ON MY WEDDING DAY 2


 

SCENE 2: -

(Asubuhi nyingine, siku moja baada ya kijana Patrick kutoka London, Olivia amelala kwao, wakati simu yake inaita sana na kwa kuwa yupo usingizini hasikii, mama yake anaingia chumbani humu anaona simu yake inaita anamuamsha)

Mama: Olivia… (Anampiga piga)

Olivia:(huku anavuta shuka) mama niache bwana, we si unajua jana mimi nilichelewa kurudi nyumbani (sauti ya kama mtu aliyelemewa na usingizi sana)

Mama: mwenzio anakupigia simu

Olivia:(anakurupuka) mama yangu (anachukua simu yake mara moja) duh...Missed calls 14 duh!!!huku kulala kulala gani mbona nimezidi(anampigia)

(Simu inaita mwisho inapokelewa)

Mama :( anaondoka)

Patrick: dah…wewe unalala utasema umekufa nimeamkia hapa kwenu Leo nimesimama hapa mpaka nimekoma

Olivia: pole dear…yaani usingizi huwa unanichukulia muda kweli

Patrick: eeh jamani embu badilika huko kulala kama umekufa kumenichanganya mwenzio nikajua umedanja (anacheka) nipo hapa nje

Olivia :( anacheka) karibu ndani dear, sasa mbona umesimama nje?

Patrick: nilijua nitakupata mapema nilitaka twende rock city mall tukafanye shopping au umebanana leo

Olivia: no, niko free

Patrick: twende sasa

Olivia :( anacheka tena) hata sijaoga…ngoja nioge kwanza

Patrick: hapo sasa utanichelewesha unajua...

Olivia :( anashuka kitandani) ngoja nije maana kuingia ndani umekataa

Patrick :( anacheka) mi naona ndani nitachelewa Sana we Fanya twende

Olivia :( anafika nje) njoo bwana

Patrick :( bado simu ipo sikioni) nitachelewa

Olivia: dakika mbili nyingi

Patrick :( anaingia nae ndani)

Olivia: hivi umegundua?

Patrick: nini?

Olivia: bado tunaongea na simu

Patrick :( anacheka) sijagundua Hilo…we umetoka mtupu ndo nilikuwa nakushangaa

Olivia :( anacheka Sana) nimetoka uchi??? Ila Patrick we chizi (anacheka sana)

Patrick: ndo hivyo…mama yuko wapi?

Olivia: atakuwa ndani

Patrick: eti eeh

Olivia: nimuite aje akupe kampani?

Patrick: usimsumbue we kaoge bwana

Olivia: je ungependa chai?

Patrick: sasa hivi saa tatu yote hii

Olivia: sasa je?

Patrick: hapana nimeshakunywa

Olivia: poa (anamuwashia runinga ndogo iliyokuwepo hapo sebuleni) enjoy feel at home

Patrick: thank you honey

Olivia: poa (anaenda nje kwenda kuogea nje)

Patrick: mbona unaenda kuogea nje ndani hakuna bafu?

Olivia: hakuna bafu

Patrick: hii Ni nyumba yenu au mmepanga?

Olivia: yetu…

Patrick: duh…sasa na khanga moja mke wangu hao majirani si huwa wanafaidi?

Olivia: umeanza wivu

Patrick: Mimi nina wivu mpaka huwa najiogopa

Olivia :( anacheka) mi naenda kuoga bwana hatutamaliza na haya masihala yako

Patrick: fanya haraka nikakufanyie shopping my wife

Olivia: poa

Patrick: pia ulizia Kama tunaweza kupata nafasi tukaweka choo cha ndani…maana sio kwa kuwafaidisha midume huko nje

Olivia: ipo sehemu ilitengwa kwa ajili ya choo cha ndani ila hatukukamilisha maana pesa nayo ikawa haionekani

Patrick: usijali…nipo hapa…sitaki mke wangu uwe unaenda kuoga nje na watu walivyo hawana dogo watakuwa wanakuchungulia

Olivia :(anacheka sana) yaani wewe (anaenda zake kuoga)

Patrick: oga haraka bwana

Olivia: poa (anaingia bafuni)

Patrick :( anaendelea kuangalia runinga ila anaitazama sana nyumba ile kubwa na yenye ramani nzuri tu sema tu imechakaa sana) lazima nimtengenezee Olivia wangu mazingira mazuri nay a kuvutia hivi…hamna kwa kweli

Olivia :( anatoka bafuni) si unaona?

Patrick: mwenzangu umeoga vizuri kweli

Olivia: kabisa halafu huwezi kuamini

Patrick: haya kavae

Olivia (: haraka anaingia kuvaa, Kama dakika kumi hivi anakuwa amemaliza kuvaa, anaenda kwenye dressing table yake chakavu anaanza kujipodoa na kama dakika tano anatoka alipo Patrick) si umeona... (Anamuita mama) mama

Mama :( anakuja) eeh baba huyo

Patrick: naam mama, shikamoo?

Mama: marahaba (kwa Olivia) nini, nimesikia umeniita

Olivia: natoka mama yangu, tutaonana baadae

Mama: sawa mama

Patrick :( anatoa pesa mfukoni mwake kisha anampa mama) mama chukua hizi zitakusaidia siku mbili tatu mama yangu

Mama: Asante baba…Mungu akuzidishie

Patrick: asante mama

Olivia: kwaheri

Patrick :( anatangulia nje)

Olivia :( anamnong’oneza) sh. Ngapi (anacheka) na mimi naomba

Mama: wee nae mbea embu nenda mwenzio anakusubiri

Olivia :( anacheka kisha anaenda nje alipo Patrick)

Patrick: umemeliza kucheka

Olivia :( anacheka tena)

Patrick: inaonekana humalizi leo

Olivia :( anacheka tena)

Patrick: basi tukae hapa tucheke wote

Olivia: twende bwana

Patrick :( anamfungulia mlango anahakikisha kuwa amekaa kisha anapanda kwenye gari analiwasha halafu wanaondoka)


Post a Comment

0 Comments