SCENE
11: -
BAADA
YA WIKI MBILI: -
(Ni
asubuhi nyingine njema machoni pa bwana, Olivia amekaa katika mgahawa mmoja
ambao yeye na Patrick walipenda kwenda kunywa chai pamoja au wakati mwingine
kupata chakula cha mchana pamoja, amekaa pale lakini anaonekana hana raha
kabisa ya kila kitu, anaonekana kumkumbuka Patrick kwani mara nyingi aliitazama
picha ya Patrick iliyokuwa ipo katika simu yake)
Olivia:(huku
anaiangalia picha ya Patrick) my love…nimekukumbuka sana, nini kilitokea
kwetu mpaka mambo yetu yakaharibika
(Wakati
huo Patrick nae anaingia mahala pale, tararibu anaenda kukaa meza iliyokuwa
haina mtu kisha anamuita mhudumu)
Olivia:(anasikia
sauti ya Patrick na kugeukia inapotokea) Patrick?
Patrick:(anaangaza
huku na huku akiwa ana nia ya kumtafuta mhudumu lakini anajikuta macho yake
yameangalia kwa mtu mmoja nae ni Olivia) Olivia…baby(anamuendea)mambo
vipi Olivia?
Olivia:(anatabasamu)
safi za siku?
Patrick:
nzuri…hupokei simu yangu Olivia…kwanini lakini?
Olivia….
sio hivyo mambo ni mengi Patrick…
Patrick:au
bado umechukia kitendo cha mimi kukuficha?
Olivia:
embu karibu kwanza uketi ndo tuongee…
Patrick:(anavuta
kiti kisha anakaa)
Olivia:
wifi hajambo
Patrick:
nani sasa agnes au Halima?
Olivia:
mpenzi wako
Patrick:(anacheka)
sina mpenzi, mimi mpenzi wangu ni wewe ingawa umeamua kutafuta mpenzi mwingine
Olivia:(anashangaa)
wewe Patrick, iam single and very single sina mwanaume wala nini
Patrick:
unasema kweli? mimi niliambiwa na Edwin kuwa una mtu wako na mna mipango ya
ndoa…
Olivia:(anacheka)
mimi Monica aliniambia kuwa ulienda kwa huyo mpenzi wako mpya na kutoa mahari…
Patrick:
halafu Olivia bana unapenda sana kumuamini Monica
Olivia:
she is my friend
Patrick:(anamuangalia
kwa muda kisha anasimama na kumkumbatia mpenzi wake huyo) I missed you so much,
tusahau hayo ya Monica sijui Edwin wana lengo la kututenganisha
Olivia:
sasa kwanini wafanye hivyo?
Patrick:
sijui kwakweli si uchawi tu
Olivia:(anacheka)
yaani wewe
Patrick:
nakupenda naomba turudiane…nilete mahari kwenu ili tuoane
Olivia:
uko serious unataka kuwa mume wangu Patrick?
Patrick:
Zaidi ya serious…
Olivia:(anatabasamu)
I love you Patrick…mwanaume wa moyo wangu
Patrick:
nami nakupenda Zaidi mke wangu
Olivia:(anacheka)
Patrick:(anatabasamu)
Mhudumu:(anakuja)
kaka karibu…
Patrick:
asante sana…nipe tu supu ya kuku na chapatti mbili
Mhudumu:
sawa(anaondoka)
Patrick:(anamgeukia
Olivia aliyekuwa anamuangalia muda wote wakati anaagiza) wewe vipi? mbona
unaniangalia sana
Olivia:
nilikukumbuka sana na tangu tuachane hii ni wiki ya pili nimekuwa nikija hapa
kupata chakula nikiwa na matumaini ya kukuona mpenzi wangu
Patrick:
hata mimi huwa nakuja hapa kila siku nikiwa na tumaini la kukuona maana
nilikuwa naogopa kuja kwenu nikihofia nitamkuta mpenzi wako mpya halafu nilivyo
na wivu sijui tu ingekuwaje?
Olivia:(anacheka)
nani alikuambia?
Patrick:
Edwin…
Olivia:
na yeye…mmbeya huyo amenikera
Patrick:
labda anakutaka
Olivia:
ah…wapi?
Mhudumu:(analeta
supu na kuitenga hapo kisha anaondoka)
Olivia:
nitamwambia monica kuwa nimerudiana na wewe atafurahi kweli
Patrick:
usimwambie
Olivia:
baby…Monica ni Zaidi ya rafiki yangu yaani ni kama dada yangu kabisa…nampenda
kama dada
Patrick:
rafiki yako ndo adui yako my love…usimwamini sana Monica
Olivia:
lakini kama kunidhuru angekuwa ameshafanya hivyo siku nyingi
Patrick:
kila mtu ni mtu mbaya kutokana na mazingira yaliyomchochea kuwa mtu mbaya
Olivia:mi
hata sikuelewi
Patrick:
kama kweli unanipenda basi naomba unielewe kuwa sitaki Edwin wala Monica wajue
tumerudiana
Olivia:
yaani sitaki maugomvi na wewe kwahiyo nitakutii…
Patrick:
asante (kimya huku anakunywa supu yake)
Olivia:(anacheka
kidogo) umekonda baby
Patrick:
mawazo…chezea kukosa mke wewe
Olivia:(anacheka
huku anatoa simu yake na kutaka kujipiga picha yeye na Patrick)
Patrick:
hapana, najua unataka kumtumia Monica, baby ukifanya hivyo mipango yetu
itaharibika…kunywa chai twende kwa dada Agnes na Halima maana wamekukumbuka
kweli yaani
Olivia:mi
nimeshamaliza kunywa chai nakusubiri wewe love (anajipiga picha)
Patrick:
I love you
Olivia:(bado
anaonekana kunogewa na kupiga picha) umeshaniambia…kuwa unanipenda baby…
Patrick:
nataka nishinde nakwambia hivyo ili usiniache tena nataka uniamini mimi na
usiamini unachoambia hasahasa na Monica
Olivia:
poa baby…
Patrick:(ananyanyuka
na kwenda kunawa) twende…
Olivia:(ananyanyuka
pia na kwenda kunawa)
Patrick:
nakupenda Olivia
Olivia:(anacheka
kisha anamwagia maji usoni)
Patrick:
wewe acha watu wanatushangaa(anacheka)twende nyumbani (anamuita
mhudumu)
Mhudumu :(
anakuja)
Patrick:(anatoa
noti ya shilingi elfu kumi) wawili, mimi na mke wangu
Olivia:(anacheka)
Patrick
:(kwa mhudumu) keep change (kwa Olivia) twende
Olivia
:( anamfuata nyuma)
(Kwa
pamoja wanatoka na kuelekea mpaka katika maegesho ya magari na kupanda gari la
Patrick)
Patrick:
nimekuja peke yangu naondoka na mke
Olivia :(
anacheka)
Patrick :(
anacheka) umefurahi eeh…najua hata wewe ulikuwa umenimisi (anaanza
kuendesha gari taratibu)
Olivia:
(anaonekana kufurahia sana uwepo wa mpenzi wake)
(Wanaendelea kufurahia maisha kwa
pamoja huku kila mmoja wao anatoa ya moyoni na wanaonekena kuwa walikumbukana
sana baada ya kupotezana kwa takribani wiki mbili)

0 Comments