IAM IN LOVE WITH MY HOUSEGIRL 1

 

SCENE 1: -

(Ni jioni  tulivu sana,upepo mwanana toka bahari ya hindi unapuliza kwa mbali na hali kwa ujumla inaonekana nzuri,kundi la watu limekusanyika sehemu moja na kwa ajili ya  kusherekea jambo fulani .Mbele ya watu hao yaani jukwaani amesimama Mr.Bembele mfanyabiashara mkubwa na tajiri mkubwa jijini hapo,uso wake unaonekana una furaha sana na pembeni yake amesimama mtoto wake wa pekee wa kiume aitwae Raymond,Kijana Raymond ni kijana mtanashati , mrefu na rangi yake ni maji ya kunde  ametoka  kuhitimu elimu yake ya chuo kikuu nchini India,na mkusanyiko ule wa watu ulikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kwa hatua ile nzuri aliyoipiga )

Mr. Bembele :( anakohoa kidogo) Jamani habarini za jioni mabibi na mabwana…

Watu :( wanaitikia)

Mr.Bembele: leo ni siku  ya furaha sana kwangu ,na ninawashukuru wote mlioungana nami pamoja na mwanangu wa pekee Raymond katika siku hii (ananyamaza kidogo)mbali na mwanangu aliyefanikisha sherehe na mipango yote ni mke wangu mpendwa Mrs.Gloria Bembele(kwa mkewe) tafadhali pita mbele uwasalimie wageni wote waalikwa waliofika hapa kuungana nasi leo katika siku hii muhimu ya kumpongeza mtoto wetu wa pekee aliyetupa heshima kwa kufanikiwa kuhitimu shahada yake ya udaktari nchini India,tafadhali mke wangu pita mbele

Mrs.Bembele :( akiwa mwenye furaha na tabasamu zuri likiwa limetanda usoni mwake anapita mbele huku akiwa anawapungia watu mikono, baada ya hatua chache anafika alipo mumewe pamoja na mtoto wake anachukua kipaza sauti kutoka kwa mumewe) nashukuru. Sana kwa nafasi hii, sio siri Nina furaha sana yaani hata sijui nielezee vipi furaha hii...

Watu :( wanacheka)

Mrs.Bembele :( huku anamuangalia mwanae) baba yangu mzazi maana nilikupa jina la baba yangu...hongera sana mwanangu Mungu akulinde na kuendelea kukuheshimisha siku zote za maisha yako…baba hongera kwa kuwa daktari, nakusihi uwe daktari mzuri mwenye upendo na mwenye kuwajali wagonjwa maskini na matajiri, uweke utu mbele baba kuliko pesa (anawageukia watu kisha anatabasamu tena) nawapenda sana...na asanteni kwa kuja

Watu :( Kwa pamoja) tunakupenda pia… (Wanapiga makofi)

Mrs.Bembele :( Kwa mwanae tena) nakupenda Sana baba yangu…

Raymond :( anamkumbatia) nami nakupenda Sana mama yangu…namuomba mungu aniongoze nikayashike Yale uliyoniambia…nakupenda sana mama yangu

Mr. Bembele (anajikoholesha kidogo) naona Mimi sina nafasi tena eti eeh maana ni mama na mtoto...Nipeni a Mimi hayo maupendo jamani (anaguna)

Watu (wakiwemo Raymond Na mama yake wanaangua kicheko)

Mr. Bembele: natania najua mnanipenda sana tu sisi ni familia moja… (kwa watu) basi sawa mke wangu ameongea mengi sana hapa na mimi sina cha kuongezea zaidi ni kwamba nakupenda sana pia mwanangu na nina zawadi zako maana umejua kunifurahisha mwanangu... (Anamuita meneja wake) meneja tafadhali nilete hizo nyaraka pamoja na funguo

Watu: wow!!!

Mr. Bembele: eti wow! Nyie watu wambea jamani (anacheka)

Meneja :( anakuja akiwa ameshikilia hivyo alivyoagizwa na mara baada ya kumfikia Mr. Bembele anamkabidhi)

Mr. Bembele: basi sawa mpendwa (anavipokea vitu vile) Asante tafadhali rudi ukaketi

Meneja :( anarudi alipokuwa ameketi)

Mr. Bembele:(kwa Raymond) kwanza kabisa mwanangu nakupongeza kwa kuwa mtoto mwenye nidhamu kwa watu baki na hata sisi wazazi wako, pia baba ninakupongeza kwa kuhitimu vyema elimu yako na hatimae umekuwa daktari, (anatulia kidogo huku anamuangalia mwanae usoni) kitu cha kwanza mwanangu nakupa kazi…kwenye hospitali yangu mwenyewe, wewe si unajua ile ni hospitali yangu na si yako? Inakupasa sasa utafute na wewe hospitali yako…nakufungulia kwa kukupa kazi sasa akili kichwani mwako

Raymond :( anatabasamu) Asante baba

Mr. Bembele: utakuwa ndo boss pale…

Watu :( wanapiga makofi) wow…

Raymond: Asante dad...Asante Sana

Mr. Bembele: sambamba na kazi hiyo nzuri lazima boss aishi nyumba nzuri…kwahiyo nakupa nyumba mpya yenye kila kitu ndani…kama zawadi na ina jina lako na hakuna mtu atakae kusumbua hata hapo baadae (anamkabidhi bahasha iliyokuwa na hati ya nyumba) hii nyumba ni yako sasa ni zawadi yetu kwako

Raymond: Oh My God!!Dad…this is too much…Asante dad…really nakushukuru Sana my dear dad… (Anaipokea)

Mr. Bembele :( anacheka) bado kuna zawadi nyingine…ningependa kukuzawadia…unajua ukiwa boss bwana ni lazima utumie vitu vizuri otherwise watu watajuaje kuwa wewe ni boss? Nakuzawadia gari Kwa ajili ya kazi zako na matembezi pia

Raymond: Oh...No Dad vitu vingine si ungeacha tu dad…this is too much... (Anataka kulia)

Watu: aaaaawh!!!

Mr. Bembele: (anacheka kidogo) no…usilie mtoto wangu…bado Nina zawadi yako nyingine tena najua hii utaipenda kuliko zote

Raymond: nyingine dad?

Mr. Bembele: ndio dear leo ni mwendo wa zawadi (anageukia kwa watu kisha anamiita binti mmoja) Christina…tafadhali njoo mbele hapa, kuna jambo nataka kuzungumza leo mbele za watu

Christina :( msichana Mrembo kwa muonekano wake harakaharaka ni mwanadada mwenye Maisha ya hali ya juu. anaenda mbele Kama alivyoelekezwa, na baada ya hatua Kadhaa anamfikia Mr. Bembele aliyekuwa amesimama mbele yeye na familia yake)

Mr. Bembele: Christina mama...

Christina: (Kwa heshima Sana) abee baba yangu

Mr. Bembele:(kwa watu) jamani mabibi na mabwana Christina na Raymond ni wapenzi wa muda Mrefu sana sasa hivi wanaweza wakawa wamefikisha miaka hata kumi kwenye mahusiano yao au nadanganya (anawageukia Raymond na Christina)

Raymond: Ni sita tu dad… (Anacheka kidogo)

Mr. Bembele: hiyo baba sio michache… (Anawaangalia watu) nawatangazia kuwa baada ya miezi miwili Christina na Raymond watafunga ndoa…na gharama zote za ndoa na kila kitu nitagharamia mimi (anatabasamu)

Watu :( wanashangilia na waliopiga vigelegele nao walikuwepo)

Raymond :( anaonekana hana raha na ile habari kwani ghafla tu uso wake uliokuwa na tabasamu unazima, na tabasamu linapotea) lakini dad…

Mr. Bembele: hakuna cha lakini hapa ushakuwa mkubwa Raymond ni muda muafaka sasa unatakiwa kuoa na kila kitu nitagharamikia mimi… (Anawageukia watu)

Mrs.Bembele :( anamsogeza Raymond pembeni) nini tatizo mpendwa wangu? Nakuona umekosa raha ghafla kuna shida gani baba?

Raymond: hamna kitu mama nipo sawa (analazimisha tabasamu)

Mrs.Bembele: unanificha hata Mimi mama yako Raymond mtoto wangu

Raymond: hapana mama kweli...Hakuna kinachonisumbua, labda nimechoka

Mr. Bembele :( Kwa mke na mtoto wake) kuna nini mbona sisi tunasherekea nyie mnanong’onezana?

Raymond: tusamehe baba…

Mr. Bembele :( anacheka) nambie Raymond baba umeipenda zawadi gani kati ya hizi nilizokupa?

Raymond :( bado anaonekana hana furaha) zote nzuri dad…Asante sana baba yangu nakuahidi nitakuwa daktari mzuri na kama mama alivyoniambia nitahakikisha kila mtu anapata huduma nzuri awe mkubwa au mdogo, tajiri au fukara wote kwangu watakuwa sawa…Mungu anisaidie

Watu :( wanapiga makofi)

Christina :( anamtabasamia Raymond)

Raymond :( anatabasamu pia lakini si kwa furaha)

Mr. Bembele :( ananyanyua glasi) to my son…cheers

Watu :( wananyanyua glasi pia) cheers!!!

(Muziki unawashwa na kila mtua anaonekana ana furaha, watu wanaselebuka, wanakunywa na kula watakavyo, sherehe imefana kweli na hakuna hata mmoja anaeonekana hana raha isipokuwa mwenye sherehe, wakati watu wanaendelea kufurahia mama Raymond, anagundua mwanae hana raha anamfuata)

Mrs.Bembele :( anamfikia) hauko kawaida tangu baba yako alipotangaza kuwa unatakiwa kufunga ndoa…baba ni nini tatizo mwanangu jamani tafadhali niambie mimi na wewe mbona hatufichani kitu?

Raymond :( kimya kidogo huku ameangalia chini kisha anamuangalia mama yake) mama…

Mrs.Bembele: abee mwanangu

Raymond: kwanini dad hakuniuliza Kama nataka kuoa sasa au lah?

Mrs.Bembele: mwanangu, baba yako amefanya tu ku assume kwamba pengine utafurahi sana akitangaza kuwa wewe na mpenzi wako wa miaka mingi mtafunga ndoa, yeye kwake hiyo imekuwa tu kama zawadi na si vinginevyo tafadhali usigombane na baba yako muache tu na fanya asemalo maana…yeye ndo baba yako sa unadhani utafanyaje, (anacheka kidogo) yaani wewe mimi nikajua sijui umefanya nini kumbe kisa hujaambiwa kuwa leo ndoa yako itakuwa inatangazwa…. mtoto una madeko wewe loh (anamfinya sikio)

Raymond :( anacheka) mama unaniumiza bwana

Mrs.Bembele: muone macho yake (anacheka)

Raymond :( anatabasamu)

Mrs.Bembele: usikasirike bwana haya mambo madogo Sana…hili sio tatizo kabisa au hutaki kuoa?

Raymond: sio hivyo mama

Mrs.Bembele: sasa baba hilo sio tatizo kabisa mwanangu

Raymond: najua (anakaa kimya kidogo) hilo sio tatizo mama, tatizo ni kwamba…

Christina :( anakuja ghafla) Raymond honey… (Anambusu mdomoni)

Raymond :( Kwa ukali) kuwa na adabu we huoni mama yupo hapa?

Christina: mambo ya kizungu baby jamani wewe si umekaa uzunguni…?

Raymond :( anamkatisha) sikuwa uzunguni nilikuwa uhindini…na nimejifunza heshima

Mrs.Bembele: ongeeni taratibu tupo kwenye kadamnasi ya watu, watu ni wengi sana acheni balaa nyie watoto, Christina nenda nyumbani maana umelewa sana, Raymond nenda kwa watu huko hii sherehe ni yako

Christina :( huku anaondoka) aaah!!!Wazee wengine bwana

Raymond: we Christina unasema?

Christina: naenda nyumbani

Raymond: yaani huyu mwanamke… (Anatikisa kichwa kisha anaenda walipo watu wengine)

Mrs.Bembele:sasa nimeelewa kwanini Raymond alichukia mara  baada ya kutangazwa kuwa anatakiwa afunge ndoa na mpenzi wake kumbe wana shida kati yao hawaendani na pia hawaelewani yaani ni kama mzungu na mchina wakiwekwa sehemu moja ni lazima hawatafurahia uwepo wa kila mmoja wao hapo…Christina na Raymond ni wapenzi wa miaka mingi lakini hawaelewani sasa watakuwaje wanandoa kwa hali hii?maskini mwanangu amejiingiza sehemu ambayo yeye mwenyewe hajui atatoka vipi(anatikisa kichwa kisha anaelekea walipo wengine)

Mr. Bembele :( anamjia mkewe) oh my wife…ulikuwa wapi embu tufurahie mtoto wetu kamaliza masomo yake na kesho au kesho kutwa anaanza kazi na baada ya miezi miwili atafunga ndoa… (Anakunywa kinywaji chake)

Mrs.Bembele:ni kweli mume wangu embu tufurahie (anaendelea kufurahia sherehe ile)

Post a Comment

1 Comments

  1. Hello my people don't forget to visit this blog everyday for more and more stories

    ReplyDelete