I KILLED MY LOVER 6

 


SCENE 6: -

BAADA YA MWEZI MMOJA (BAADA YA MSIBA)

(Ni alfajiri, Liliana amelala katika chumba chenye mfano wa stoo, maana kuna makorokoro mengi sana, na cha kushangaza amelazwa chini na ukiangalia hii ni nyumba aliyoachiwa na wazazi wake, wakati amelala anaingia shangazi yake akiwa amejawa hasira sana)

Shangazi: we Liliana mbona umelala mpaka sasa hivi na unajua kuwa hatuna mfanyakazi na wanangu wanahitaji kwenda shuleni

Liliana:(anaamka akiwa anatetemeka) samahani shangazi na leo nimejisahau kuamka mapema shangazi yangu nisamehe

Shangazi:(anampiga kofi la nguvu) pumbavu!!!!sana wewe kila siku unakosea ni lini utaelewa kuwa wewe ni mfanyakazi humu ndani na unatakiwa uwahi asubuhi kupika chai na kuwatayarisha wanangu

Liliana: lakini shangazi hata mimi ninatakiwa niwe naenda shule

Shangazi:si unaenda za serikali kwani huendi shule?

Liliana: lakini baba yangu si aliacha hela ya mimi kusoma?

Shangazi:(anamsukuma kwa nguvu) embu katayarishe Watoto wenye wazazi wao…wewe si huna mama wala baba?

Liliana:(anaenda huku Analia, anafika jikoni anakaa na kuanza kukumbuka mapenzi aliyokuwa anaonyeshwa na mama na baba yake, anajikuta machozi yanamtoka sana)

Shangazi:(anakuja) mbona wewe mtoto ni mvivu sana?

Liliana:(ananyanyuka na kuanza kupika chai kisha anatenga mezani anawaamsha watoto wa shangazi yake) amkeni mkanywe chai

Bella:(mmoja wa watoto wa shangazi yake) we mjinga nini…unaingiaje chumbani kwetu bila hodi?

Shangazi: nenda kamuamshe na mjomba wako anywe chai aende kazini

Liliana: sawa shangazi… (anagonga mlango) hodi

Mjomba: karibu

Liliana:(anaingia)

Mjomba:(anajikuta kumtamani hivyo anajikuta analamba midomo) karibu Lily…(anamvuta)

Liliana: niache mjomba…

Mjomba: nitakukamata…tu

Liliana:(anatoka anakimbia)

Shangazi: umeona nini? Mbona umetoka mbio kama mtu kaona mzimu?

Liliana: hamna kitu shangazi…

(watoto wa shangazi yake wamekaa mezani wanakunywa chai huku Liliana anaenda nje kufagia uwanja, ameinama anafagia huku anaimba nyimbo za huzuni za kuwakumbuka wazazi wake)

Shangazi:(analeta mabaki walioacha mume na watoto wake) kula chakula hiki na uende shuleni usije ukasema hatukusomeshi…

Liliana:(anachukua na kuanza kula)

Shangazi:(anarudi kwa wanae) haya fanyeni haraka niwapeleke shuleni wanangu…

Bella: mama, mimi huyo Liliana ananiudhi kweli…siku hizi hata hafui nguo zetu

Anna:(anaguna) Bella acha uongo mbona anatufulia? halafu mama mbona hii ni nyumba yao halafu analala stoo

Shangazi: kelele mshenzi mkubwa wewe…huna adabu wala shukrani

Anna: mama Mungu hapendi lakini

Shangazi: atajua mwenyewe awe anapenda asiwe anapenda atajua mwenyewe…

Anna:(anabaki anatikisa kichwa ishara ya kusikitika)

Shangazi: fanyeni haraka… (ananyanyuka na kwenda nje kwenye gari)

Bella na Anna:(wanamfuata)

Anna:(kwa Liliana) fanya haraka uende shule…mdogo wangu…

Shangazi:(kwa ukali) embu panda kwenye gari

Anna: mama lakini

Shangazi:(anawasha gari kisha analiondoa kwa kasi sana)

Anna:(anamchungulia Liliana kupitia kioo cha nyuma) maskini!!! Kwani kosa lake ni nini jamani?

Shangazi:(kwa Anna) naomba ukae vizuri wewe Anna

Bella: yaani anajifanya kumuonea huruma

Shangazi: tukimfanya awe mwenye nyumba tutaikosa hii nyumba mwanangu ndo maana tunatakiwa tumfanye aogope

Anna: lakini mama hii ni nyumba yao na pia hili ni gari lao, kwani tukikaa nae vizuri hatutaishi?

Shangazi: naomba unyamaze we mtoto usie na adabu kwa mama yako…acha tu enjoy muda wetu ndo huu

Anna:(anaona akae kimya)

(Upande wa Liliana huku amebaki peke yake na mjomba wake maana bado hajaondoka kwenda kazini)

Mjomba:(anamuendea alipokuwa amekaa anakula mabaki yao) pole maskini unakula mabaki…

Liliana:(kimya huku anamalizia kula)

Mjomba: naweza kukufanya kuwa unakula vizuri ukinikubali…niwe mpenzi wako…

Liliana:(anamuangalia) mjomba mimi ni mtoto mdogo sana na ndo kwanza nipo darasa la tatu mjomba nitakuwaje mpenzi wako?

Mjomba: unanibishia?

Liliana: siwezi kuwa mpenzi wako mi bado mdogo sana na pia ni ndugu yako

Mjomba: poa we jifanye sasa mjeuri utakula jeuri yako na kuanzia sasa hivi utateseke mpaka uombe kifo…kwani tatizo nini, si nalala na wewe kidogo tu nakuwa nakupa chakula kizuri

Liliana: sitaki…mjomba sitaki (anaingia ndani)

Mjomba:(anamuangalia kwa tamaa) mtoto mzuri sana jamani lazima niwe nae, dada nae alizaa mtoto mzuri jamani mwee

Liliana:(anatoka amevaa sare za shule za shule ya msingi za serikali amebeba na ufagio wake)

Mjomba: kwahiyo Lily…unasemaje?

Liliana: hapana mjomba…

Mjomba: hautakuwa unafanya kazi nyingi…nikubalie nitamwambia shangazi yako akupunguzie kazi

Liliana: nimekataa mjomba kwakweli sitaki tena sitaki kwelikweli huwezi amini na ukiendelea kuniuliza na kunisumbua nitamwambia shangazi…

Mjomba: unadhani atakuamini? (anacheka kwa kejeli) hawezi kukuamini…yaani wewe mkombozi wako ni mimi na sio shangazi yako ndugu yangu

Liliana: mjomba wewe si mdogo wa mama yangu? utasemaje niwe nalala na wewe …hunionei huruma nimepoteza wazazi hata arobaini yao bado tayari mmeshaanza kunitesa kimwili na hata kiakili

Mjomba: kumbe wewe huna akili eeh

Liliana: nitamwambia ma mdogo…

Mjomba: hakuna anaekufikiria hata mmoja ndugu yangu we kubali yaishe mama

Liliana: nachelewa shule (anaondoka zake)

Mjomba: kinajifanya kijanja sio? nitakaonyesha tu…

Liliana: Mungu wangu naomba unisaidie(anatokomea)

Mjomba: unadhani siwezi kumpata huyu mtoto naweza sana tu na hakuna atakayenizuia Liliana jiandae kuwa mke wangu wa pili haijalishi wewe ni mtoto wa marehemu dada yangu…sijali nachojali sasa ni kwamba mama yako kafa…kwahiyo hatuna undugu (anacheka kisha anapanda kwenye gari na kuliondoa kuelekea kazini)

Liliana:(yuko njiani anatembea taratibu huku anaonekena ana mawazo sana )yaani mama na baba yangu waliacha pesa nyingi ili nisome leo natembea kwa miguu na kwenda shule ya serikali huku shangazi yangu na watoto wake wanatembelea magari ya baba na mama yangu jamani(anajikuta Analia sana)kwanini baba ulikufa?kwanini mama uliniacha mdogo…ndugu zako wakaanza kugombania mali zenu kidogo wauane,mama wadogo hawaji tena…yaani nimebaki mpweke sana sina rafiki Zaidi ya Anna(Analia huku anaonekana kukaribia kufika shuleni)nimewakumbuka sana wazazi wangu wapendwa jamani…(Analia sana) Maskini mimi sijui Maisha yangu yatakuwaje baada ya hapa sijui nitaishije mimi (anafuta machozi)

Post a Comment

0 Comments