SCENE
1: -
(Majira ya saa moja usiku,hali ikiwa imepoa
na hali ya hewa kwa ujumla ni nzuri na kaupepeo Fulani mwanana kanavuma kwa
mbali,uwanja wa ndege jijini mwanza msichana mrembo sana aitwae Olivia
amesimama huku anaonekana kuna mtu anamsubiri na pia anaonekana kuwa ana shauku
kubwa sana ya kumuona mtu huyo,baada ya muda hatimae mgeni wa msichana Olivia
anawasili na anaonekana kuwa ametoka nchi ya nje,mara baada ya kufika Olivia
anamuona na kwa furaha anakimbia kumlaki mtu huyu ambae kwa haraka anaonekana
ni mwanaume wake yaani mpenzi wake maana anamkumbatia na kumbusu)
Olivia :( huku anamkimbilia) Patrick my love
Patrick:
hello baby… (Anamkumbatia na kumbusu)
Olivia :(
anambusu pia) hi darling karibu tena kwetu…
Patrick:
asante…ila hata mimi hapa ni kwetu sema tu sababu ya masomo na biashara zangu
najikuta nakaa sana nje…ila sijasahau kuwa mimi ni mtanzania huoni hata lugha naijua
(Anacheka kidogo)
Olivia:
haswa mpenzi…naona kabisa kuwa unaikumbuka kabisa lugha yetu
Patrick:
Oh! I missed you so very much baby...Nikikuambia uje England huji unajivuta
kweli sijui kwanini
Olivia:
bado visa yangu haijatoka ila ikitoka nitakuwa naenda na wewe
Patrick
:( anacheka) asante…ok yaani nimechoka kweli nahitaji kwenda kupumzika...Nilikuambia
kuwa nikija tena nitakuonyesha nyumba yangu nahisi Leo ndo siku nzuri na
muafaka wa mimi na wewe kwenda kuiona nyumba yangu
Olivia:
si umesema kuwa umechoka? kwanini usiende kupumzika tu
Patrick:
wewe umekuja kunipokea airport Ili unipeleke wapi
Olivia:
ok sweetheart…umeshinda sina la kuzungumza…umeshinda
Patrick
:( anacheka sana) ok dear twende…zetu
( Pamoja wanaondoka uwanjani hapo
nje ya uwanja huo yupo dereva wa kijana Patrick aliyekuwa anamsubiri boss wake
muda mrefu,taratibu wakiwa wameshikana mikono Patrick na Olivia wanaliendea
gari lile,kisha wanapanda na bila kupoteza muda wanaondoka kuelekea nyumbani
kwa Patrick…baada ya mwendo wa kama nusu saa wanafika katika jumba safi na la
kifahari,nyumba inapendeza na inaonekana ni ya gharama kubwa sana,geti
safi,kuna walinzi na wamama wawili ambao wanaonekana ndo wamepewa jukumu la
kuiangalia nyumba hiyo,Patrick anashuka kwenye gari kisha anamfungulia mlango Olivia
ambae pia anashuka kwenye gari hilo huku anashangaa sana mazingira hayo
yanayovutia kuliko)
Patrick:
karibu sana my love, hapa ni nyumbani kwangu, (anawaonyeshea wavulana waliokuwa wamesimama karibu na geti) wale ni walinzi wa nyumba yangu
ni kama ndugu zangu pia
Olivia:
oh!!!Nice to meet them (anatabasamu)
Patrick:na
wale (anaonyeshea wanawake wawili wa makamo)
hawa ni mama ambao nimewaweka waangalie nyumba yangu kipindi tu napokuwa sipo
nyumbani nipo labda London au Dubai kwa ajili ya biashara zangu
Olivia:
oh…jamani nashukuru kuwafahamu (anatabasamu)
Patrick
:( anawaita wafanya kazi wake wote) tafadhali njooni…
Wafanyakazi
:( wanamuendea)
Patrick
:( Kwa heshima anamsalimia mmoja wa
wamama) shikamoo dada Agnes…
Agnes:
marahaba baba habari za London?
Patrick:
nzuri sana (kwa mama mwingine) da.
Halima...Shikamoo
Halima:
marahaba mdogo wangu habari za London?
Patrick:
nzuri tu…
Agnes:
naona umekuja na mwali
Patrick :( anacheka) anaitwa Olivia ni mpenzi
wangu tulikutana katika mitandao ya kijamii…Instagram (anacheka)
Halima:
sawa…ni muda gani sasa?
Patrick :( anacheka) ni muda kidogo mama yake
anajua na mara nyingi huwa nikija naenda moja kwa moja kwao kwanza halafu ndo
nakuja nyumbani…kwahiyo ni muda sasa tangu tuwe wapenzi nampenda na nina malengo
nae
Agnes:
siku hizi utandawazi sisi zamani tulikuwa tunakutana na wapenzi wetu kwenye
chagulaga huko au unaletea mchumba nyumbani lakini siku hizi mambo yamekuwa
tofauti watoto wengi wanakutana mitandaoni
Halima:
nakwambia kazi kweli kweli jamani…
Agnes :( Kwa Olivia) karibu wifi
Olivia :( Kwa heshima huku anapiga magoti)
shikamooni mawifi zangu
Kwa pamoja:
marahaba hujambo
Olivia:
sijambo
Patrick:
ok... dear, hawa ni kama dada zangu sio kama ni dada zangu (anacheka kidogo)
…wameniangalia muda wote wa maisha yangu yaani tangu baba na mama bado wapo hai
wenyewe wamekuwa ndo dada zangu mimi kwetu nipo peke yangu...Kama wewe tu (kwa
Agnes) yupo peke yake huyu (anatabasamu)
Agnes:
jamani kweli?
Patrick:
ndo hivyo sister… (Kwa Olivia)
kwahiyo ndo hivyo mpenzi nadhani nilikuambia kuwa baba na mama yangu walikufa
kwa ajali ya ndege walikuwa wanatoka Dubai, kwahiyo sina baba wala mama wala
kaka ila nina dada zangu wawili hawa hapa
Olivia:
oh, nashukuru na ninafurahi sana kuwafahamu…mimi naitwa Olivia kama baby
alivyokwisha nitambulisha nina umri wa miaka 27, ninaishi nyegezi, ninaishi na
mama yangu sina baba
Halima:
pole Sana Kwa kupoteza mzazi mmoja ila yote ni kumshukuru sana Mungu maana
wanasema kazi yake haina makosa yeye akipanga amepanga kikubwa tu ni kuwaombea
wapumzike kwa Amani
Olivia:
amina wifi…
Agnes:
karibuni ndani naona Patrick amaeamua kufanya utambulisho nje
Patrick :( anacheka) kumbe nimefanya kosa eeh
Halima: Sana...Tena
Kama mchumba ilibidi aingie ndani kwanza tumpe maji au juisi au wine ndo tuanze
utambulisho
Patrick:
basi nisameheni au nichapeni bakora (anacheka)
Agnes:
umeshasamehewa
(wanacheka kisha wanaingia ndani
ambako ndo ufahari wote ulipo, sofa safi meza kubwa ya kioo, runinga yenye kioo
kikubwa ukutani, ukienda sehemu ya kulia sasa ndo utakubali, maana pana samani
nzuri na za thamani, Olivia anapashangaa sana, dada Agnes na dada Halima
wanatenga vinywaji, na wanapomaliza kutenga, wanaketi na wenyewe na taratibu
wanakunywa vinywaji vyao)
Patrick
:( Kwa Olivia) feel at home darling…
Olivia
:( hata hasikii maana akili yake
imeshageukia kwenye vitu vya kifahari anavyoviona sebuleni)
Patrick:
baby…
Olivia :( anakuwa Kama ameshtuliwa usingizini)
yes…baby
Patrick :( anacheka) feel at home…
Olivia:
thank you baby…
(Kwa pamoja wanaangua kicheko, huku
wanaendelea kunywa vinywaji vyao taratibu)
Halima :( huku ananyanyuka) ngoja nikaangalie
dinner Kama iko tayari
Olivia
:( anaangalia simu yake) ah…mi naona
niwaache usiku umeingia na sijamuaga mama
Patrick
:( anatoa simu yake matata aina ya iphone)
ngoja nikuagie Kwa mama yako ingawa hautalala huku ila utachelewa kidogo (anapiga simu inaita mwisho inapokelewa)
hello mama…shikamoo
Mama:
marahaba baba hujambo?
Patrick:
sijambo…Patrick anaongea hapa
Mama:
najua baba upo hapa nchini?
Patrick:
ndio mama, ndo nimekuja Leo, ndo nimefika mama yangu
Mama:
sawa baba karibu
Patrick:
Asante mama…samahani mama
Mama:
bila samahani baba
Patrick:
nipo na Olivia na tutapata nae chakula cha usiku kwahiyo atachelewa kidogo…mama
yangu
Mama:
ondoa shaka mwanangu kuwa huru baba ni mwenzio huyo mwanangu kuwa nae huru tu
Patrick:
Asante mama…nitamleta baadae
Mama:
sawa baba
Patrick
:( anakata simu) kesi imeisha au sio...lets
enjoy baby
Olivia:
sawa (anacheka tena)

0 Comments