SCENE
5: -
(Olivia
amekaa sebuleni kwao na rafiki yake kipenzi aitwae Monica, wanapata vinywaji
baridi huku wakibadilishana mawazo mawili matatu.)
Monica
:( anaguna) shoga danga ulilolipata shoga usiliache…
Olivia:
sio danga huyo shoga yangu ni mwanaume ninaempenda kwa dhati na ninatamani sana
anioe
Monica:(anakunywa
kinywaji kidogo) aisee maana kapabadilisha kwenu ndani ya siku kadhaa tu
kila kitu kipo sawa ona jamani hadi raha
Olivia:
ndo hivyo shoga yangu mwanaume wa hivyo unaanzaje kumuita danga?
Monica:
kwakweli
Olivia:(kimya
kidogo huku anakunywa soda yake taratibu)
Monica:(anaonyeshea
runinga kubwa iliyokuwepo sebuleni hapo) na hiyo TV kakununulia yeye
Olivia:
ndio hata haya masofa yeye ndo aliniletea na bado mama anatakiwa kwenda
kutibiwa Nairobi mwezi ujao
Monica:
wewe huyo mwanamume mbona bonge la kitu shoga yangu mi mbona sipati wa hivyo?
Olivia:(anacheka)
jamani…utapata tu wakati wako bado haujafika
Monica: huyo
mumeo ni mtu mzima?
Olivia:
sio sana ana miaka 35
Monica:
ametoa wapi mali zote hizo? mbona bado mdogo sana?
Olivia:(anacheka)
Monica:
asije akawa jinni…maana si uliniambia mlikutana instagram
Olivia:
ndo hivyo shoga yangu
Monica:
mwenzangu jinni hilo…
Olivia:
hamna bwana (anacheka) yaani anasali sana
Monica:
ana vituo vya mafuta…sijui vingapi
Olivia:
vitatu…tu jamani
Monica:
sasa vichache hivyo…sijui na mabasi mangapi
Olivia:
matano…
Monica:(anaguna)
embu nimuone si una picha zake…
Olivia:
nyingi sana
Monica:
nionyeshe…
Olivia:(anachukua
simu yake aina ya iphone kisha anamuonyesha picha ya Patrick)
Monica:
shoga…mbona mwanaume mtamu hivi…mzuri hivi…yaani umepata mwanamume ana kila
kitu…halafu mrefu huyu yuko vizuri sana kwenye mambo yetu yaleeee
Olivia:
umeanza(anacheka)yaani huwezagi kuacha kuongea ujinga rafiki yangu
Monica:
halafu kakununulia simu nyingine mpya na upya wake… (anampa glasi) embu niongezee
kinywaji nijinywee hapa
Olivia:(anaipokea
glasi, anasimama kisha anaelekea jikoni)
Monica:(anajisemea
moyoni) mwanaume ana kila kitu huyu, cheki alivyo mzuri
Olivia:(anarudi
na kinywaji anampa kisha yeye anachukua cha kwake kisha anaendelea kunywa
taratibu)
Monica:
halafu si huwa anaenda London sana…?
Olivia:
ndio…kuna biashara aliachiwa na wazazi wake ndo huwa anakuwa anaifanya
Monica:
biashara gani
Olivia:
siwezi kukuambia sasa hivi…
Monica:
niambie bwana au madawa ya kulevya…?
Olivia: hamna…sio
madawa ya kulevya…dhahabu…
Monica:
dah…huyu mwanaume ni noma sana
(mama
anakuja wakati huo wapo bado wapo kwenye maongezi)
Olivia:
shikamoo mama
Mama:
marahaba mama…
Monica:
shikamoo mama
Mama:
marahaba mwanangu… (kwa Olivia) mwenzio nanakutafuta sana mbona
hupatikani
Olivia:
Patrick ana vituko mimi mbona simu yangu ipo hewani
Monica:
labda mtandao…
Mama:
chukua simu yangu umpigie… (anampa kisha anaondoka) ukimaliza niletee ndani
(anaingia ndani)
Monica:
bonge la simu la mama
Olivia:
kaletewa na mkwe wake (anapiga simu ya Patrick inaita mwisho inapokelewa)
honey…
Patrick:
mambo…
Olivia:(anatabasamu
kidogo) poa…
Patrick:
hupatikani
Olivia:
nisamehe baby
Patrick:it
is okay…sasa Jumamosi…naomba uje na rafiki yako maana na mimi nakuja na rafiki
yangu…yaani anatafuta mchumba yaani pamoja na pesa zake hajapata mwanamke
anasema kuwa Mungu amenijalia mwanamke mzuri hivyo nay eye anataka mwanmke
mzuri kama wewe na mwenye akili ya maisha nikamwambia kuwa na wewe una rafiki
yako mnafanana kama mapacha so akasema kuwa anataka kumuona hivyo njoo nae sawa
ee
Olivia:(kwa
Monica) Mungu kakusikia…jumamosi tutaenda kukutana na rafiki yake Patrick
na yeye anatafuta mchumba kama wewe
Patrick:(anacheka)
kumbe yupo hapo eeh
Olivia:
yeah…
Monica:(anacheka)
Patrick:
basi poa tutawakutanisha jumamosi
Olivia:
wazo zuri…sana
Patrick:
enhe mambo mengine?
Olivia:
nimekumisi bae…
Patrick:
ofisini unapajua…nyumbani unapajua…pale kwenye kitimoto unapajua unashindwa
kuja?
Olivia:
njoo wewe…
Patrick:
duh…mama yupo hapo mi naona aibu bwana
Monica
:( anamuangalia Olivia)
Olivia:(anacheka)
we njoo kwanza yeye siku hizi anashinda ndani anaangalia tamthilia zake za
kihindi zilizotafsiriwa
Patrick:
sawasawa ana Amani sasa hivi ee
Olivia:
saaaana…asante baby
Patrick:
usijali, you are my wife lazima nikuangalie wewe na uwapendao…
Olivia:
I love you Patrick
Patrick:
I love you my queen
Olivia:
baadae...
Patrick:
baadae (anakata simu)
Olivia:(anashusha
simu na kuiweka mezani)
Monica:
mnapendana kweli…hadi raha
Olivia:(anacheka)
Monica:
mna muda gani now…
Olivia:
mwaka tayari…maana tumeanza kuchati muda mrefu sana…baadae tukaja kuonana
halafu akarudi London...amekaa kule muda mrefu juzijuzi ndo amerudi
Monica:
anarudi lini London
Olivia:
bado sana
Monica:
haya…bwana una bahati mara nyingi watu wakikutana mitandaoni wanachezewa kisha
wanaachwa solemba ila kwako jamaa anaonekana kapagawa kabisaaaa
Olivia:(anacheka)
yote ni mipango ya Mungu...si unakumbuka nilivyohangaika na mahusiano
Monica:
nakumbuka vizuri sana…
Olivia:
kwahiyo Mungu yupo na anatenda
Monica:(anaguna)
kwako tu…
Olivia:
usikate tamaa rafiki yangu, twende hiyo jumamosi tuone Mungu kakuwekea
nini…maana Patrick anasema hata huyo rafiki yake anatafuta mwanamke muda mrefu
ila hajapata…twende shoga yangu
Monica:
ndo uniazime nguo
Olivia(anacheka)usijali
shoga yangu
Monica:(anacheka)
twende mwaya nikamuone shem kwa macho
Olivia:
poa…cheers…to our men
Monica :(
ananyanyua glasi) cheers... (Anagonga glasi)
(Wanacheka
huku wanaendelea kunywa vinywaji vyao)
Olivia:
twende tukapike jikoni
Monica:
poa
(Wananyanyuka
wanaelekea jikoni ili wapike wanapofika huku wanaanza kupika huku wanaonekana
kufurahiana, wanapika huku wanakunywa vinywaji na mazungumzo pamoja na vicheko
vinaendelea)
Monica:
naona shoga yangu hata mama yako anasikia raha si kwa kubadilika huku…loh
Olivia:
acha tu shosti…nampenda na kumheshimu Patrick kanitoa mbali huyu kaka (anaguna)
Monica:
tena mbali sio kitoto (anacheka kimbea) si na mimi litokee danga
linibadilishe maisha?
Olivia:
Mungu ni mwema sana rafiki yangu, atatokea tu wala hata usijali
Monica:
eti ee
Olivia:
nyumba ilikuwa imeparama nyiee—Mungu huyu achene aitwe Mungu
Monica:
nakumbuka shoga yangu sasa hivi imekuwa tamu hiyo…(anaguna)
Olivia:
ndo hivyo kila jambo na wakati wake…kuna wakati wa kuvuna na kupanda…
Monica:
mwenzangu huu kwako ni wakati wa kuvuna, sijui shoga ulipanda lini ila unavuna
ona nyumba ilivyo tamu
Olivia:
acha tu
(wanacheka
huku wanagonga mikoo)
Monica:
shoga mwanaume umepata…tena mwenye roho yake(anaguna)
Olivia:
namshukuru Mungu sana jamani

0 Comments