SCENE
53: -
USIKU
WA SIKU HIYO: -
NYUMBANI
KWA JEREMY: -
(wazazi
wa Miriam wakiambatana na Colton wanafika nyumbani kwa Jeremy)
Jeremy:
(anafungua mlango) mama mkwe
Mary:
abeee baba
Jeremy:
mbona usiku sana kheri? (anaangalia
pembeni ya Mary anamuona Colton) Oh God… Colton? (anashangaa sana)
Colton:
za jioni shemeji
Jeremy:
shemeji?
Mary:
tunaomba uturuhusu kuingia ndani
Jeremy:
nakuruhusu wewe lakini sio huyu mnyama ni kwasababu yake mchumba wangu yupo
jela
Colton: ((kwa unyonge) iam so sorry
Jeremy:
tell me umefaidikiaa nini… (kwa ukali)
nakuuliza umefaidika nini?
Vincent:
msamehe ndo maana tumekuja kujua tunafanyaje
Jeremy:
mpenzi wangu anateseka kumbe wewe hukufa … (anachukia
sana)
Mary:
ndo maana tumekuja tujadili cha kufanya
Jeremy:
(anatulia)
Mary:
naomba utukaribishe baba
Jeremy:
karibuni (kwa Vincent) shikamoo
Vincent:
marahaba
(wanaketi)
Jeremy:
mtatumia nini?
Vincent:
mimi niko sawa
Colton:
hata mimi nipo sawa
Mary:
hata mimi nipo sawa tu
Jeremy:
(anakaa pembeni ya Mary) ndio mama
mkwe karibu
Mary:
huyu ni baba yake Miriam
Jeremy:
kumbe mlikuwa mnawasiliana?
Mary:
hapana alimkumbuka tu mwanae akaenda kwa mama yang undo wakanitafuta mimi…
Jeremy:
karibu baba mkwe…
Vincent:
asante mkwe
Mary:
cha kushangaza Colton ni mwanae
Jeremy:
(anashangaa sana) kwa maana nyingine
Colton ni kaka wa Miriam
Mary:
ndio
Jeremy: (kwa Colton) yaani this is incredible
and a perfect coincidence Miriam alihitaji muujiza na muujiza wenyewe ndo huu
Mary:
nini kifanyike?
Jeremy:
kwanza mimi nimshukuru Mungu kwa ukuu wake lakini pili iwe siri yetu tusiamini
mtu Colton atakuwa kadi yetu ya thamani sana siku ya hukumu
Mary:
kwanini siku ya hukumu
Jeremy:
nadhani ni nzuri Zaidi… (kwa Colton)
so nani alikuwa anakulipa?
Colton: Ariana
Jeremy:
nilijua tu
Mary:
ulijua? Ulijuaje?
Jeremy:
Miriam amekuwa akisema mara kwa mara kuwa jioni ile ni Ariana ndo alimpigia
simu…Miriam hawezi kudanganya…mdomo wake huongea ukweli tu
Vincent:
unampenda sana mwanangu
Jeremy:
nampenda sana Miriam baba mkwe yaani nampenda (anatabasamu kidogo) yeye ni
malkia wangu…
Vincent:
najisikia vizuri sana kusikia hivyo...
Jeremy: (kwa Colton) bado unawasiliana na Ariana?
Colton:
huwa ananipigia ila mimi huwa sitaki kumpokelea...aliniumiza sana alitoa damu
yangu alinikata niliumia sana
Jeremy:
pole sana
Colton:
kiukweli nahitaji mdogo wangu awe huru
Jeremy:
sawa...utaishi hapa kuanzia sasa hivi nitakuficha hapa akuna atakayejua upo
wapi
Colton:
sawa shemeji
Jeremy:
usijali…as long as unataka kumsaidia Miriam mimi nitakulinda
Colton:
usisahau kuwa mimi ni kaka yake ingawa nimefanya kosa (anasikitika kidogo) Miriam has to forgive me
Jeremy:
atakusamehe hana shida ila nataka kukuuliza Ariana alikupa sh. ngapi kufanya
haya?
Vincent:
(anainamisha kichwa)
Colton:
sikupewa hata mia mbovu shemeji yaani hata sijui kwanini au nini kilinifanya
nifanye haya…tena kibaya nimetenda kwa mdogo wangu
Jeremy:
naona kabisa unajutia sana
Colton:
kabisa shemeji nilianza kujutia baada ya kumsaidia Ariana lakini baada ya kujua
kuwa Miriam ni mdogo wangu nimejuta mara mia shemeji
Vincent:
nini hatima ya Colton kwenye hili
Jeremy:
(anakaa kimya kidogo)
Mary:
nini kitatokea kwa Colton baba
Jeremy:
sijui maana sio mtaalamu wa sheria ila navyoona ataadhibiwa sawa kabisa na Ariana
lakini yeye itakuwa kidogo na kama atakuwa na tabia nzuri itapunguzwa
Colton:
kwa vyovyote shemeji mimi nipo tayari kwa adhabu yoyote nilifanya vile kwa
sababu ya mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa Ariana (anasikitika) yalinipeleka
pabaya
Jeremy:
aisee
Vincent:
mkwe tusaidie
Jeremy: haina shida tutafanya juu chini hata
kama ataenda jela hatakaa sana…tuna mwanasheria mzuri
Vincent:
asante mkwe
Jeremy:
tupo pamoja
Colton: Ariana
ananipigia simu sana nimjibuje
Jeremy:
akikupigia pokea akikuomba mkutane kutana nae
Colton: (anakaa kimya)
Jeremy:
atajaribu kukuua nitakupa bullet proof hautadhulika
Colton:
asante sana shemeji kwanza kwa kunisamehe
Jeremy:
usijali tupo pamoja maadamu umekiri mimi nashukuru na kufurahi kwa ukiri wako
Colton:
asante shem
Mary: (anatabasamu)
Vincent:
tuungane kumsaidia mpendwa wetu
Mary:
bila shaka
Jeremy:
bila shaka baba mkwe
Vincent:
(anatabasamu kidogo)
(wanaendelea na
maongezi yao)
0 Comments