SCENE 2: -
( Asubuhi
nyingine tena tulivu jua kwa mbali jua limeanza kuchomoza kila mtu maeneo yale
anaonekana anafanya mambo yake na hakuna hata mmoja mwenye muda na mwenzie,Raymond
na rafiki yake wa karibu wanaingia katika mjengo mmoja wa kifahari naposema wa
kifahari niamini ni wa kifahari kweli,geti tu ni la kufunga na kufungua kwa
rimoti,mara baada ya kuingia kwenye mjengo huo wa kifahari ambao kwa sasa ni
mali halali ya Mr.Raymond Bembele…mtoto wa kwanza na wa mwisho wa tajiri Bembele
na mkewe.Raymond na rafiki yake wanashuka kwenye gari ambalo pia ni zawadi ya Raymond
kutoka kwa wazazi wake)
Edmond :(
rafiki kipenzi wa Raymond) eh! Bwana dah!!Bonge la mjengo...dah! Mond...
Raymond :( huku
anacheka) nambie Mond...
Edmond: huu mjengo mwanangu bonge la kitu haki ya Mungu
tena sikudanganyi, hii nyumba mwanangu ni fireeeee
Raymond :(
anatabasamu) au sio… (Anacheka tena)
Edmond: ndo maana yake…dah!!Mpaka nakutamania
mwanangu dah!!Yaani na mimi ningekuwa na wazazi dah!!
Raymond: usiseme hivyo Mond kazi ya Mungu haina
makosa yeye akipanga hakuna wa kupangua cha msingi ni kuwaombea tu wazazi waendelee
kupumzika kwa amani
Edmond: ofcourse, sema nini Mond…wewe ni Zaidi ya
ndugu yangu mwanangu mi nilijua kuwa ukishapanda cheo na mimi utanisahau na
uwalimu wangu lakini dah!!Umenikumbuka my brother hata kwenye sherehe yako
nilikuwepo…dah na leo umekuja kufungua nyumba yako kwa mara ya kwanza umeniita
kweli wewe ni Zaidi ya ndugu
Raymond: usijali Mond…tupo pamoja msela wangu...na
tutazidi kuwa pamoja
Edmond: Asante Sana rafiki yangu (anaendelea kushangaa jumba lile la kifahari)
Raymond :( anamshika
begani) poa tuingie ndani
Edmond: dah!!Huko ndani sipapatii picha mwanangu
Raymond :(
anacheka) ndo ngoja tupacheki maana hata Mimi sijapaona mwanangu (anafungua mlango)
(Kwa pamoja wanaingia ndani)
Edmond: Oh My God!!...hii ni nyumba au paradise
niambie tu mapema matendo yangu mazuri yamenileta hapa...aisee nimefika
mbinguni mwenzenu
Raymond: acha zako Mond…hapa sio mbinguni ni
nyumbani kwangu…ghetto langu
Edmond: getto???!!!Hili mbona jumba hili mwenzangu...
Raymond; mi bado bachela…sina mke
Edmond: utakuwa nae hivi karibuni mzee wako Jana
katutangazia kuwa utakuwa mume wa mtu baada ya miezi kadhaa…najua umefurahi
sana maana sio kwa kumpenda Christina huko (anamuangalia
usoni) si umefurahi eeh!!!
Raymond: Edmond we ni mshikaji wangu wa miaka na
wewe unaelewa fika kuwa mimi sitaki kuoa sasa hivi na unaelewa kabisa jamu
zangu na huyu demu leo hii unaniuliza kama nina furaha ya kuwa mume wa Christina,
kweli hilo swali unaliona liko sawa kweli?
Edmond: nisamehe Raymond mi nilikuwa nakutania tu
mtu wangu nisamehe Sana kaka yaishe
Raymond: usijali my brother Mimi na wewe hatuwezi kuzinguana
Edmond: ndo maana yake ila embu nambie kitu hapa
nielewe kwanini usimsamehe tu Christina na umuoe tu...
Raymond; kumsamehe nilishamsamehe lakini sioni kama
anaweza kuwa mke wangu ni kweli nilikuwa nampenda lakini kwa kitendo
alichonifanyia…mimi nilimheshimu ila yeye akanifanyia vile alivyofanya na hapo
ni mpenzi akiwa mchumba je au mke si ataniua…christina sio mwanamke nayemtaka
yaani she is not for me kabisa tutapotezeana muda tu ila ukweli ni kwamba kama
mama alivyosema kwa kuwa dad…ndo kaamua basi ni kuwa mpole tu sina jinsi
Edmond :(
anaguna) ila mwanamke mshenzi
Raymond: sio kidogo nakwambia
Edmond :(
anabadilisha mada) nionyeshe vyumba…
Raymond:(anacheka)
umeanza… (anacheka tena) mimi
mwenyewe sipajui kabisa hapa nababia tu (anafungua chumba kimoja) wow...
Edmond: chumba chumba jamani chumba kweli ndugu
yangu
Raymond: hiki sijui ni chumba changu
Edmond: embu endelea kufunga na kufungua vyumba
tutakipata tu cha kwako
Raymond :(
anaendelea kufungua na kufunga vyumba na hatimaye anakipata chumba chake)
wow…sasa hiki ndo chumba changu…Mond cheki kitanda hicho
Edmond: mdogo wangu oa baba hichi kitanda utakuwa
unalala peke yako? Oa haraka Sana
Raymond: huyo mwanamke wa kuoa sasa bado sijamuona
kabisa hata nisemeje sijampata kabisa
Edmond :(
anacheka Sana) yaani wewe huna aibu kabisa yaani wazazi wako wamekuchagulia
mke unakataa sasa utakaa Na nani kwenye jumba lote hili?
Raymond: hata na wewe unaonaje hiyo
Edmond: Mimi natarajia kuoa hapa nakusanya tu
mahari tu…
Raymond: nitakusaidia kaka yangu we siku ukitaka
kwenda Kwa kina Catherine basi niambie nitakuwa hapa kuusaidia my brother
Edmond: ah…Raymond my brother ushanisaidia Sana tu
acha hili nikomae nalo kibishi tu mtu wangu
Raymond: let me help you my friend (anamshika bega ishara ya kumsihi Sana)
Edmond: sina ubishi sawa…haina shida nisaidie tu
ila unanilemaza
Raymond: utakoma (anacheka)
(Mlango unagongwa)
Raymond: pita mlango uko wazi
Edmond: utakaribisha na majambazi my brother
Raymond: majambazi asubuhi yote hii?
(Kuna mtu anaingia ndani kwakuwa hawamfahamu wanamuangalia tu)
Mtu: habari zenu jamani
Kwa pamoja: salama...
Mtu: Mimi ninaitwa Ramadhani nimeagizwa hapa na Mr.
Bembele
Raymond: sawa huyo ni baba yangu, ndio amekuagiza nini?
Ramadhani: Mimi ndio mlinzi wako na mali zako zote
humu ndani, ila mimi nitakuwa nakaa pale getini
Raymond: oh…karibu sana kaka Ramadhani…mimi naitwa Dk.
Raymond Bembele ni mtoto wa pekee wa bwana na bibi Bembele nashukuru sana kwa
ujio wako maana nilikuwa nawaza sana ningepata wapi mlinzi sasa hivi ila kweli
Mungu anaishi na amenisaidia kwahiyo karibu sana (anamgeukia Edmond) huyu ni rafiki yangu kipenzi yaani keshakuwa
kama ndugu, anaitwa Edmond...
Ramadhani: eeh!!Raymond, Edmond…hizo Mond mwishoni
mmezigundua? Au hamjazindua?
Edmond: zamani Sana
(Wanacheka)
Raymond: aisee karibu Sana Mr. Ramadhani
Ramadhani: asanteni Sana kina Mond (anacheka KISHA anaondoka)
Edmond: mshikaji anaonekana yuko vizuri Sana,
mcheshi, nimemfurahia…ukiwa mpweke nenda getini ukachekeshwe
Raymond: umeona eeh…yaani napenda watu wa hivi
nafurahi sana kukaa nao
Edmond :(
anabadilisha mada) aisee Nina njaa kweli hakuna jiko
Raymond: we mwehu kweli yaani ushawahi kuona nyumba
haina jiko sema hakuna chakula Kama una njaa Nina njaa Zaidi yako mtu wangu cha
kufanya tukale nje mtaani huko maana hapa Mimi hiyo nguvu ya kuingia jikoni
mara sokoni kwasasa sina kabisa, kwahiyo twende zetu magengeni
Edmond: poa mi nakusikiliza wewe boss
Raymond: nishakwambia usiwe unaniita boss sipendi
hilo jina kweli yaani
Edmond: nisamehe mdogo wangu sikuiti tena (anamkumbatia)
Raymond :(
anamsukuma) embu twende huko
Edmond :( anamuachia) haya twende
(Wanaondoka
kuelekea nje wanapanda gari na kuondoka zao)
0 Comments