SCENE 51: -
(asubuhi ya siku ya jumapili kama ilivyo kawaida ya Raymond kukaa
bustanini kwake akiperuzi mtandaoni na kipenzi chake anafanya usafi na kazi nyingine.
Nje ya geti kunasikika honi na haraka Ramadhani anafungua geti hilo na kuruhusu
gari la Christina kuingia ndani. Christina anaegesha gari lake kisha anashuka
kwenye gari, Angelina nae anatokea ndani hivyo wanakutana)
Angelina: shikamoo...Dada
Christina: marahaba…Raymond yuko wapi?
Angelina: bustanini… (Anamuongoza njia)
Christina :( anamfuata)
(Wanafika)
Raymond :(
akiwa hajamuona Christina anamshika mkono Angelina na kupeleka kidevuni kwake)
we mbona kama bado unaniogopa? mimi ni mumeo unajua(anacheka)
Angelina: dada Christina anakuja
Raymond :( anamuachia)
ndo maana unaogopa au?
Christina :( anafika
alipo) habari yako Raymond
Raymond: salama shikamoo…?
Christina: marahaba...za hapa?
Raymond: nzuri tu… (kimya kidogo) karibu uketi
Christina :( anaketi
kiti cha pembeni kidogo na Raymond)
Raymond: karibu
Christina: Nina mazungumzo na wewe…
Raymond: okay…karibu nakusikiliza… (Anaacha kuperuzi na kumsikiliza)
Christina: wawili Mimi na wewe, naomba Angelina
utupishe
Raymond:(anacheka kidogo) labda hujui au labda
umesahau…ni kwamba, Angelina ni mchumba wangu yaani mke mtarajiwa sasa
unapomwambia mazungumzo ni yetu na atupishe unamvunjia adabu unajua? hakuna cha
kufichana kati yangu mimi na Yeye...
Christina: samahani
Angelina: ngoja nikalete vinywaji (anaondoka)
Christina: sorry
Raymond :( anamuangalia
sana) enhe sema shida yako tafadhali
Christina: naomba unisamehe
Raymond: nitakusameheje huku sijui kosa lako?
Nikusamehe nini?
Christina:(anacheka
kidogo) maisha bwana…nilijaribu kukurudisha akili yako nyuma miaka miwili
ili ukumbuke penzi letu na lengo lilikuwa nikurudishe kwangu na tufunge ndoa
iliyokuwa imepangwa kama miezi nane iliyopita (anacheka) ila kwa bahati mbaya, moyo ukazidi akili… (Kimya huku anamuangalia Sana Raymond)
ukadhihirisha kuwa moyo wako ni wa Angelina na hata tufanye nini hatuwezi
kubadili hilo
Raymond :( anamuangalia
Sana)
Christina: najua hunielewi
Raymond: nakuelewa…vizuri Sana Christina na
tulikuwa tunajiuliza nani atakuwa amenifanyia hivyo…akili ilikuwa sio yangu kwa
siku kumi zilizopita sijui nilisumbua watu hapo sijui
Christina: naomba unisamehe sana Raymond nilikosea
sana
Raymond: nimeshakusamehe ile tu wewe kugundua
ulichofanya ni kibaya tayari umeshatubu makosa yako nimekusamehe mama…yaishe
Christina :( analengwa
na machozi) its funny right? Yaani tumekaa almost six years lakini hatukuwa
na mapenzi baina yetu kila mtu alikuwa anawaza yake mimi nilimpenda Peter na
wewe njiani ukakutana na Angelina na kumpenda sana, its funny eti eeh
Raymond :( anacheka
kidogo) sometimes ni hivyo…maisha ndivyo yalivyo...Unaweza kukaa na mtu
muda mrefu halafu sio ubavu wako na ukakutana na mtu wiki mbili tu akawa ubavu
wako
Christina :( anacheka)
ni kweli
Raymond :( anacheka
pia) nimefurahi umejua hilo…wewe ni mwanamke mrembo you deserve pure happiness...kama
mimi nilivyopata furaha kwa kukutana na Angelina na nikampenda regardless
hatufanani kitabaka
Christina: hata Mimi na Peter
Raymond: exactly…go girl…go and fight for your love
and get it back wewe na Peter mnapendana na kila mtu anajua hilo…
Christina:(anaguna)
samahani tena
Raymond: nini tena?
Christina: muda wote huo nilikuwa natembea na baba yako,
nilifanya vile sababu ya uroho wa mali na pesa… (anasikitika) yaani najisikia vibaya sana...
Raymond: its okay Christina…na sijui nikwambieje naishukuru
ile siku hata kama ilikuwa ni ngumu kumeza ila baada ya hapo matokeo yake
yalikuwa mazuri (anacheka kidogo)
baada ya hapo badala mahusiano yangu na baba yangu kuwa mabaya yamekuwa mazuri
na baba amekuwa akinisikiliza sana…yaani amebadilika sana mpaka mama anashangaa
…
Christina:(anacheka)
Raymond: ilikuwa mbaya lakini imetoa matokea mazuri
sasa mimi na baba yangu hatugombani hovyo...Amekuwa hana gubu Kama zamani
Christina: ndo hivyo bwana mambo hubadilika na
unakuta kitu kidogo ndo kimesababisha
Raymond: kweli kabisa
Christina:(kimya
huku anamuangalia) nitakukumbuka lakini maana nilikuwa nimekuzoea sana
Raymond: pamoja na yote tutabaki kuwa marafiki
wazuri tu my dear
(wanakumbatiana)
Angelina:(anakuja
akitokea ndani akiwa amebaba vinywaji kwenye trei anapoawaona anakosa raha na
wivu unampanda anaamua kurudi ndani)
Christina:(anamuona Angelina) mama mwenye nyumba
unaenda wapi?
Angelina:(anarudi) nilikuwa naenda ndani
Christina:(anamfuata
na kuchukua glasi moja ya kinywaji) yaani juisi tu umeenda kuchukua mwaka
tangu tumeanza mazungumzo mpaka tumemaliza
Raymond:(anacheka)
Angelina: nilikuwa natengeneza juisi
Raymond:(anachukua
kinywaji) muda wote huo?
Christina: Angelina naomba umtunze Raymond na
usipomtunza nitamrudia
Angelina:(anacheka)
Raymond:by the way…nichukue nafasi hii
kukukaribisha kwenye harusi ya Edmond na Catherine
Christina: oh (anaweka
kinywaji mezani) nitakuja...ni lini?
Raymond: mwezi ujao
Christina: sawa…nitakuja…
Raymond: karibu sana...
Christina: sawa…ngoja niwaache jamani
Raymond: haya bwana sie tupo
Christina: nawatakia kila la kheri katika mipango
yenu ya harusi na Maisha pia
Angelina na Raymond: asante sana (wanatabasamu)
Christina: (anaondoka)
Angelina: huyu ni Christina?
Raymond: ndo yeye...au kwanini usimkimbilie
umuulize
Angelina: amekuwaje?
Raymond: nahisi amechoka tu
Angelina: kwakweli
Raymond:(anampakata)
Angelina:(anamkalia
huku anamuangalia kimahaba)
Raymond: unataka kufanya nini
Angelina: wapi?
Raymond: nimeagiza msichana mwingine…
Angelina: umekumbuka hilo?
Raymond: Ramadhani aliniambia kuwa nilimuagiza
nikajua labda nilimuagiza wakati akili imehamia miaka miwili iliyopita
(wote wanacheka)
Raymond: sasa huyo dada akija nataka uwe unafanya
kitu Fulani
Angelina: mimi si hausigeli?
Raymond: ulikuwa…ila sasa wewe ni mchumba wangu na
ninakupenda sana na utakuwa mke wangu hivi karibuni nataka uwe na kazi yako
Angelina: Mimi unajua sijasoma
Raymond: ah akili tu mke wangu…utaniambia unataka
kufanya nini?
Angelina: sawa...Nitakuambia
Raymond: enhe…nambie
Angelina: mama amefurahi sana kukuona umerudi
kwenye hali yako ya kawaida
Raymond: mama yako au mama yangu
Angelina: mama yako
Raymond: eti eeh… (Anamuangalia usoni) yaani wewe mrembo
Angelina :( anaona aibu)
Raymond: nataka nikakununulie gauni moja matata kwa
ajili ya harusi ya Edmond na Catherine
Angelina: Asante, nitafurahi sana
Raymond: eti ee (anambusu ishara ya upendo wake kwa Angelina)
(Wanaonekana wapo kwenye mahaba mazito Sana)
0 Comments