SCENE 8: -
(Asubuhi ya kesho yake Anna
anafika shuleni anaonekana akiwa na mawazo mengi sana kichwani kwake)
Anna:
Liliana anahangaika sana na haya maisha najiuliza kosa lake nini? je kosa lake
labda ni kufiwa na wazazi wake akiwa katika umri mdogo? namuonea huruma
sana…halafu baba si ni ndugu yake wa damu bora mama unaweza kusema kwakuwa
hawachangii damu ndo maana anamtesa namna ile…
Bella:
dada Anna unaonekana una mawazo sana kulikoni?
Anna:
hamna mbona nipo kawaida sana?
Bella:
haya kama uko kawaida…
Shangazi:(mama
yao) hata mimi nakuona hauko sawa kama kuna kitu kinakusumbua niambie mwanangu
tuna pesa na magari ya kutosha kila kitu sasa ni chetu sio maisha tuliyokuwa
tunaishi mwanangu…niambie chochote nitakununulia
Anna:ni
kweli tuna magari nyumba nzuri na pia tuna pesa maisha yetu ni mazuri sana tu
ila vyote hivi sio vyetu mama ni vya yule tunayemuacha nyumbani anafanya kazi
na kwenda kwenye shule za kawaida
shangazi:
funga bakuli lako kabla sijakupiga vibaya sana…we mbwa wewe
Anna:
Mungu hapendi tunachomfanyia mtoto wa watu mama
shangazi:
nenda darasani mbwa wewe
Anna:(anaondoka na kuelekea darasani)
Shangazi:(kwa Bella) na wewe unataka kuniambia
nini mimi?
Bella:
aku!!! Mi naona uko sawa tu mama
Shangazi:(anatabasamu) wewe mwanangu ndo mjanja…(anacheka)haya mama waweza kwenda tu
darasani baadae nitakuja kuwachukua…
Bella:
sawa mama… (anakimbia darasani)
Shangazi
:(anapanda gari na kuondoka)
(Upande wa Anna anafika ofisini
kwa mwalimu wake wa darasa)
Anna:(anagonga mlango)
Mwl
Monica: Karibu Anna…
Anna:
asante mwalimu… (anaingia kisha anakaa
katika kiti kilicho karibu na meza ya mwalimu huyo) shikamoo mwalimu
Monica:
marahaba mama hujambo?
Anna:(kinyonge) sijambo…
Monica:
vipi? mbona unaonekana huna raha?
Anna:
kuna shida mwalimu sina mtu wa kumwambia Zaidi yako mwalimu…
Monica:
nini tatizo mwanangu…mbona unanitisha?
Anna:(anasikitika kidogo) hivi huwa hakuna
taasisi ambazo zinaweza kusaidia mtoto anayenyanyaswa…kihisia, kimwili na
kadhalika?
Monica:
zipo…ila kwanini unaniuliza? je unateswa?
Anna:
hapana sio mimi mwalimu…
Monica:ni
nani?
Anna:
binamu yangu…ni mtoto wa shangazi yangu…wazazi wake walikufa katika ajali ya
gari na walipokufa wazazi wangu wakajitolea kumlea maana sisi ndugu zetu wengi
wanaishi nchi za nje…kwahiyo wakaona nyumba ya marehemu shangazi yangu isikae
bila watu ndo tukawa tumehamia hapo, cha kushangaza binamu yangu anateseka
sana…ananyimwa chakula, analala stoo
Monica:(anasikitika sana) maskini
Anna:
anafanya kazi zote za hapo nyumbani…anasoma shule ambayo ni ya serikali na hapo
anaenda shule mara baada ya kufanya kazi nyingi sana ufaulu wake uko chini sana
kutokana na kwamba anaenda shule akiwa amechoka analala akifika shule yaani
anasikitisha sana jamani
Monica:
aisee…unaonekana unaumia sana
Anna:na
kilichoniumiza sana na Zaidi nan do nikaona nitafute mtu anisaidie…ni kwamba
baba yangu anambaka binamu yangu mara kwa mara
Monica:(kwa mshangao) eti!!!!???
Anna:
ndio mwalimu…binamu yangu anabakwa na mjomba wake kila usiku…
Monica:
hii imekuwa too much…ngoja... (anachukua
simu yake na kubonyeza namba Fulani) ngoja inaita…ngoja nimwambie huyu wa
haki za watoto na wazee…atatusaidia ni rafiki yangu sana
Anna:
sawa mwalimu utakuwa umenisaidia sana
Monica:
hello Eliza…mambo vipi?
Eliza:
poa wewe za siku?
Monica:
nzuri…upo ofisini?
Eliza:
ndio nipo ofisini…my dear
Monica:
nataka kuripoti unyanyasaji wa mtoto
Eliza:
yes nambie…
Monica:(anaanza kumsimulia kama alivyosimuliwa na Anna)
Eliza:
Duh...hii nayo kali yaani nyumba ni marehemu wazazi wake yeye anakaa kama
hausigeli humo? eeh yaani jamani kwani wafu huwa hawaoni waje wamuokoe mtoto
wao?
Monica:
yaani acha tu na kali kuliko yote sasa, mtoto anatumika yaani anabakwa na
mjomba wake
Eliza:
aisee hiyo sasa tutachukua hatua mara moja…lazima tuende kwenye nyumba hiyo na
kujionea hayo wenyewe
Monica:
sawa haina shida rafiki yangu na nilijua utanisaidia tu na ndo maana nikaona nikupigie
wewe
Eliza:
usijali mtoto huyo hataona tena mateso…sisi tupo kwa ajili yake
Monica:
shukrani (anakata simu na kumgeukia Anna)
usijali mwanangu binamu yako hatakuwa na tabu tena yaani umemuokoa sana…
Anna:
sawa mwalimu nami nafurahi kusikia hivyo maana si kwa kuteseka kule jamani
yaani
Monica:
usijali hayo yameisha…
Anna:
sawa mwalimu ngoja mi niende darasani ila wakienda nyumbani wasiwaambie mimi
ndo nimekuambia
Monica:
usijali na wala hawatajua tutaenda kiakili sana
Anna:
sawa mwalimu…mi naenda(anaondoka)
Monica:
maskini huyo mtoto anaonekana anateseka sana, yaani mali za wazazi wako lakini
unakaa kama sio zako na hao wazazi jamani hawajui hata kuvunga hata kidogo
yaani wanamtesa waziwazi…eeh Mwenyezi Mungu nipe maisha marefu niwatunze
wanangu hata wakuekue kidogo wajitegemee na sio jinsi huyu mtoto alivyoachwa
(Upande alipo Anna)
Anna:
natumaini mwalimu atamsaidia binamu yangu maana si kwa kuteseka huko…
Bella
:( anamjia) dada…ulikuwa wapi mbona
nimekutafuta Sana?
Anna:
nilikuwepo mbona?
Bella:
sijakuona kabisa
Anna:
nipo (anaelekea darasani kwake)
Bella
:( anamsimamisha) dada…uko sawa?
Anna:
nitakuwaje sawa huku binamu yangu anateseka kwenye nyumba yake?
Bella:
kwani wewe dada yote hayo yanakuhusu nini? Si umuache?
Anna:
mimi na wewe tunatofautiaana sana…mimi inaniumiza sana hii hali…. ile nyumba ni
yake, magari yote ni yake…leo hii yeye ndo kawa mtumishi anasoma shule ya ajabu
ajabu amabyo haieleweki?
Bella:(anaonyesha kupuuzia maneno ya dada yake)
aah… (anaondoka na kuelekea darasani
kwake maana wanasoma madarasa tofauti tofauti yeye yupo la tano na dada yake
yupo la saba)
Anna:Mungu
atusamehe sana mimi na familia yangu hasahasa baba yangu kwa kitendo cha
kumbaka mfululizo malaika wa Mungu…(anaonyesha
huzuni sana)Mungu naomba kitu kimoja Mungu wangu…umsaidie binamu yangu
apate haki yake…tuishi nae ndio ila akae kama mwenye nyumba na sio mtumishi wa
nyumbani inaniumiza sana jamani na kila kukicha lazima apigwe na kutukanwa
matusi mengi kama mbwa…hana Amani je atakuwa mtu wa namna gani kama kila siku
lazima apigwe vidonda kila mahali…namuonea huruma sana Mungu kama unaishi naomba uonekane kwa binamu yangu ili
aishi maisha aliyoyazoea…nampenda sana binamu yangu na ninajua wakati wa bwana
umekaribia na ataenda kutenda sawasawa na mapenzi yake
Mwl
wa zamu: we Anna mbona hauingii darasani?
Anna:
samahani mwalimu (anakimbilia darasani)
0 Comments