MUNGU MKUU 47


 

SCENE 47: -

BAADA YA MWEZI MMOJA: -

MAHAKAMANI: -

(Asubuhi iliyo njema kwa watu kasoro kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Miriam ambao wana huzuni nyingi kwa lile lililopo mbele yao, Ariana nae yupo na anajifanya kuwa na huzuni kama walivyo wengine)

Mwanasheria: (anashusha pumzi) hata sijui nifanyeje

Jeremy: kwanini?

Mwansharia: rekodi inayoonyesha rekodi ya simu za Miriam zimepotea

Ariana: Mungu huyo yaani mlikuwa mnanisingizia mimi kuwa niliongea na Miriam jioni ile ona sasa yamepotea

David: (baba yake Jeremy) nani alikusingizia?

Ariana: si Miriam

David: aisee

Keddy: (amekonda kwa mawazo) mimi sijui nachotaka mwanangu tu awe huru ameteseka mwezi mzima

Ken: acha tu

Mary: mimi namuachia Mungu tu naamini mwanangu kwa vyovyote vile atakuwa huru

Mwanasheria: hatuna cha kujitetea kwa upande wetu…na hilo ndo tatizo

Vanessa: vipi nguo za Miriam alizokuwa amevaa jioni ile?

Mwanasheria: haijulikani ziko wapi…

Mary: Mungu wangu mwanangu

Mwanasheria: njooni ndani naona inataka kuanza

(Wanaingia, wote wanakaa upande atakaokaa Miriam)

 Miriam: (anaingia akiwa na unyonge, pembeni yake kuna askari magereza wawili)

Mary: (anamuangalia mwanae) Mungu ulinipa mtoto pekee huwezi kumchukua mapema huwezi kumchukua mwanangu nakuomba Mungu…mama na baba yangu wako wapi niliwapigia simu wakasema wanakuja kumuona mjukuu wao kwa mara ya kwanza tangu azaliwe wako wapi jamani…wangekuja labda wangenipa nguvu (anapokea ujumbe kwenye simu yake) dada…amesema wapo hapo nje… (kwa mwanasheria) naomba nikawachukue watu hapo nje mara moja…

Mwanasheria: sawa ila usichelewe hakimu akiingia usiingie

Mary: (anatoka haraka anapofika nje anamuona dada yake pamoja nawazazi wake) asante kwa kuja nilikuwa nawahitaji sana

Mama: hujambo mwanangu?

Mary: Mary: shikamoo mama, shikamoo baba, shikamoo dada

(Wanaitikia)

Dada: pole mdogo wangu ila Mungu yupo

Mary: asante…haya twendeni ndani…

(Wanaingia)

Hakimu: (anaingia)

Watu: (wanasimama)

Hakimu: (anaketi)

Watu: (wanaketi pia)

Dada: (kwa Mary) mtoto ni yule pale mbele…

Mary: (kwa kunong’ona) ndio

Dada: mnafanana

Mary: (anatabasamu) Huyu (anamshika Jeremy) mkwe wetu

Dada: oh, baba hujambo?

Jeremy: sijambo shikamoo mama

Dada: marahaba… poleni yatapita tu haya

Jeremy: nina uhakika

Mary: haya tusikilize

Mwendesha mashtaka: Miriam Kennedy…anashtakiwa na jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kosa la kumuua kwa kumshambulia kwa kisu bwana Colton Mshana usiku wa tarehe 13/04… (kwa Miriam) kweli sio kweli

Miriam: (amekaa pembeni ya mwanasheria wake) sio kweli

(Minong’ono)

Hakimu: naomba utulivu tafadhali

(Utulivu)

Mwendesha mashtaka: basi tukusikie mwanasheria upande wa mshtakiwa

Mwanasheria: (ananyanyuka) asante mheshimiwa hakimu…mnamo tarehe 13/04 saa moja jioni mteja wangu alipigiwa simu na dada yake akitakwa waonane kuna maongezi kidogo wanataka wafanye bila kusita mteja wangu alichukua usafiri mpaka eneo waliokubaliana alipofika dada yake alimwambia asubiri anakuja lakini ghafla mteja wangu alisikia mtu anambana pua na hatimaye akaanguka chini alipoamka alikuta marehemu amelala pembeni yake na mikono yake imejaa rangi inayofanana na damu

(Minong’ono)

Hakimu: (anagonga meza kuamuru utulivu)

(Utulivu)

Mwanasheria: hajakaa vizuri polisi wakafika na kumkamata kwa kosa la mauaji… ni hivyo tu mheshimiwa (anainama kisha anaenda kukaa)

Hakimu: mwanasheria upande wa Jamhuri

Mwanasheria 2: (ananyanyuka) asante mheshimiwa (kwa mwanasheria 1) umesema kuwa mteja wako alipigiwa simu na dada yake…

Mwanasheria 1: ndio

Mwanasheria 2: wewe ni mwanasheria wa utetezi …tuone basi rekodi za simu ya huyo mteja wako

Mwanasheria 1: zimepotea

Mwansheria 2: zimeenda wapi?

Mwanasheria 1: siwezi kufahamu (anageuka na kumuangalia Jeremy)

Mwanasheria 2: hujui eeh hivi kwanini nakuuliza wewe … (kwa hakimu) naomba nimuite mtuhumiwa ndo nimhoji maana yeye ndo alikuwepo

Hakimu: fanya hivyo

Miriam: (ananyanyuka na kwenda kizimbani)

Mama Mary: (anamuangalia kwa upendo) mjukuu wangu mrembo…

Jeremy: (anamuangalia kwa upendo sana) be strong my love…

Miriam: (amesimama kizimbani)

Mwanasheria 2: mtetezi wako amesema kuwa ulipoamka ukakuta rangi inayofanana na damu…

Miriam: ndio

Mwanasheria 2: ulijuaje?

Miriam: ilikuwa sio damu…

Mwanasheria 2: unatudanganya ee

Miriam: hapana

Mwanasheria 2: (analeta nguo za Miriam) hizi ndo nguo zako?

Miriam: ndio

Mwanasheria 2: zina damu na damu yenyewe ni ya mwanadamu na mwanadamu huyo ni Colton

(Minong’ono)

Hakimu: (anagonga meza)

(Utulivu)

Mwanasheria 2: (anampelekea nguo hizo hakimu)

Hakimu: (anaziangalia) kweli zina damu na vipimo vinaonesha kuwa ni damu ya Colton

Mwanasheria 2: sasa je unapotuambia kuwa uliona rangi

Miriam: haki ya Mungu tena nasema ukweli

Mwanasheria 2: unasema uongo kujitetea

Miriam: sio kweli

Mwanasheria 2: nimemaliza… (kwa hakimu) mtuhumiwa anadanganya na anafanya juu chini kujitetea ili aepuke adhabu naomba mahakama yako tukufu impatie mtuhumiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wote…alimuua yule mwanaume ili atunze penzi lake na hawara yake mwingine mwenye pesa Zaidi

Jeremy: mimi hawara tena? (anatikisa kichwa)

Miriam: kila neno unaloongea ni uongo…ninampenda mwanaume aliyenichumbia na pia sikuwahi hata siku moja kumsaliti kwa kumuangalia mwanaume mwingine huyo Colton nilikuwa simfahamu nilimfahamu siku alipoletwa na dada Ariana

(Minong’ono)

Hakimu: (anagonga meza kuamuru utulivu)

(Utulivu)

Mwanasheria 2: usitumie nguvu nyingi maana tayari imeshajulikana kuwa wewe ni muuaji na sababu yake ni hiyo

Miriam: usiusemee moyo wangu

Hakimu: (kwa Miriam) acha kujibizana na mwanasheria…

Ariana: (anacheka)

Jeremy: (anamuona) sasa nini kinachekesha hapo?

Ariana: eeh jamani kwahiyo hata kucheka napangiwa

Jeremy: Mungu akusamehe Ariana

Ariana: embu niacheni mie

Dada yake Mary: (anamuangalia Miriam) maskini ameshalia mpaka amekinai…

Miriam: (anataka kutapika)

Hakimu: naomba niahirishe hili mpaka baada ya siku kumi na baada ya kusikia ushahidi wote mahakama hii ipo tayari kutoa hukumu yake labda kama kuna mabadiliko ambayo naamini hayapo (anagonga meza anasimama na kuondoka zake)

Watu: (wanasimama pia)

Jeremy: (anamkimbilia Miriam) baby are you okay… (anamkumbatia)

Miriam: najiskia vibaya…

(Askari magereza wanamchukua na kuondoka nae)

Post a Comment

0 Comments