SCENE 50: -
(Asubuhi ya kesho yake Raymond anafika ofisini kwake akiwa na furaha
kupita kiasi)
Raymond: Rachel, Pendo…mambo zenu
(Rachel na
Pendo wanashangaa)
Rachel: kwani mwenzetu vipi?
Raymond: kwani vipi?
Pendo: mkurugenzi uko sawa?
Raymond: kabisaaaaa…
Glory:(anakuja
akitokea ofisini kwa Raymond) bosi…
Raymond: umeanza...
Glory: haya mwanangu…za siku?
Raymond: siku gani? Oh, sawa nilikuwa likizo…Angelina
kaniambia
Rachel: mwenzangu mbona hatukuelewi…mara ya mwisho
umeondoka hapa ulikuwa hata hutukumbuki can you imagine mpaka mlango wa kutokea
ulikuwa umeusahau...Yaani unatushangaa...Tunakuambia wewe ni dokta unakataa
unasema kuwa bado unasoma yaani ulikuwa kama umepoteza kumbukumbu
Raymond: yaani hata siwaelewi kabisa mnajua anayway
nipokeeni basi
Pendo: hujaja na zawadi, tutakupokea nini sasa?
Raymond: nimetoka likizo, nipokeeni hata begi
jamani
(Glory, Pendo na Rachel wanaangaliana)
Pendo: wewe bwana sisi hatukuelewi…umeondoka hapa
umetusahau unatuuliza kabisa kwani nyinyi ni kina nani?
Glory:au mwanangu ulikuwa unatudeshi
Raymond: Mimi sijui… (Anaelekea ofisini kwake) nileteeni chai
Glory: sawa mwanangu (anaelekea jikoni)
Raymond :( anaingia
ofisini) oh it’s good to be back… (anajitupa
kwenye sofa) ngoja nimpigie Edmond(anapiga)
(Simu inaita)
Edmond: Mond…
Raymond: mambo Mond?
Edmond: poa…
Raymond: yaani nimekumisi wewe jamani… (Anaguna)
Edmond: jamani wewe nae si tumeonana juzi tu hapo?
Raymond: Mimi na wewe?
Edmond: ndio
Raymond: yaani hapa nilipo siwaelewi kabisa…kila
mtu ananichanganya...Anyway mi nimekupigia simu kale ka inshu vipi brother?
Edmond: kapi?
Raymond: kupeleka mahari kwa kina Angelina bila
yeye kujua
Edmond :( anacheka
kidogo kisha anaguna) si umeshamwambia
Raymond: wewe…sijathubutu kumwambia
Edmond: Raymond unajua sikuelewi?
Raymond: hata mimi sikuelewi...
Edmond: mimi nani?
Raymond:si Edmond
Edmond: nini kipo mbele yangu?
Raymond: harusi yako wewe na Catherine
Edmond: kabla ya?
Raymond: harusi yangu na Angelina
Edmond: Angelina ni nani?
Raymond: kipenzi cha moyo wangu na pia ni mchumba
wangu natarajia kumuoa mama na baba tayari wamesharidhia
Edmond: ulikutana nae wapi?
Raymond: kwangu…ulimleta Kama mfanya kazi wa ndani
mimi nikampenda nakuanza nae mahusiano
Edmond: Kama wiki moja na nusu ulikuwa nae wapi?
Raymond: Serengeti
Edmond: baada ya hapo
Raymond: sijui
Edmond :( anajisemea
moyoni) amekumbuka basi akili yake iko sawa sasa hivi
Raymond; kwani vipi? Mbona unanihoji maswali Kama
unataka kunipa kazi au shemeji ndo kakwambia tukitaka kuoa kwao lazima tupigwe
maswali?
Edmond :( anacheka
kidogo) hapana unajua Kama wiki na nusu ulikuwa hata hauko vizuri ulikuwa
kama umepoteza kumbukumbu kama vile akili yako imerudi nyuma miaka miwili
Raymond: unaniambia kweli au unanitania
Edmond: kweli…
Raymond :( anaguna)
nilikuwa namtesa Angelina?
Edmond: cha kushangaza hapana hata hukumtesa na
Zaidi tu ulimpenda tu yaani mpaka tukawa tunashangaa
Raymond :( anatabasamu)
Edmond sijawahi kupenda mwanamke Kama navyompenda Angelina, yaani dah!!
Edmond: hiyo imejidhihirisha Kwa hizi siku kadhaa
ulizokuwa umepoteza kumbukumbu…aliyekutengeneza alijua utarudi miaka miwili nyuma
na kurudisha mapenzi yako
Raymond: wewe unahisi ni nani? Mimi nahisi ni Christina…ingawa
sina uhakika sana
Edmond: wote hatuna uhakika
Raymond: nimewatesa ee
Edmond: kiasi maana msala wenyewe hata sio wa siku
nyingi…sana kwahiyo poa tu…anyway welcome back brother
Raymond: thank you ingawa mwenzenu sikuwa hata na
wazo
Edmond: nguvu za Giza hizo…
Raymond: sasa mama si atakuwa alikuwa anahangaika
Sana
Edmond :( anaguna)
sijajua ingawa Nina uhakika lazima atakuwa alikuwa anahangaika ndio ukizingatia
wewe ni mwanae wa pekee lazima ahangaike
Raymond: Angelina je?
Edmond :( anacheka
kidogo) yaani wewe na Angelina tu…alikonda
Raymond: ananipenda ee (anatabasamu)
Edmond: anakupenda ndio
Raymond: nafurahi Sana…poa tuonane jioni tuweke
mipango vizuri ya harusi yenu au sio
Edmond: poa mwanangu…Asante umerudi mwana…
Raymond: usijali pamoja Sana
(Wanakata simu)
Glory :( anaingia
ofisi akiwa amebeba kikombe cha chai na chupa ya chai)
Raymond: we nae mi mpaka njaa imeisha loh…ulikuwa
unanunua? Au ulikuwa unachemshia mshumaa…khaa
Glory :( anacheka) hamna bwana mambo mengi huko
jikoni acha tu mwanagu
Raymond: haya mimina mambo hayo
(Anammiminia chai kwenye kikombe,
anamkaribisha kisha anatoka, Raymond anaendelea kunywa chai huku anaangalia
mwenendo wa kazi ulivyokuwa siku zote ambapo hakuwepo)
0 Comments