I KILLED MY LOVER 7

 


SCENE 7: -

(majira ya saa nne usiku, Liliana anajiandaa kulala katika godoro lake hafifu analolifanya kitanda na chumba chake ni stoo yenye giza totoro, baada ya kutandika kitanda chake analala huku amewasha tochi yake ndogo inayotumia betri, wakati yupo usingizini anashtuliwa na mtu na anaamua kukaa ili amsikilize anachosema)

Liliana: mjomba mbona usiku sana mi nimechoka nataka kulala ili kesho niwahi kuamka niwaandalie chai na mimi niwahi shule

Mjomba:(anacheka) nimekuja kuchukuaa jibu langu (anamshika mkono kwa nguvu)

Liliana: mjomba unafanya nini? unaniumiza mikono

Mjomba: acha kudeka…wewe mtoto wa Paulina kwanini unajifanya una msimamo?

Liliana:(anaanza kulia)

Mjomba:(anaweka kidole mdomoni mwake ishara ya kumnyamazisha) ssssh…nyamaza…na ninaomba unisikilize

Liliana:(anaonekana anaogopa sana) mjomba…

Mjomba: hata usiogope Liliana sitakuua tena itakuwa vizuri nitakuwa nakutetea kwa shangazi yako asiwe anakupiga na wala kukutesa

Liliana: hapana mi kwanza bado ni mdogo sana mjomba na pia ni mtoto wa dada yako…

Mjomba: nimeshakuambia na ninakuambia tena huyo dada yangu hayupo tena ameshakufa kwahiyo wewe ni halali yangu…ukikataa nakubaka…

Liliana: najua huwezi kufanya hivyo

Mjomba:(anacheka) kweli eeh

Liliana:(anamshangaa)

Mjomba:(anamvua nguo zake kwa nguvu)

Liliana:(Analia) mjomba niache jamani… (Analia tena)

Mjomba:(anamuingilia kimwili kwa nguvu)

Liliana:(Analia sana) shangazi

(upande wa pili chumbani alipolala shangazi yake Liliana anasikia kilio kile ila wala hanyanyuki kumsaidia)

Shangazi:(anajifunika shuka vizuri)

Mjomba:(anaendelea kumuingilia Liliana kimwili bila hata ya huruma)

Liliana: mama yangu… (Analia sana) nakuita mama yangu jamani uko wapi?

Mjomba:(anamaliza na kushuka kifuani kwa mtoto Liliana) sasa hiyo itakuwa sio mwisho leo ni kila siku…wewe ni mke mdogo (anacheka kisha anaondoka)

Liliana:(Analia sana) mama kwanini ulikufa na kuniacha yatima sasa sisomi shule nzuri, mimi ndo kijakazi humu ndani…nalala stoo wakati hii ni nyumba yetu, ona sasa mama mjomba amenibaka tena bila hata huruma na mimi ni mtoto mdogo sana mama yangu…kwanini ulikufa umeniacha mdogo hivi mama (Analia sana) mama yangu jamani (anazima tochi yake kisha analala huku anaendelea kulia sana) kesho nitamwambia shangazi…

(Mlango unafunguliwa)

Liliana: hapana mjomba nimeumia sana, sitaki tena (anawasha tochi)

Anna: hapana binamu ni mimi…mbona unamuogopa baba?

Liliana: hapana binamu…simuogopi labda nilikuwa naota…

Anna: mbona unalia?

Liliana: hapana mbona mimi silii?

Anna: nimekusikia unalia na ndo maana nimekuja kukuona

Liliana: nitakuwa nilikuwa naota…

Anna: hapana binamu, kuna kitu unanificha…niamini nitakusaidia

Liliana:(anaanza kulia tena) binamu naomba unitoroshe niondoke hapa la si hivyo nitakufa au nitajiua

Anna: kwanini unasema hivyo?

Liliana: siwezi endelea kukaa siwezi binamu

Anna: kwanini?

Liliana: nateseka Anna…nitakufa (Analia)

Anna: nakuelewa binamu…sasa ukitoka hapa utaenda kuishi wapi?

Liliana: popote tu

Anna:na ndugu zetu wengi wanaishi nchi za nje jamani…

Liliana:mi hata sijui nitafanyaje ila tu nataka unisaidie kutoroka hapa

Anna: hapana ngoja tufanye hivi nitamuulizia rafiki yangu shuleni kama unaweza kukaa kwao kidogo baadae nitakusaidia hata hela kidogo nitamuibia mama, ili upange hata chumba

Liliana: nitashukuru dada yangu

Anna: sawa unaniamini?

Liliana: ndio…

Anna: niambie unalilia nini?

Liliana:(kimya)

Anna: niamini kuwa nitakuwa na wewe siku zote za maisha yako…

Liliana: mjomba amenibaka

Anna:(anashangaa sana) eti nini? (anatikisa kichwa ishara ya kusikitika) baba yangu ni Zaidi ya mnyama…hafai katika jamii

Liliana: ndio binamu hapa nilipo nina maumivu makali sana…

Anna:(Analia) maskini binamu yangu, ndo maana nimesikia kilio cha uchungu sana kumbe baba yangu ndo alikuwa anafanya unyama kama huo?

Liliana:na amesema sio mwisho leo…kwanzia leo nitakuwa mke mdogo

Anna: haiwezekani…lazima tumwambie mama

Liliana: nitamwambia kesho patakapopambazuka

Anna: sasa ninaelewa kwanini unataka kutoroka mi nilijua ni kwasababu ya manyanyaso ya mama yangu kumbe hata baba yangu amekunyanyasa jamani tena kijinsia na kimwili…baba yang undo kakuumiza Zaidi

Liliana:(Analia)

Anna:(anamfuta machozi) nyamaza usile binamu yangu…nitatafuta njia nikamshtaki polisi na kuanzia leo hatakugusa hata iweje labda kama sipo

Liliana: asante dada yangu

Anna: kuna wanadamu ni kama wanyama na wanyama ni afadhali sana…sasa wewe si mdogo sana hata mimi ni mkubwa kwako tena mbali sana

Liliana: mimi nina miaka saba tu dada

Anna: pole mdogo wangu (anamuangalia usoni) maskini yaani unatia huruma ila mimi nitakuwa na wewe muda wote hata usemeje nitakuwa na wewe tu

Liliana: asante dada

Anna: umekula?

Liliana: ndio…

Anna: ila sidhani kama ulishiba

Liliana: ah…sijisikii kula

Anna: poa mi ngoja nikalale…twende tukalale huku

Liliana: Bella yupo

Anna: niachie mimi (ananyanyuka na kutoka nje)

Liliana:(ananyanyuka na kumfuata)

(Wanaenda mojakwa moja mpaka chumbani kwa Anna na Bella na wanapofika Anna anamsogeza Bella ukutani na kumlaza Liliana)

Bella:(anashtuka toka usingizini) mbona yupo hapa?

Anna :( anacheka kidogo) hivi hujui huyu ndo mwenye hii nyumba na vitanda vyote sasa nakuomba ulale kimya hapa

Bella :( haleti ubishi analala)

Anna :( anawafunika shuka kisha na yeye analala)

Post a Comment

0 Comments