SCENE
3: -
(ni
asubuhi nyingine nzuri na njema, ndege wa angani wanaruka ruka wakimsifu Mungu
na uumbaji wake, Patrick yupo bustanini kwake amekaa ametulia, anakunywa chai
huku anafuatilia habari mbalimbali kupitia simu yake ya mkononi, wakati
anaendelea kupitia mawili matatu anapata wazo la kumpigia mpenzi wake simu)
Patrick:
ngoja nimpigie baby simu kwanza nimemkumbuka tangu jana mchana tulipoachana nae
sijamuona tena (anaweka simu yake sikioni inaita mwisho inapokelewa) my
Queen
Olivia: yes,
my king, bado umelala?
Patrick
:( anacheka kidogo) huwezi amini nilitaka kukuuliza hivyo pia umefanya
kuniwahi, sijalala nipo bustanini nakula upepo mwanana huku ninakunywa chai
vipi wewe umelala?
Olivia:
hapana nipo tu, nimetoka kuoga
Patrick:
njoo nyumbani kuna vitu nataka tuzungumze…
Olivia:
sawa…nakuja
Patrick:
nikupe dakika ngapi? au nimwambie dereva wangu aje akuchukue?
Olivia: hata hivyo ni sawa pia
Patrick:
tukupe muda gani utakuwa umemaliza kujiandaa?
Olivia:
dakika kumi na tano
Patrick:
utakuwa umemaliza kujiremba kweli?
Olivia:
kabisa
Patrick:
basi sawa, ngoja nimwambie aje akuchukue
Olivia:
poa (anakata simu)
Patrick :(
anamuita dereva wake) Edrick...
Edrick
:( anakuja mbio mbio) naam boss
Patrick:
nakupa namba ya mtu hapa, umpigie akueleze yuko maeneo gani umchukue umlete
nyumbani hapa, ni shemeji yako(anacheka)halafu nishakwambia usiwe
unaniita boss jamani
Edrick:
samahani boss
Patrick:
umeniita tena boss…
Edrick:
samahani Patrick
Patrick:
hapo sawa, ngoja nikutajie namba ya shemeji yako utampigia... (Anamtajia)
Edrick
:( anaichukua kisha anaihifadhi) sawa mdogo wangu ngoja nikamchukue
shemeji yangu
Patrick
:( anacheka Sana) poa kaka yangu
Edrick
:( anaondoka nae huku anacheka)
BAADA
YA DAKIKA ISHIRINI
(Edrick
anarudi akiwa na Olivia, wanapofika wanaegesha gari kisha Olivia kwa madaha
anashuka kwenye gari la kifahari la bwana Patrick Kalenzi ambae ni mpenzi wake)
Patrick
:( anamuona) wow…Queen Kumbe ni Zaidi ya mzungu ee
Olivia
:( huku anamuendea) kwanini?
Patrick:
umeniambia dakika kumi na tano kweli zikawa hivyo
Olivia:
hapana baby, zimezidi kama dakika tano (anafika alipo Patrick)
Patrick:
sio mbaya (anambusu mdomoni kisha anamkumbatia) karibu nilikuwa
nimekukumbuka kweli Jana tulipomaliza shopping nikakuacha nyumbani sikukuona
tena Jana hata dinner ulikataa kula na mimi
Olivia:
nilikuwa na mama si unajua mama anaumwa sana so inabidi mara nyingi nikae nae
Patrick:
anyways sawa hiyo haina shida, karibu ukae mi nilikuwa nakunywa chai
Olivia
:( anatabasamu kisha anakaa karibu kabisa na alipokaa Patrick) nambie
Patrick:
karibu tunywe chai…nenda jikoni waambie wakupe unachotaka then tuje tukae hapa
mi huwa napenda sana kukaa hapa patulivu sana
Olivia:
napaona ni pazuri sana...ila mwenzio nishakunywa chai
Patrick:
poa basi hata juisi au hata maziwa basi fanya hivyo, ili nafsi yangu itulie
jamani sweetheart
Olivia:
sawa usije ukalia…(anacheka)
Patrick
:( anacheka)
Olivia
:( anaenda jikoni na baada ya muda anarudi akiwa amebeba juisi ya embe)
sasa naona utafurahi
Patrick;
hapo sawa, kwanza sisi hapa mgeni akija natakiwa awe mwenyeji wakati huohuo,
umewakuta kina dada Halima?
Olivia: wapo...
Patrick:
yaani hapa ni kujichotea tu hakuna mtu wa kukuuliza
Olivia:
wow…mnaishi vizuri sana,
Patrick:ni
jambo zuri sana kuishi hivyo maana unaweza kusema kuwa unamtesa mwanadamu
mwenzio na je siku akiamua kukupokonya kila kitu alichokupa? anapokonya wewe
anampa huyo uliyekuwa unamuona hafai utafanyaje? ni muhimu sana baby kuwa na
roho ya Wema ili hata siku huna watu watakukumbuka kwa ule wema ingawa si kwa
asilimia kubwa ila tu watakukumbuka na hata Mungu atakuhurumia, jifunze kukaa
na mtu na kumchukulia na ukipata nafasi ya kumsaidia msaidie…hiyo nayo ni zaidi
ya sadaka.
Olivia:
nakupenda Patrick, we ni mtu wa pekee sana.
Patrick:
usije tu kunisaliti, nitajiua, nauogopa usaliti sana na Zaidi nauchukia usaliti,
kama umeamua kunipenda wewe nipende na kama umeamua kunipotezea muda nambie na nionyeshe mapema ili nijitoe mapema kabisa…
Olivia:
usijali mpenzi wangu sitawahi kuja kukusaliti
Patrick:
na ukifanya hivyo?
Olivia:
siwezi hata kufikiria nakupenda sana na kama nikifanya hivyo basi niache
Patrick:
haya ni vyema ulivyojichagulia adhabu ila hiyo kama utanisaliti ndo nakuacha
lakini kama hujanisaliti…nitakupenda na kukutunza milele
Olivia:
nakupenda
Patrick:
nakupenda Zaidi
Olivia :(
anamlalia begani)
Patrick:
tupendane mpenzi wangu
Olivia:
Mungu atusaidie
Patrick:
atatusaidia unadhani anakawia kuwasaidia watu wake? (anabadilisha mada)
baby…mimi kuna vitu nataka nikufanyie mimi kama mpenzi wako,
Olivia:
vitu gani?
Patrick:
kwanza kabisa kuifanyia matengenezo nyumba yenu lakini cha pili nikufungulie
biashara au nikusomeshe chagua kimoja kati ya masomo au biashara
Olivia;
baby, uko serious unataka kunifanyia hayo?
Patrick:na
Zaidi mpenzi wangu, mimi nimekupenda sana maana kwanza unaonekana una akili sana,
unapambana kwa ajili ya mama yako kweli wewe ni mwanamke unaefaa sana kuitwa
mke
Olivia:(anacheka)
asante my love ni lazima nipambane kwa ajili ya mama yangu, kwake yeye ni mimi
t undo ndugu yake hana mume, kaka wala dada kwahiyo inabidi nipambane tu
Patrick:
hicho ndio kilichonifurahisha kwako wewe ni jembe, sasa mimi nataka nikusukume
uzikaribie ndoto zako
Olivia:
nitashukuru Sana mume wangu
Patrick:
I love you
Olivia
:( anambusu mdomoni)
Patrick:
kazi utakayo nifanyia ni kuandika kwenye karatasi wapi panahitaji matengenezo
na gharama zake na pia utanipa jibu kuwa umechagua nini kati ya masomo au
biashara na gharama ya kitu ulichochagua sawa ee
Olivia:
sawa
Patrick:
nivipate mapema ili nipange bajeti zangu
Olivia:
ok baby Leo nitaenda kujadiliana na mama tuone tutahitaji kiasi gani
Patrick:
sawa malkia wangu…
Olivia :(
anatabasamu huku anamuangalia mpenzi wake usoni)
Patrick:
mbona unaniangalia Sana unataka kunikariri au?
Olivia:
hapana naangalia tu ukuu wa Mungu, nimeteseka sana na maisha ila ghafla tu
ukatokea wewe,
Patrick:
njia za Mungu hazichunguziki yeye akipanga amepanga na hakuna mtu hata mmoja
ambae anaweza kupangua hata iweje
Olivia:
namwamini sana Mungu wangu, Mungu aliyewavusha waisraeli kwenye bahari ya shamu,
namtukuza kwa mambo yake makuu
Patrick:
hata mimi namuamini sana Mungu, Mungu aliyemlinda Daniel kwenye shimo
lililokuwa na simba wakali, namuamini Mungu wa Ibrahim, Isaka na Jacobo
Olivia:
wow…unaijua biblia baby
Patrick:
mimi mlokole
Olivia:
kweli?
Patrick:
sana
Olivia:
nitakuwa nakupitia kila Jumapili ili twende kanisani
Patrick:
sawa…nitakuwa nafurahi sana
Olivia:
kweli
Patrick:
Sana
Olivia:
mama atafurahi sana
Patrick:
anapenda walokole ee
Olivia:
yeye mwenyewe mlokole
(Mazungumzo Yao yanaendelea kwa muda huku kila
mmoja wao anaufurahia uwepo wa mwenzie)
Patrick:
kwahiyo Andika nilivyokuomba tuone naanzia wapi
Olivia:
sawa la azizi
Patrick:
na jibu kwamba unataka kufanya nini kati ya masomo au biashara au tunaweza
kufanya vyote wewe unatakaje?
Olivia:
yaani napagawa mwenzio ila nitakuambia
Patrick:
usipagawe ndo kwanza tunaanza tulia mtoto upendwe vizuri
Olivia:
Mungu huyu (anaguna)
Patrick:
unatakiwa kujua mumeo nina roho ya kitajiri kwahiyo utaenjoi
Olivia:
hata mimi nimeona
Patrick:
basis awa (anacheka)
Olivia:
nakupenda patrick
Patrick:
nakupenda pia

0 Comments