasa hivi

Keddy: nakuomba mwanangu usifanye hivyo…nakuomba mama hili litaisha tutatafuta mwanasheria mzuri atakusaidia Ariana wewe kiri tu kosa utapunguziwa adhabu

Ariana: nilienjoi sana kuona mateso ya Miriam niligharamika sana kuona mateso ya Miriam sijuti wala nini afadhali mara moja tu maishani mwangu nimepata nafasi ya kufurahia… (kwa Miriam) I hate you nakuchukia sana wewe mwanaharamu

Ken: usimuite mdogo wako hivyo...

Ariana: kwani nasema uongo? wazazi wake walikuwa sio wanandoa mama yake alikuwa hawara ndo akazaliwa

Mary: usimtukane mwanangu

Ariana: oh, mama mwenye mtoto kaingilia (anacheka kwa dharau) I don’t give a damn (anafyonza)

Askari: (wanajiandaa kumkamata)

Araina: hata msijisumbue

Colton: (amekaa kimya)

Jeremy: (anamshika Miriam) hujaumia?

Miriam: sijaumia…please naomba umsaidie dada yangu

Jeremy: pamoja na yote aliyokufanyia umemsamehe?

Miriam: ndio Jeremy…

Jeremy: isingekuwa Mungu wewe sasa hivi si tungekuwa tunalia kwamba umehukumiwa kifo…

Miriam: hayo nayasahau Jeremy…

Jeremy: usimsogelee atakuumiza

Miriam: (anamsogelea Ariana)

Mary: (anamvuta kwa nguvu) Miriam…

Miriam: mama

Vincent: tulia Miriam…

Ariana: msinisogelee… (anataka kukimbia)

(Askari kadhaa wanamkamata na kumfunga pingu)

Ariana: niacheni

Askari: (wanampeleka gerezani)

Miriam: Ariana…

Colton: (anamuendea dada yake)

Miriam: kaka

Colton: (Anamkumbatia huku Analia) iam so sorry my sister

Miriam: it is okay dear brother…

Colton: tangu nimekuona siku ya kwanza nimekutendea yasiyo mazuri

Miriam: usijali ni mapito tu hayo kaka…namtukuza Mungu aliyelifumbua hili ingawa nasikitika kuwa kaka yangu utapata shida

Colton: nilijitakiwa mwenyewe acha nilipe

Miriam: iam so sorry brother…lakini tupo pamoja

Vincent: wanangu (anawakumbatia) asante Mungu Miriam upo huru sasa

Mary: (anafurahi sana) nimelia sana asante Mungu umesikia kilio changu

Keddy: hongereni sana

Mary: hongera kwetu sote

Miriam: (kwa Keddy) mama nisamehe

Keddy: oh, Miriam kwanini?

Miriam: kwa lolote

Keddy: hapana Ariana amevuna alichopanda

Miriam: oh mama

Keddy: (anatokwa machozi)

Jeremy: (anamshika bega Keddy) mama usilie

Hakimu: (anagonga meza kuamuru utulivu)

(utulivu)

Hakimu: baada ya kusikia hayo mahakama inamuachia huru Miriam Kenedy na kiumshikilia Bwana Colton Vincent Mshana na kumhukumu miaka mitatu jela kwa kosa la kushirikiana na Ariana Kenedy kwenye kuidanganya mahakama…kesi hii imefungwa rasmi

(Mwanasheria na Jeremy wanakumbatiana kwa ushindi)

Miriam: (hana raha pamoja na kwamba wameshinda hilo)

Ken: (analia sana)

Miriam: (anamfuata Ken) dad

Ken: (anamkumbatia) iam so sorry kwa mateso yote yaliyosababishwa na Ariana

Miriam: baba (anamkumbatia)

Jeremy: twendeni nyumbani mama kijacho

(wanacheka)

Askari: (wanamchukua Colton)

(wanabaki wakiwa na hisia mchanganyiko huzuni lakini pia furaha kwa kuwa UKUU wa MUNGU umejidhihirisha)

 

Post a Comment

0 Comments