SCENE
48: -
RUMANDE:
-
(Jioni
yake, Miriam yupo na rafiki yake waliokutana jela wanazungumza mawili matatu
huku Miriam anaonekana bado anajisikia vibaya)
Rafiki:
una nini lakini miriam mbona sikuelewi? Nasikia ulijisikia kichefuchefu
mahakamani
Miriam:
hata sijui eliza
Eliza:
umeona siku zako?
Miriam:
zimepitiliza sijaona…kwani vipi?
Eliza:
unaweza kuwa mjamzito
Miriam:
haiwezekani
Eliza:
kama ulitembea na shemeji ndo majibu yake
Miriam:
hii ni aibu… jamani sikutegemea na siku hiyo tulijisahau hata haikuwa lengo na
ilitokea mara moja tu
Eliza: (anatabasamu)
hiyo mara moja sasa ndo imetuletea habari njema
Miriam:
Mungu wangu...
Askari:
Miriam una wageni
Miriam: oh,
kama ni Jeremy mwambie siwezi kumuona
Askari:
wamekuja watu kama saba ni ndugu zako…
Miriam;
(ananyanyuka na kutoka anapiga hatua mpaka walipo ndugu zake)
(Miongoni
mwa wageni hao wapo wazazi wa Mary, Jeremy, Vanessa, dada wa Mary na mwanaume
mmoja wa makamo ya mzee Ken)
Miriam:
shikamooni
(Wanaitikia)
Vanessa:
hello Miriam
Miriam:
mambo?
Miriam:
poa
Mary:
unaendeleaje mama?
Miriam:
bado najisikia kizunguzungu
Mary:
pole mama
Jeremy:
pole sana…utapona
Miriam:
asante…
Mary:
Miriam...nimekuja na hawa watu leo walikuwa wanataka kukuona
Miriam: (anatabasamu)
Mary:
hawa ni bibi na babu yako
Babu:
mke huyo
(Wanacheka)
Miriam:
(anamkumbatia)
Bibi:
mke mwenza…
Miriam:
(anamkumbatia)
Mary:
huyu ni mama yako mkubwa ni dada yangu
Miriam:
(anamkumbatia)
Mary: na
huyu ni baba yako mzazi
Miriam:
mlikuwa mnawasiliana?
Mary:
hapana mama…niliunganishwa na bibi na babu yako kwa miaka mingi kumbe alikuwa
anakutafuta…waliponipata mimi ndo nikaona nije nikutambulishe
Miriam:
sawa nimefurahi kusikia…mimi naitwa Miriam
Baba: (anacheka)
nakujua… mimi naitwa Vincent na wewe ni mwanangu wa pili na wa mwisho
Miriam:
nina kaka au dada?
Vincent:
kaka
Miriam:
(anamkumbatia)
(Wanafurahi)
Vanessa:
shoga una familia mbili
Miriam:
(anacheka) Mungu amenipendelea
Askari:
(anakuja)
Miriam:
muda umeisha?
Askari:
hapana nimeleta majibu yako hapa mpo wote naona ni muda mzuri kusema
Mary:
majibu ya nini?
Askari:
Miriam ni mjamzito
Jeremy: (anafurahi
kupita kiasi) oh My God…naenda kuwa baba…Oh God
Miriam: (anakaa
kimya)
Mary:
Miriam
Miriam:
mama hata sikupanga haki ya Mungu mama nisamehe
Mary:
kwani mimi nimesemaje?
Dada:
hongera sana mwanangu najua umeipata bila kuwa na ndoa ila ni Baraka hongera
sana
Miriam:
mnasema kweli? Ila sasa ndo naenda kunyongwa naombeni niitoe hii mimba
Vincent:
nani kasema unaenda kufungwa mwanangu? Hufungwi wala kunyongwa bado upo sana
embu niachie mke au mume mwenza nijidai mimi…
(Wanacheka)
Jeremy:
thank you my love…kwenye wakati mgumu kama huu tumepata jambo jema
Miriam:
(anatabasamu)
Babu:
hongera mke kwa habari hii njema…tutailea ni kwa bahati mbaya sana hatukukubali
wewe maana mama yako nae alikuzaa akiwa bado mtoto mdogo sana alituudhi
tukamfukuza hii dhambi inatutafuna …sasa kwako tutamlea huyo mtoto…
Bibi: (anamshika
tumbo) aje huyo kiumbe atakayekuwa Baraka kwa ulimwengu mzima
Miriam: oh,
bibi jamani…asante kwa Baraka zako
Vanessa:
hongera sana rafiki yangu
Jeremy:
hongera (anamkumbatia)
Miriam:
(anamkumbatia pia)
Mary:
nitawaambia Keddy na Ken
Jeremy:
asante Mungu (anambusu Miriam)
Miriam:
(anaona aibu)
Vincent:
oh mwanangu...nimefurahi kukuona na Zaidi kusikia habari hii kuwa naitwa babu
baada ya miezi kadhaa
Mary:
asante Mungu
Vincent:
tukija tena tutakuja na kaka yako…
Miriam:
mlete kabla sijanyongwa
Jeremy:
honey please
Miriam:
just kidding…nendeni sasa
(Wanacheka)
Jeremy:
(anambusu) kesho
Miriam:
haya tuopo jamani
(Wanaondoka)
Miriam:
(anarudi rumande)
0 Comments