SCENE 51: -
NYUMBANI
KWA VINCENT:
(Majira
ya saa mbili usiku Vincent amekaa nyumbani kwake akiangalia taarifa ya habari
huku anapata kinywaji chake cha baridi huku matamanio ya moyo wake yanaonekana
machoni kwake kuwa anatamani kuwa na watu pembeni yake)
Vincent:
nimewakumbuka wanangu sana mmoja nimeishi nae sema akanikimbia lakini mwingine
sijawahi kumuona (anasikitika) sina
mke namkumbuka sana Mary sijui nifanyeje nimezungumza nae ila anaonekana ana
mawazo sana juu ya mwanae ambae ni mwanangu
(mlango unagongwa)
Vincent:
nani usiku huu? (ananyanyuka na kufungua
mlango) Colton
Colton:
baba (anaingia huku Analia)
Vincent:
mwanangu shida nini?
Colton:
nimechoka baba…nimechoka kufanya dhambi
Vincent:
sielewi unachoongea
Colton:
dad
Vincent:
embu kaa unywe kwanza maji kisha uniambie
Colton:
(anakaa)
Vincent:
(anamletea glasi ya maji) kunywa
halafu kaa utulie
Colton:
(anapokea kisha anakunywa) asante
baba
Vincent:
usijali…tulia…
Colton:
mimi sio mtu mbaya baba ni ujinga wangu tu ndo ulisababisha haya
Vincent:
umefanyaje?
Colton:
nimejifanya nimekufa ili mdada wa watu aende jela
Vincent:
hiyo ni mbaya mwanangu ila bora sasa limeisha au?
Colton:
sijui baba ila tu nimeona nitoroke nije nikae na wewe
Vincent:
umefanya vyema maana hata mimi nimempata yule mama aliyemzaa mdogo wako amesema
nionane nae ili nikutane na mwanangu ingawa anasema mwanangu yupo jela sasa hii
ni wiki ya pili
Colton:
huwezi amini hata mimi tangu nimefanya huo ujinga hii ni wiki ya pili
Vincent:
son, embu nisindikize kesho tukakutane na mama mtoto ili atupeleke kwa mdogo
wako mwanangu utajisikia vizuri…ukimuona mdogo wako nimekuwa nikiongelea hilo
kwa miaka sasa
Colton:
ndio baba…
Vincent:
ila sijaelewa kitu umesema kuwa umejifanya umekufa enhe ikawaje baada ya
kujifanya umekufa?
Colton:
baba nilikaa mochwari kwa usiku kucha palipokaribia kukucha nikaja kuchukuliwa
na askari mmoja akanitoa
Vincent:
mochwari wewe mtoto?
Vincent:
ndio baba mochwari
Vincent:
aisee watoto utasema huna kwenu…huku una kwenu na mimi baba yako nina nyumba za
kutosha za wewe kulala sasa ukaenda kulala mochwari (anasikitika) enhe kwahiyo wakakuzika au?
Colton:
hapana …askari waliolipwa na Ariana wakanitorosha ila walitengeneza kaburi
Vincent:
(anashangaa)
Colton:
baba nimefanya kosa najutia
Vincent:
jutia mwanangu umefanya jambo baya sana kwanza ni dhambi…kumbuka una mdogo wako
wa kike utajisikiaje mtu akimfanyia kama ulivyomfanyia huyo binti?
Colton:
baba tufanyeje?
Vincent:
aisee kwani kesi inaanza kusikilizwa lini?
Colton:
baada ya wiki mbili
Vincent:
tuna muda wa kujifikiria cha kufanya
Colton:
maskini Miriam…
Vincent:
ndo nani
Colton:
huyo dada…yupo jela kwa kosa ambalo hata sio kosa
Vincent:
nikupe nini ili ulale mwanangu? Kesho ukiamka utaenda kwa dada yako mtaongea
atakushauri cha kufanya
Colton:
yes, dad…ngoja nikaoge nilale
Vincent:
hauli?
Colton:
No dad…sili lakini kabla ya kesho natamani kwenda kanisani nimuombe Mungu wangu
msamaha kwa kujifanya nimekufa…ili mtu mwingine ateseke
Vincent:
pole mwanangu
Colton:
ila kwanini naumia sana…kwanini naumia kupita kiasi?
Vincent:
sababu wewe sio mtu mbaya hata kama tukilazimisha
Colton:
(machozi yanamtoka)
Vincent:
(anamfuta machozi) acha kulia
mwanangu…(anamkumbatia) baada ya
kuonana na dada yako tutafanya mpango huyo binti uliyemsingizia atoke gerezani
Colton:
okay dad… (ananyanyuka na kwenda chumbani
kwake)
Vincent:
maskini mwanangu ila najua kesho akikutana na mdogo wake atakuwa sawa tu
0 Comments