SCENE
49: -
NYUMBANI
KWA KEN
(Majira ya saa mbili na robo
usiku, Ken na familia yake wamekaa wanapata chakula cha usiku, kila mmoja
anaonekana hana raha)
Keddy:
yaani sijisikii kula kabisa jamani
Ken:
jitahidi mke wangu…kula kidogo Miriam anatuhitaji tukiwa wote tuna nguvu
Keddy:
maskini mwanangu…
Ariana:
(anajisemea moyoni) eti mwanangu…(anafyonza)
Mary:
anaendelea vizuri
Ken:
enhe asubuhi alijisikia vibaya…umeenda kufuatilia shida ni nini? Maana sikuweza
kwenda kwa sababu presha yangu ilipanda…
Mary:
pole sana…kaka niliwapeleka ndugu zangu wakamuone…na pia nilimpeleka baba yake
Keddy:
kumbe mlikuwa mnawasiliana?
Mary:
hata Miriam ameniuliza hivyo…No sikuwa nina mawasiliano nao siku moja mama
alinipigia akasema baba Miriam ananitafuta sana…sasa sijui labda alienda
nyumbani nikakutana nae ndo nikaona nimpeleke akamuone Miriam maana alikuwa
anatamani kumuona Miriam
Ariana:
(anabenjua midomo)
Mary: Miriam
amefurahi sana
Keddy: (anatabasamu)
Mary:
halafu kuna habari tumekutana nayo
Ken: ipi
tena?
Mary: ni
mjamzito
Ken:
acha bwana
Keddy:
ndo maana alijisikia kichefuchefu
Ken:
huwezi kuamini hata sijakasirika sijui kwanini
Ariana:
(ananyanyuka) nimeshiba
Keddy:
uko sawa Ariana?
Ariana:
yeah (anaingia chumbani kwake)
Keddy:
shida nini?
Mary:
atakuwa ameshiba kweli muache akapumzike…tuna mambo mengi sana ya kufikiria
kumbuka yeye ni dada yake Miriam kama tulivyo hatuna hamu ya kula hata yeye
hana hamu ya kula
Ken:
kuna kitu hakiko sawa sijui ni nini ila nahisi kuna kitu hakipo sawa
Keddy:
kama nini baba Ariana?
Ken:
sijui
(Mary na Keddy wanaangaliana)
Keddy:
sikuelewi
Ken:
huwezi
Mary:
fafanua
Ken:
tuachane nayo
Keddy:
haya bwana kama hutuambii
Ken: ila
kwa yote nimefurahi tumezeeka
(wanacheka)
Keddy:
kadada anatuletea ka Miriam kadogo
Mary:
katakuwa ka Jeremy maana hampendi Jeremy huyo
Keddy:
ee kweli
Mary:
anamkataa
Ken: eeh
mtoto ana balaa huyu…Jeremy anasemaje
Mary: si
unamjua alivyo mpole anafukuzwa anaondoka lakini kesho anarudi tena
(wanacheka)
Keddy:
habari hii imetusaulisha machungu yaani kisema cha baba Ariana wala hata
sijachukia…yaani hata kama majirani watatunyooshea kidole lakini hii habari
naamini imemfurahisha hata Miriam
Mary:
kabisa
(Huku ndani alipo Ariana)
Ariana: (Analia) Miriam ana mimba ya Jeremy ana
mimba ya Jeremy yule Malaya amepata nafasi tena ya kuwa na furaha halafu sasa
kama kawaida watu wanamfurahia kwani mimi nina balaa gani hapa
nimechanganyikiwa na mengi siku ile sikuukuta mwili wa Colton sijui yuko wapi
yaani hata sielewi…halafu nimekaa nakula Napata habari ya kwamba Miriam
mjamzito…oh comeon they must be kidding…(anajitupa
kitandani) embu ngoja nihakikishe hizi habari maana huyu Mary anajifanyaga
kiropo sana (anachukua simu yake na
kumpigia Jeremy)
(Simu inaita)
Jeremy: (anapokea) hello shem
Ariana:
ah…yes za kwako?
Jeremy:
ah kama unavyojua mambo yangu sio mazuri sana…ila namtukuza Mungu nipo napumua
Ariana:
okay ulienda kumuona Miriam?
Jeremy:
ndio hata hapa nimetoka kumuona siwezi kumuacha hasa kwenye wakati huu…
Ariana:
wakati gani?
Jeremy:
Miriam is pregnant with my child…I swear Ariana iam so happy…penzi letu limezaa
matunda…
Ariana:
(anachukia sana)
Jeremy:
Miriam is pregnant with my child
Ariana:
sasa nini faida ya kuwa na ujauzito huku baada ya wiki moja anaenda kuhukumiwa
kifo?
Jeremy:
(anacheka)
Ariana:
unacheka nini?
Jeremy:
embu tuiachie mahakama iamue juu ya hilo
Ariana:
ushahidi wote unaonyesha ameua
Jeremy:
eeh ahata mimi niliona kuwa dogo ushuhuda wote unamuonyesha kuwa ni muuaji…ila
tusubiri si bado siku kadhaa tu?
Ariana:
Miriam atakufa get that in your head Jeremy and move on
Jeremy:
nitakuwa na Miriam hata mpaka siku ananyongwa na kama ikiwezekana I will live
in her memories I will refuse to forget her…she is the love of my life
Ariana:
bora yake
Jeremy:
yes…enhe ulinipigia simu kuniambiaje?
Ariana:
nothing…
Jeremy:
hujafurahi kusikia kuwa mdogo wangu amenibebea mimba (anatabsamu) you should see her…kang’aa kamimba kamempenda kweli
yaani…(anacheka)
Ariana:
(anakata simu kwa hasira) shit…that
woman…damn her…I hate her… (anafuta
machozi) ni sawa lakini acha wajipe moyo kwamba wataomba mahakama
wampunguzie adhabu kisa ana mimba…atahukumiwa tu na mtoto ataachwa kama yatima
nikiwa mama yake wa kambo nitamtesa sana yaani hawataamini… wajipe moyo tu
(Huku kwa Jeremy)
Jeremy:
lets wait for that day…siku sio nyingi…dunia itashuhudia Ukuu wa Mungu …watu
watakiri kwa vinywa vyao kuwa MUNGU MKUU kwa maajabu atakayoyaonyesha…Mungu
wetu sio kiziwi na wala hataacha mwenye haki aibike…tusubiri hiyo siku…oh my
love thank you for ths gift najua tumeenda vibaya tumezini ila Mungu amelipanga
hili...nakupenda Miriam wangu…Mungu naomba uwe nasi siku ya hukumu…hakimu
atusikie tunachosema
(Kwa Ariana)
Ariana:
nina uhakika watashindwa watu watakuwa wanazimia kama nzi siku hiyo acha
wajishaue…yaani nitacheka siku hiyo nitafurahi sana na Miriam na limimba lake
hilo litoto la laana watakufa pamoja (anacheka
kwa nguvu) naisubiri kwa hamu sana siku ya hukumu…
0 Comments