SCENE
4: -
(Patrick
yuko ofisini kwake anafanya kazi zake za kila siku, wakati huo mlango wa
ofisini kwake unagongwa)
Patrick:
ingia mlango uko wazi
Mtu:(anaingia
kisha anasimama mbele yake)
Patrick:
karibu… (ananyanyua kichwa anatabasamu mara baada ya kumuona mgeni wake)
wow…Edwin…
Edwin:
nambie…
Patrick:
rafiki yangu muda mrefu sana ulipotelea wapi my brother…
Edwin:mi
nipo bwana… (anavuta kiti kisha anakaa)
Patrick:
dah!!!sio siri nimefurahi kukuona Edwin…rafiki yangu wa miaka mingi jamani
Edwin:
hata mimi nimefurahi kukuona my friend…how is London...
Patrick:
pako poa tu my friend…how is South Africa?
Edwin:
pako very fine my friend yaani pako poa kuliko kawaida…
Patrick:
eti eeh…that’s very good…
Edwin:by
the way nambie…my friend una jipya gani maishani mwako maana ulinipigia simu
una hamu kweli ya kuniona
Patrick:
kama ulivyosema tu kuwa nilikuwa na hamu ya kukuona
Edwin:
kwanini
Patrick:
nilikukumbuka na pia nilitaka kukuambia kuwa iam in love
Edwin:
wow…really
Patrick:
yes…I love her so much kiasi kwamba nataka awe mke wangu…nitamuoa huyu
dada…just nasubiri atulie
Edwin:
what do you mean atulie?
Patrick:
ana majukumu mengi sana na akili yake haijawa tayari kuwa mke wa mtu maana
anaona kama akiolewa atamuacha mama yake katika hali ambayo si nzuri
Edwin:
kwanini usimsaidie afikie hayo malengo haraka ili sisi tule ubwabwa
Patrick:(anacheka)
nipo kwenye hatua za mwanzo kumsaidia, nampenda na ninamthamini sana
Edwin:(anacheka
kidogo) sijawahi kukuona ukimuongelea mwanamke jinsi unavyomuongelea huyu
mwanamke
Patrick:
she is so perfect for me yaani ni bonge la demu…mpole, mpenda watu, anayafanya
majukumu yake kwa moyo, yaani kwa kifupi anafaa kuwa mke…
Edwin:
nataka nimuone huyu dada, anaitwa nani?
Patrick:
Olivia…
Edwin:
ana jina zuri sana nimelipenda…mlikutana wapi?
Patrick:
instagram…alini follow, akawa ana comment sana picha zangu mwisho wa siku
tukaanza kuchat…sikujua kuwa anaishi Mwanza so nilipotoka London nikamwambia
kuwa tukutane Mwanza akasema huku ndiko anapoishi, nilifurahi kumuona kwa mara
ya kwanza, she is so beautiful
Edwin:
naomba nimuone kama una picha yake hapo
Patrick:
nakosaje picha yake kwa mfano (anachukua simu yake kisha anamuonyesha rafiki yake)
huyu ndo malkia wangu…kipenzi cha nafsi yangu
Edwin:(anaiangalia
ile picha kisha anang’ata midomo na kulamba midomo yake kama mtu aliyetamani
kitu anachokiona) oh…My God, she is so beautiful…naomba nimuone kwa macho
kabisa
Patrick:(anacheka
kidogo) kwani hapa humuoni kwa macho…
Edwin:
No..No…yaani nataka nimuone live bila chenga
Patrick:
usijali my friend…Jumamosi huwa napenda kwenda nae migahawani ili tukae pamoja
sasa siku ya jumamosi ndo utamuona shemeji yako
Edwin:
Jumamosi mbona mbali sana
Patrick
:( anamtania) mbona una hamu ya kumuona mke wangu umemtamani nini?
Edwin:
hapana…kwanini useme hivyo? Nataka tu kumuona kwanini ameuchukua moyo wako
hivyo?
Patrick:
nakutania…(anacheka)najua huwezi kunichukulia mwanamke nimpendae kwa
dhati…wewe ni kama kaka yangu wa damu
Edwin:
uko sawa kabisa Patrick…siwezi kumtamani na wala kumuangalia mwanamke
uliyemchagua maana wewe ni kama mdogo wangu wa damu…na pia umeshanisaidia vitu
vingi sana my dear
Patrick:
that’s right my brother cha kufanya tu ni kuombeana ili mimi na Olivia wangu
tufunge ndoa
Edwin:(anajichekesha
sana) haina shida my brother
Patrick:
by the way umefika tu nikaanza stori zangu za mwanamke wangu mpya…
Edwin:
No, it is ok najua ulifurahi sana…maaana navyojua wewe mdogo wangu hujawahi
kabisa kupenda mtu hivi…mara nyingi ulikuwa unachezea tu wadada wa watu
Patrick:
tulikuwa tunachezea wote…hukumbuki hata wewe ulikuwa na hizo…au mpaka leo bado
una katabia ka wanawake…niambie ukweli maana sijakaa na wewe siku nyingi mimi
baada ya msiba wa wazazi wangu nikaenda London na wewe ukaenda South Africa
basi hata hatukuonana tena…
Edwin: yes,
my brother hatukuonana tena na nilikua na kukumbuka sana makeke yako na jinsi
ulivyokuwa unatumia pesa kupata wanawake, najua na huyu umetumia pesa nyingi
sana
Patrick:
huyu yeye imekuwa tofauti…nilipokuwa London nilikuwa simtumiii pesa na wala
hakujua kama naweza kuwa nina pesa nyingi kiasi hiki…kwahiyo alinikubali
tu…hivyohivyo na hata mar azote nilipokwa nakuja na kumsalimia sikuwahi
kumuonyesha kuwa nina pesa so alinikubali hivyo hivyo…kwahiyo nilipoona hivyo
nikaamua kumweka maanani…so she is wife material
Edwin:
hongera sana kwa mwanamke mpya mpya my brother, mwenzio sijapata hata mpenzi
Patrick:
don’t give up my brother, Mungu ni mwema siku zote atakupa tu
Edwin:ni
matumaini yangu pia
Patrick:
ok…what would you like…soda, beer au wine?
Edwin:
unajua napenda shampeni
Patrick:
ok… (anachukua simu yake ya mezani kisha anampigia sekretari wake)
nambie Mary…naomba utuletee waini ofisini
Sekretari:
sawa boss
Patrick:
enhe!!!nambie…mbona umepoa huna yake makeke yako my brother…
Edwin:
maisha magumu sana my brother, sina mpenzi
Patrick:
ah!!hiyo isikupe tabu mbona wanaake ni wengi sana
Sekretari:(anakuja
na wine pamoja na glasi za wine mbili kisha anaziweka mezani kisha
anawakaribisha halafu anaondoka)
Patrick:
unaweza ukamchukua hata huyu yuko vizuri sana
Edwin:
nataka kama wako
Patrick:
yupo rafiki yake yaani wapo kama mapacha… (anamimina waini kwenye glasi kisha
anampa Edwin)
Edwin:(anapokea)
waambie jumamosi waje wote
Patrick:
hiyo itakuwa sawa kabisa…ngoja nitamwambia…aje nae Jumamosi
Edwin:(ananyanyua
glasi) cheers…
Patrick:
cheers…
(wanagonga
glasi zao huku wanaonekana wana furaha sana)
Patrick:
oh… (anaangalia simu yake) simu inaita, na ni shemeji yako(anapokea)hello
baby…
Olivia:
nambie honey…I miss you so much…
Patrick:
I miss you too…my queen
Olivia:(anacheka)
Patrick:
nambie mbona huongei unacheka tu mama
Olivia:
uko wapi?
Patrick:
ofisini my dear…nafanya kazi
Olivia:
ok…mi nipo nyumbani na mama
Patrick:
mnafanya nini?
Olivia:
tunaangalia runinga…flat screen…mpya na upya wake
Patrick:
wow (anacheka kidogo) …na je tayari mafundi wameshajenga choo cha ndani?
Olivia:
ndio mume wangu
Patrick:
afadhali maana dah!!nilikuwa Napata tu wivu kila nikifikiria kuwa huwa unaenda
kuoga nje na khanga moja dah
Olivia:(anacheka
tena) yaani wewe una matatizo sana
Patrick:
huwa nina wivu sana yaani hiyo ndo kasoro yangu
Olivia:
nakuahidi sitakupa sababu ya kuwa na wivu my love
Patrick:
asante sana…my love
Olivia:
asante darling na pia mafundi wamekuja kuweka uzio ndo wanamalizia, walianza
jana leo wanamalizia
Patrick:
asante mama…you are the queen; I have always wanted to keep in my palace yaani
wewe ni malkia niliyekuwa namtaka katika himaya yangu
Olivia:
I promise to never let you down my King
Patrick:
I love you
Olivia:
I love you too king
Patrick :(
anakata simu kisha anatabasamu)
Edwin:
kweli hapo nimekubali kwamba kweli unampenda huyu dada…yaani mpaka nyumba yao
umeona uanze kuikarabati…kweli ni kipenzi cha nafsi yako, umekamatika kijana (anacheka)
Patrick:
(anacheka) haswaaaa—binti amenikamata lakini nimefanya hivyo maana
nataka nimuoe
Edwin:
cheers to that…
Patrick:
cheers
(Wanaendelea
kunywa vinywaji vyao huku wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale)
Edwin:
Patrick unataka kuoa?
Patrick:
exactly…nimempata the right person kwanini nivunge? Naoa mwenzenu yaani naoa
kabisaaaa kama nimepata niliyemtaka kwanini nichelewe?
Edwin:si
ndo hapo? ila lazima niseme kila shetani na mbuyu wake na wewe mbuyu wako ni
huyu demu…Duh mpaka ume surrender kabisa? huyu dada kakupa nini?
Patrick:
yaani, sijui kanipa nini jamani …sijui kaniroga(anacheka)
Edwin:
itakuwa, Patrick huyuhuyu wa kuchezea watoto wa watu leo umependa baba…noma
sana na ulikuwa unabadilisha mademu wewe (anacheka)
Patrick:
watu hubadilika bro we huamini hilo?
Edwin:
naamini na nakupongeza sana
Patrick:
cheers to that
edwin:
cheers
(wanagonga
glasi huku wanaendelea na mazungumzo yao)

0 Comments