SCENE 60: -
LONDON UINGEREZA: -
FUNGATE LA MIRIAM NA
JEREMY (HONEYMOON)
(hali
ya ubaridi Fulani mtulivu umetambaa katika jiji maarufu duniani pande hizo za
kwa malikia Elizabeth, Miriam amesimama peke yake huku anaonekana kufurahi mandhari
na hali ya hewa ya jiji hilo)
Miriam:
oh, nimepapenda sana huku…ni pazuri Sanaa
Jeremy:
(anakuja kwa nyuma yake na kumkumbatia) baby
Miriam:
baby
Jeremy:
(anampaa kinywaji)
Miriam:
baby unajua kuwa mimi sinywi pombe
Jeremy:
unajua hata mimi sipendi nawala sinywi pombe hii ni shampeni na walaa haina
kilevi
Miriam:
kama ile tuliyokunywa kwenye sherehe ya harusi yetu?
Jeremy:
yes, my love
Miriam:
(anapokea) asante sana baba G
Jeremy:
usijali mpenzi wangu…mke wangu
Miriam:
(anacheka kisha anakunywa kidogo) mmh tamu
Jeremy:
najua ni tamu sana… (anacheka kisha anamkumbatia) tupange kupata mdogo
wake G maana G tulimpata kwa bahati mbaya…
Miriam:
jamani mume wangu mtoto wetu ndo kwanza ana miezi sita
Jeremy:
najua mke wanagu ila sasa haitakuwa bahati mbaya itakuwa ni ndani ya ndoa
haitakuwa kama kipindi kile
Miriam:
(anacheka) najua ilikuwa tulizidiwa sana siku hiyo (anacheka)
huwezi kuamini nilikuwa nawaza labda utaniacha
Jeremy:
siwezi…na nisingeweza…tangu siku ile nimekuona mara ya kwanza nilijisemea kuwa
nitafanyakila kitu ili uwe mke wangu (anacheka) kuna mara nyingine
nilikuwa nafunga kuombea huu uhusiano uishie kwenye ndoa
Miriam:
hata mimi nilikuwa nafunga…nilijua tu kuwa MUNGU wetu sio kiziwi atatufikisha
ona sasa ametufikisha
Jeremy:
kabisa…
Miriam:
nakupenda Jeremy
Jeremy:
hunizidi… naahidi kuwa nitakupenda sana mpaka basi…(anamkumbatia) G
kalala tumtafute mdogo wake
Miriam:
mume wangu tuenjoi kwanza hali ya hewa ya mji huu…kwanza utanipeleka kwenye
jumba la kifalme?
Jeremy:
nitakupeleka mke wangu, nitakupeleka na Mexico kwa wale waigizaji unaowapenda
kisha tutaenda New York kisha Canada na kama utapenda kwendaa China na Dubai
nitakupeleka
Miriam:
asante sana mume wangu...namuwaza sana dada yangu
Jeremy:
sh... sh... usimuwaze mtu yeyote tafadhali huu ni wakati wetu mpenzi
Miriam:
(anazungusha mikono yake mabegani kwa mumewe) sawa ila usiseme mtoto
wetu G ni wa kimakosa…mume wangu mtoto wetu ni matunda ya penzi letu haijalishi
tulimpataje jibu ni kwamba yeye ni zawadi kubwa sana tuliyopewa nay eye aliye
MKUU kuliko vyote na huyo ni MUNGU
Jeremy:
yes, my wife…nisamehe kama nimesema vibaya mpenzi…ni kweli mtoto wetu ni zawadi
na matunda mazuri ya penzi letu
Miriam;
(anambusu)
Jeremy:
(anarudisha busu kwa mahaba mazito)
Miriam:
I love you my king
Jeremy:
I love you my queen
(wanakumbatiana
kwa mahaba mazito)
Glory:
(anacheza cheza)
Miriam:
(anamuona) G kaamka
Jeremy:
hana muda na sisi…
Miriam:
(anacheka) hata mimi namuona hana muda na sisi
Jeremy:
(anambeba mkewe)
Miriam:
(anacheka) jamani Jeremy
Jeremy:
asante Yesu Miriam ni mke wangu sasa
Miriam:
(anacheka)
Jeremy:
(anamlaza kitandani)
Miriam:
(anatabasamu)
Jeremy:
all that is well ends well…all is well kwa UKUU wa MUNGU
Miriam:
namuomba Mungu awe na sisi daima na daima
Jeremy:
(analala pembeni yake) love you baby
Miriam:
I love you
Glory:
(Analia kwa nguvu)
Miriam:
oh Glory
(wanacheka)
THE END
Miriam
na jeremy wanaendelea kuishi kwa amani bila kuogopa kitu chochote, wanapata
watoto wengi kadri ya jinsi walivyopenda na Mungu alivyowajalia , Mary na
Vincent wanafanikiwa kupata mtoto mwingine wa kike ambae ni mdogo wake Miriam
na Colton, Colton na Vanessa wanabarikiwa watoto pia na wanaishi kwa Amani na
upendo. baada ya muda mrefu hatimaye Ariana
nae Mungu anamsaidia anapata mume anaolewa na kuzaa watoto mapacha, kila mtu
anaishi vizuri kadri alivyoomba kwa Mungu.

0 Comments