SCENE 52: -
(Jioni
nyingine tulivu na njema jua linaanza kuzama, Christina yupo nyuma ya nyumba
yao ameweka kiti na anaonekana ni mtu anayehitaji utulivu maana amekaa kipweke
sana, anasoma kitu Fulani kwenye simu yake)
Christina: mambo ni mengi sana kwenye hii dunia...
(anashusha pumzi) kila mtu ana mtu
wake kasoro mimi…(anasikitika)Peter simuelewi,
nimeshaamua kuachana na Raymond lakini pia hata baba yake Raymond nimeamua
kumuacha watu na familia zao…tusije tukajikuta sisi ndo tunaoharibu nyumba za
watu acha tu nitulie kwanza ukiwa ni mtu wa kulazimisha vitu huwezi kuwa na
Amani
(Sauti nzito ya kiume inatokea nyuma yake)
Sauti: mambo...Nimekutafuta sana
Christina :(
anageuka) wow (anafurahi Sana) Peter…
Peter :( anatabasamu)
Tina… (Anamuendea na kumkumbatia)
Christina :( anamkumbatia
pia) umekuja?
Peter :( anavuta
kiti anakaa) unadhani nisingekuja? Tina umenifukuza mara nyingi sana ila
siwezi kuondoka na kuenda mbali mpenzi wangu nakupenda sana
Christina :( anatabasamu)
mbona mara ya mwisho uliniambia kuwa hunitaki tena?
Peter: ah…niliona tu umemkazania Sana Raymond
Christina: nini kimekurudisha?
Peter: siwezi kuishi bila wewe Christina sijui
umenipa nini nashindwa kabisa kuishi bila wewe…nipo tayari kuwa hata spea tairi
kwako ilimradi tu usikae mbali na mimi
Christina :(
anacheka kisha anaguna) eti spea tairi…una vituko wewe
Peter: vituko tena mwenzio nateseka wewe unaniambia
nina vituko?
Christina: Peter nakupenda pia tena sana mpenzi
wangu…Ni kweli nilikuwa namkomalia sana Raymond ni kwasababu kwanza alikuwa
mchumba wangu wewe si umenikuta na Raymond
Peter: ndio
Christina: lakini pili niliona Raymond ni wangu tu
yaani hata kama simpendi kimapenzi atabaki kuwa wangu maana nina mamlaka juu
yake…(anasikitika)nilikosea sana kama
shangazi alivyosema kuwa Raymond ni wa Angelina, na Bembele ni wa Glory na Peter
ni wa Christina
(Wanacheka)
Christina: mapenzi hayalazimishwi halafu mtu
akishapenda haijalishi kapenda nani kilema, maskini au tajiri kitu upendo kinabaki
kuwa upendo tu...kwa mfano Raymond si alikuwa mchumba wangu tumekaa kwenye
mahusiano kwa muda ila tukawa hatupendani kuna kipindi mimi nikakutana na wewe
nikawa nalazimisha niendelee kumpenda Raymond
Peter :( anamsikiliza
kwa makini sana)
Christina: hata ningefanyaje nisingeishia na Raymond
maana mimi sikuwa nampenda napenda tu mali zake na jina lake hapa mjini lakini
pia hata yeye njiani akakutana na Angelina akampenda tena akampenda sana kuliko
hata alivyowahi kunipenda mimi, baba yake akapinga sana lakini wapi, mimi
mwenyewe nikapinga sana kwa kujaribu kuyaharibu mapenzi yao yaani mpaka
nilimroga Raymond kwa kujaribu kurudisha akili yake nyuma lakini wapi
Peter: aisee
Christina: kwahiyo mapenzi bwana…sijui nisemeje
Peter: nakuelewa sana mpenzi
Christina :( anavuta
pumzi kama mtu aliyechoka sana) nakupenda sana Peter wewe ni wa kwangu
Peter: hautarudi kwa Raymond
Christina: hapana…tumeshaachana nimegundua kuwa
wewe ni wangu na Raymond ni wa Angelina
Peter:(anatoa
kitu Fulani mfukoni)
Christina:(anatabasamu)
nini Peter?
Peter:(anapiga
goti moja)
Christina: sikuelewi unajua?
Peter: siwezi kuishi bila wewe Christina...miaka
mitatu iliyopita pamoja na kwamba nilijua wewe ni mpenzi wa mtu mwingine
nilikupenda hivyo hivyo
Christina:(anatabasamu)
jamani maajabu haya
Peter: nilikusubiri ugeuze moyo wako na uwe
kwangu…nilitembea na pete hii mara zote mara baada ya kukupenda kwa dhati …sina
mali ila ninakuhakikishia nitakutunza Christina kama mke wangu na mama wa
watoto wangu
Christina: Oh My God!!!(anataka kulia)
Peter: nitajitahidi niendane na maisha
uliyoyazoea…nitakuwa mume mwema hata wewe utaona…
Christina: nakupenda sana Peter (Analia)
Peter: Christina mpenzi…Will You Marry Me?
Christina: yes…
Peter:(anamvalisha
pete ya uchumba kisha anamkumbatia) …asante sana mpenzi kwa
kunikubali…asante pia kwa kutambua thamani ya upendo kwamba mapenzi
hayalazimishwi na wala mapenzi hayabagui…karibu katika ulimwengu wangu Christina
Christina:(anambusu)
asante baby
(Shangazi, mama na baba yake Christina wanachungulia tukio lote kupitia
dirisha kubwa linalotazamana na walipo Christina na mchumba wake mpya)
Mama:(anacheka)
sasa mwanangu amekuwa… (anacheka tena)
kama filamu eeh kamkomalia Raymond kwa muda kweli…mwisho wa siku yeye mwenyewe
kaona ujinga
Baba: hamna lolote nyinyi ndo mlikuwa mnapa bichwa
Shangazi: yeye mwenyewe ndo alikuwa anatupa bichwa
(wanacheka)
Mama: kiukweli yeye na Peter wanaendana ingawa
alikuwa anaendana na Raymond pia ila
Baba: ila nini mbona hueleweki?
Mama: Raymond na Christina wameachana kimzaha
Shangazi: wale ilikuwa imeandikwa tu ni lazima
waachane ...ila (anaguna)mtoto kajua
kumpambania mwanaume ambae hata alikuwa hampendi
Mama: yaani…(anacheka)yaani
ukimkuta alivyoshupaa utasema anampenda kuliko anavyompenda huyu...
Baba: kwahiyo mnamsema vibaya Raymond
Shangazi: wala hatumsemi vibaya kaka wa watu nay
eye ni maisha tu...ni mapenzi tu
Baba: uzuri wake yeye alijiengua mapema alipojua tu
kuwa kamuangukia msichana wake wa kazi akaona aseme tu mapema ila mwenzenu huyo
(anamnyooshea kidole Christina)
alikuwa anataka kote...
Shangazi: ingemgharimu na bora tu alivyojifanya
mjinga ona sasa hivi anavyofurahi
Baba :( anatabasamu)
hivi Raymond anamuoa lini huyo hausigeli?
Mama: wewe nae hiyo ni kazi ya kina Bembele huko
wewe subiri mahari ya mwanao
Shangazi: umeona eeh…(anacheka)nani alijua kama siku moja sisi na kina Bembele tutakuwa
tunapanga mipango ya harusi kwa pamoja? ila sasa sio kwamba watoto wetu
wanaoana ni kwamba watoto wetu wanaoa na kuolewa na watu wengune kwa wakati
mmoja
Mama :( kwa
shangazi) wifi umejuaje kuwa Peter anamuoa Christina hivi karibuni
Baba: si ametuambia…
Shangazi: yeye ndo aliyenishawishi kumwambia Christina
aachane na Raymond sio wake…yeye ndo aliyehakikisha Christina anajitambua…na
kuacha utoto
Mama: Kumbe…
Shangazi: ndo hivyo na yote hiyo ni kusema kuwa
anataka amuoe atulie
Baba: Safi Sana
(Wanarudi sebuleni na kuendelea kufanya mambo yao)
Peter: I love you so much
Christina: nakupenda pia kipenzi cha moyo wangu
(Wanakumbatiana)
0 Comments