SCENE 5
(Jumamosi nyingine tulivu, kila
mtu anaonekana yupo nyumbani na anafanya shughuli zake, Ariana anatoka chumbani
kwake akiwa amefura kwa hasira kutokana na uwepo wa Miriam)
Ariana:
yaani hili litoto silipendi kweli tangu lije sina raha na maisha yangu na
ninatamani hata kuliua
Miriam:(Analia sauti ya kichanga)
Ariana:(anaifata sauti hiyo na kugundua amelala
chumbani kwa wazazi wake) cheki linalala utasema limezaliwa humu (anambeba na kuondoka nae) sasa leo ndo
siku nitakayo liua hili litoto (anatoka
nae nje na kumpeleka mbali sana, anapofika machakani anamtupa na kurudi
nyumbani baada ya muda kidogo, anapofika nyumbani anagundua kuwa hakuna hata
mmoja aliyehisi kuwa mtoto hayupo) safi sana hakuna aliyegundua kuwa mtoto
hayupo
Keddy
:( anamjia) mwanangu…ulikuwa wapi
sijakuona nilikuja chumbani kwako sijakuona mama umekunywa chai?
Ariana:
hapana…shikamoo mama
Keddy:
marahaba mama hujambo?
Ariana
:( anatabasamu) sijambo…
Keddy:
wow…leo unaonekana una furaha kweli mwanangu niambie nini siri ya furaha yako?
Ariana:
nimeamka tu vizuri mama
Keddy:
safi au ndo umeamua kumkubali mdogo wako?
Ariana:
ndio mama nimeona tu nimkubali mdogo wangu na ninaahidi kumpenda kama mdogo
wangu wa tumbo moja
Keddy:
hongera dada Ariana kwa kubadilika huko…ninafurahi sana mwanangu (anamuita Mary)
Mary…Mary
Mary:(anaitikia sauti inatokea jikoni) abeee
dada
Keddy:
njoo usikie habari njema sana kwa leo jumamosi bwana ametuzawadia habari njema
sana leo
Mary:(huku anakuja) nini tena dada?
Keddy:
Ariana ameamua kuwa dada mzuri na ameahidi kumpenda sana mdogo wake kuanzia leo
Mary:(anaonyesha furaha) kweli?
Keddya:
muulize mwenyewe...
Mary:
eti mama ya kweli hayo?
Ariana:
ndio ma mdogo ya kweli kabisa…kuwa nimeamua kumpenda na kumthamini Miriam kama
mdogo wangu wa damu
Keddy:
wow, hii ni habari njema sana kwetu…yaani kila nikikuangalia mwanangu Napata
raha sana
Mary:(anafurahi sana tena)
Ken:(anakuja akitokea chumbani na kumkumbatia
mwanae ishara ya upendo) malkia wangu hujambo mama
Ariana:
sijambo baba shikamoo…
Ken:
marahaba mama yangu mzuri… (kwa Keddy na Mary)
nyie Miriam yuko wapi?
Keddy:(anacheka) masihala hayo mume wangu
Ken:
masihala ya nini tena?
Keddy:
wewe si umetoka chumbani baba na mtoto alikuwepo huko?
Ken:
hayupo nimetoka chumbani hayupo
Ariana:(anacheka kisirisiri)
Keddy:(anaonekana kuchanganyikiwa sana na habari hiyo)
what?
Mary:(anaonekana amehamaki sana) Mungu wangu
mwanangu…
Keddy:(anaenda chumbani kuangalia kama ni kweli)
Miriam… (anaangalia alipomlaza hayupo)
Mungu wangu jamani mwanangu kweli hayupo (anaanza
kulia)
Ken:(anamfuata
mkewe na kumkumbatia) come down honey
Mary:(anaanza kulia)
Ariana:(anawaangalia tu na wala hana hata wasiwasi)
Ken:
mara ya mwisho alikuwa wapi?
Keddy:(huku Analia) nilikuwa nimemlaza hapa
mume wangu jamani
Ariana:(anajisemea moyoni) yaani mama bwana
yaani mtoto sio mwanae lakini alivyomkomalia utasema ni mwanae wa kumzaa yaani
anashindwa kunililia mimi anamlilia huyo mbwa na bora hata nilivyomtupa hana
maana mshenzi huyo
Keddy:(kwa Ariana) Ariana mama mdogo wako
amepotea sasa sijui yuko wapi…
Mary:(anaendelea kulia kwa uchungu)
Ken:(kwa Mary) Mary…embu msaidie dada yako
kwenda kuuliza kwa walinzi huko labda waliona mtu kamchukua
Mary:
sawa shemeji… (anatoka kuelekea nje)
Ariana:(anacheka moyoni) yaani hata walinzi
hawajui kama nilitoka na huyo mtoto nilimtoroshea mlango wa nyuma (anacheka tena)
Mary:(anarudi ndani) hawajamuona hata wao
Keddy:
maskini mwanangu sijui atakuwa wapi…
Ariana:
ishi, yaani mama Analia kabisa kisa mtoto ambae hajamzaa?
Keddy:
madaktari waliniambia kuwa sina uwezo wa kubeba mimba tena Mungu akaonyesha
ukuu wake na kunipa mtoto kwa njia zake mwenyewe leo simuoni sijui yuko wapi…
Mary:(huku Analia) tutampata tu dada usijali
dada yangu
Ariana:
inamaana hicho kitoto kina nini mpaka kiwe kinapendwa hivyo? yaani na
mfanyakazi anamlilia utasema ni mwanae?
Ken:(huku anaelekea nje) ngoja nikatoe
taarifa polisi(anatoka)
Keddy:
mwanangu…jamani (anamuita Ariana)
mwanangu mdogo wako kapotea
Ariana:(anamuangalia tu na wala hana cha kumwambia)
Mary:
dada ngoja nikamuangalie nje hapo…sidhani kama atakuwa ameenda mbali
Keddy:
nenda mdogo wangu…mi sina hata nguvu za kutembea najisikia vibaya sana
Mary:usiwaze
sana(anajisemea moyoni)yaani huyu
mama anampenda mwanangu sana mpaka nafurahi(anaondoka
na kuenda nje na kuanza kuangalia huku na huku)sijui atakuwa wapi na bora
hata angekuwa ni mkubwa kwamba anatembea tungejiuliza kaenda wapi yaani hapa ni
wazi tu kwamba kuna mtu kamchukua lakini ni nani na kwa nini yaani sioni hata
adui nayemjua mimi anaweza kufanya hivyo au baba yake?lakini angejuaje yote
haya kwamba mtoto anakaa hapa hapana sijui ni nani amefanya hivi(anaendelea kumtafuta)mwanangu jamani(kwa mbali anasikia sauti ya mtoto mchanga)mwanangu(anakimbilia ilipo sauti anakuta ni Miriam)jamani
mwanangu(anamkumbatia na kumbusu sana)asante
Mungu…mwanangu haya twende kwa mama yako anakusubiri(anatoka anakimbia kurudi nyumbani baada ya dakika kadhaa anafika
nyumbani)dada,nimempata Miriam
Ariana:(anakasirika sana)
Keddy:
umemtoa wapi…?
Mary:
vichakani huko…
Keddy:
(kwa mshangao) vichakani? Kaendaje?
Mary:
hata sifahamu dada mimi nilikuwa natembea tembea nikasikia analia ndo
nikamchukua na kumleta huku
Keddy:
jamani sasa alienda kimiujiza au?
Mary:
hapo ndo sijajua dada nachojua ni kwamba nimempata huko
(Wanabaki wanaangaliana)
Keddy:
haya ndo yanaitwa maajabu ya Mungu na ukuu wake unashangaza jamani (anamchukua mtoto na kumbusu na kumkumbatia)
Ariana:(anajisemea moyoni huku anamuangalia Mary)
yaani lina kiherehere kweli nani aliliambia litoke humu ndani na likamtafute
huyu mtoto natamani nilibamize(anafyonza)
Keddy:
Ariana huyu hapa mdogo wako uliyesema utampenda na kumtunza
Ariana:(anaachia tabasamu la uongo)
Keddy:
ngoja nimpigie baba Ariana (anachukua
simu na kumpigia mume wake) hello baba Ariana
Ken:(anaonekana ndo anatoka kituo cha polisi)
naam mama…
Keddy:
mtoto amepatikana
Ken:
wow…. amepatikana wapi?
Keddy:
Mary kamtoa vichakani
Ken: (anashangaa sana) vichakani? Nani kampeleka?
Keddy:
sijui mume wangu
Ken:
(anaguna)
Keddy:
kikubwa tu mtoto amepatikana
Ken:
sawa ila lazima tujue mtoto kafikaje vichakani ina maana kuna mtu kampeleka
Keddy:
mimi naona tuachane na hilo mume wangu kikubwa tu tumempata
Ken:
sawa lakini nataka tu kujua
Keddy:
baba Ariana stop
Ken:
anyways sawa
Keddy:
(anacheka kidogo)
Ken:
umefurahi ee
Keddy:
sana baba
Ken:(anatabasamu) kama naliona tabasamu
lako mke wangu…basi ni sawa kama ni hivyo ngoja nitoe taarifa polisi maana
nilikuwa tayari nimeshawataarifu juu ya kupotea kwa mtoto wetu
Keddy:
waambie tumeshamuona
Ken:
sawa (anakata simu)
Keddy:(anatabasamu)
baba Ariana amefurahi pia
Mary:
(anatabasamu)
Keddy:
alitaka kujua mtoto kafikaje vichakani ila nimeona tu haina maana kikubwa
tumemuona
Mary:
kwakweli
Keddy:
(kwa Ariana) haya mbebe mdogo wako
Ariana:
(anambeba kishingo upande)
Mary:
(anamuangalia Ariana)
Ariana:
(anajichekesha)
Keddy:
kweli umefurahi kumuona mdogo wako
Ariana:
sana mama si nimekuambia kuwa nitampenda
Keddy:
nimekubali mwanangu
Mary:
hiyo imekaa vizuri
Keddy:
(anatabasamu)
(Wote
wanajikuta wanacheka kwa furaha kasoro Ariana anayeonekana kuchukia kupita kiasi,
na mara zote wakimuangalia anaonyesha tabasamu ambalo si la furaha bali la
kinafki na la kujilazimisha)
2 Comments
👏👏
ReplyDelete👏👏
ReplyDelete