SCENE
55: -
BAADA
YA MIEZI TISA: -
HOSPITALINI:
-
(Jeremy,
Vincent, Ken, Mary, Keddy wamekusanyika hospitali wanaonekana kuwa wanasubiri
kitu Fulani kama habari Fulani)
Jeremy:
(anakaa chini baada ya kuzunguka zunguka
kwa muda)
Keddy:
hatimaye umekaa mwanaume loh
Vincent:
(anacheka) bora…
Ken: (anacheka)
(wazazi wa Jeremy wanafika)
David:
bado tu?
Ken:
bado mwenzangu
Mama:
mbona imemchukua muda hivyo? Tangu jana usiku?
Keddy:
yaani nawaza kweli sijui yamemkuta yapi?
Mary:
Mungu atamsaidia
Jeremy:
nyamazeni kidogo mimi mnanichanganya mnajua?
Mary:
tulia baba
David:
kuwa na kifua unadhani kuwa baba wa familia ni lelemama
Mama:
kwani kasemaje?
David:
anachanganyikiwa yaani hii hali imchanganye?
Jeremy:
najaribu kutafakari baba
David:
eeh baba tafakari…
(wanacheka)
Vincent:
(anachungulia) nesi bado
Mary: si
usubiri mwanaume?
Vincent:
kwakweli imechukua muda… wewe bibi mwenye miaka 37
David:
bibi mdogo kuliko bibi wote duniani
Mary:
jamani ndo raha ya kuzaa ukiwa na miaka 17…miriam ana miaka 20 sasa hivi na
anajifungua Napata mjukuu
Keddy:
hongera shoga ree sio mimi miaka 45
Jeremy:
hata wewe ni bibi kijana
Keddy:
unanipa moyo?
Jeremy:
kwe… (anamuona nesi haraka anamuendea)
nesi
Nesi: (anasimama)
Ken:
nesi…
David:
tuambie basi
Nesi:
hongereni
Jeremy:
enhe…
Nesi:
amejifungua mtoto wa kike
(wanafurahi kupita kiasi)
Vanessa:
(anakuja) nimechelewa?
Jeremy:
(anamkumbatia Vanessa) amejifungua
mtoto wa kike
Vanessa:
(anaruka ruka)
Nesi:
mnaweza kumuona
(wanaingia kwa kukimbizana)
Miriam:
(bado dhaifu)
Jeremy:
(anamkimbilia na kumkumbatia) asante
sana (anamuangalia mtoto) oh so sweet
anafanana na wewe Miriam
Miriam: (anatabasamu)
David:
jamani mjukuu
(wanacheka)
Ken:
mjukuu
Vincent:
mjukuu
(wanacheka)
Miriam: oh,
asanteni kwa maombi yenu nimejifungua salama
Mary:
amen mama
Miriam:
natamani kaka yangu angekuwepo hapa…
Sauti: (kutoka nyuma yao) mtoto anaitwa nani
vile?
(wanageuka)
Vincent:
mwanangu
Colton:
(anakuja anawakumbatia)
Jeremy:
oh shemeji(anamkumbatia)
Colton: (anamkumbatia)
Miriam: oh,
Mungu amenipendelea leo nina furaha nimepata mtoto lakini pia kaka yangu
ametoka ila nina huzuni maana dada yangu
Keddy:
amechanganyikiwa
Miriam:
mama
Ken:
wamempeleka mirembe…akili yake sio nzuri alianza kama utani hatimaye akawa
chizi kabisa
David:
haya ni mapito na majaribu siku zote ni mtaji wa kuongeza Imani na Mungu
atakapokupa jaribu ni lazima akupe na mlango wa kutokea
Keddy:
hakika shemeji
Jeremy:
jamani leo ni siku ya furaha naomba tufurahie tafadhali
Ken:
yes, embu tufurahie
Vincent:
nina habari njema
Colton:
ipi tena?
Vincent:
mpo tayari kusikia?
Miriam:
tupo tayari...
Vincent:
mimi n Mary tumeamua kufunga ndoa
(wanafurahia)
Colton:
hongereni sana
Miriam:
hongereni sana…mwananngu amekuja na Baraka zake
Jeremy:
mtoto wetu
Ken: hii
ni habari njema sana...tuna harusi mbili sasa za kuandaa harusi ya Mary na
Vincent, Miriam na Jeremy
Colton:
Colton na Vanessa
Keddy:
leo tuna surprise nyingi jamani
Ken:
mlianza wapi na lini?
Colton:
wakati nipo jela ndo tulianza kupendana, alikuwa anakuja sana yeye na Miriam na
alikuwa nanionyesha huruma ya kutosha…niliona moyo wake mzuri alisema
atanisubiri hata ningekaa miaka 10 gerezani…
David:
tuna harusi tatu
Colton:
naomba nianze mimi na Vanessa
Miriam:
jamani mambo haya…Vanessa alikuwa rafiki yangu na sasa ni wifi yangu (anatabasamu)
Jeremy: yes,
baby...na Colton alikuwa adui yangu na sasa ni shemeji yangu
Keddy:
maisha bwana yanakuwa yana mambo mengi sana ila tunayaweza mambo yote katika
yeye atutiae nguvu
Miriam:
na anayetutia nguvu ni MUNGU pekee… (kwa Ken)
Dad dada Ariana atapona na kuwa mzima usisahau ukuu wa MUNGU
Ken:
nitausahau vipi ukuu wake?
Miriam:
(amebeba kichanga chake)
Mary:
kwahiyo mtoto anaitwa nani?
Miriam: Mary
Glory
Jeremy:
(anatabasamu)
Ken:
jina zuri sana
Colton:
jina zuri sana
Keddy:
nimependa jina
Mary:
napenda jina
Vincent:
(kwa Mary) huna lolote kisa linaanza na
Mary
(wanacheka)
Ken: God
bles you child
David:
wow jina lina utukufu linapendeza
Miriam:
ni Mary Glorify…namtukuza Mungu wangu kwa mambo makubwa aliyonitokea najua ni
yeye ndo aliyapanga lakini ninajisikia vizuri sana kwamba linionyesha ukuu wake
kwenye hilo hivyo namtukuza na ndo maana mwananngu anaitwa Glorify
Mama
Jeremy: hongereni sana kwa kupata mtoto wanangu
Miriam
na Jeremy: asante mama
Vincent:
jina zuri halafu lina upako
Ken: tuongelee
harusi inaanza ya nani?
Miriam:
baba na mama
David:
yeah sio mbaya halafu anafata Colton na Vanessa
(Colton
na Vanessa wanafurahi)
Keddy:
mwisho kabisa Miriam na Jeremy
Jeremy:
imekaa vizuri tuanze mipango sasa David: yes, mara moja…
Vincent
na Mary: (wanatabasamu)
David: (anambeba kichanga) njoo mke wangu…(anambusu)
Kichanga:
(kinajikunja na kucheza cheza)
0 Comments