SCENE 3: -
(Asubuhi ya
siku ya pili yake ambao pia ni asubuhi ya kwanza ya Raymond nyumbani kwake mara
baada ya kukabidhiwa nyumba na wazazi wake. Raymond kalala fofofo huku simu
yake ya mkononi aina ya iphone 13 pro max ikiwa inaita mfululuzo bila
kupokelewa, inaita sana kitendo kinachomfanya Raymond kushtuka kutoka
usingizini, anaitazama simu yake na anagundua kuwa imeita sana na simu zote
zimetoka kwa baba yake)
Raymond; oh My God…missed calls ishirini na tano? (Anashangaa Sana) halafu zote za
dad…Mungu wangu, ngoja nimpigie (anapiga)
(Simu inaita)
Mr. Bembele: (anapokea) wewe mtoto wa Gloria
unalala sana baba, kwanini lakini?
Raymond: iam sorry dad…
Mr. Bembele: nakupa dakika 10 uwe umefika ofisini
wafanyakazi wako wanakusubiri boss wao ufike haufiki naomba uvae haraka uje
nakusubiri
Raymond:(huku
anashuka kitandani) ok dad… (anaingia
bafuni anaoga haraka kuliko kawaida baada ya muda anatoka haraka anavaa nguo
zake za ofisini KISHA anachukua ufunguo wa gari anatoka nje, anapanda gari lake
na kuliondoka kwa mwendo wa kasi sana, baada ya kama dakika kumi na tano
anafika ofisini kwake ambapo kwa sasa yeye ndo bosi)
Mr. Bembele :( anamuona
kwa mbali, anawageukia wafanya kazi ambao walikuwa wamesimama wakimsubiri kwa hamu boss huyo mpya)
jamani anakuja
Raymond :(
anaingia ofisini)
Wafanyakazi :( wanamwagia
Maua wenye kumtupia Maputo nao wapo) welcome boss…
Raymond :(
anatabasamu) jamani asanteni Sana jamani
Mr. Bembele: karibu Sana…boss
Raymond: Asante…
Mwanamke 1 :(
Kwa sauti ya chini) dah!!!Boss handsome huyu jamani
Mwanamke 2: yaani acha tu da. Pendo…yaani mwanamume
mzuri huyu cheki tabasamu duh...
Pendo: wewe Rachel naomba umheshimu huyu ni shemeji
yako
Rachel ;(
anacheka) yamekuwa hayo?
Pendo: twende tukamshike hata mkono mwenzangu
Raymond :(
anatabasamu huku anaendelea kushika watu wote mikono) asanteni jamani
Pendo: jamani kaka umependeza
Raymond: Asante dada
Mr. Bembele :( anamshika
mwanae mkono) boss…naomba sasa uje ofisini kwako tumalize hili zoezi
Raymond: ok dad…
(Mr. Bembele
na mwanae wanaelekea ofisi iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya Raymond, wanapofika
ofisini humo Raymond anavutiwa sana na uzuri wa ofisi ile)
Raymond: wow dad, this ofisi is so beautiful
Mr. Bembele: ya kwako mwanangu nimeiweka kwa ajili
yako…wewe ndo boss from now on wards mpaka uzeeke na nina Imani utaipeleka
mbele hospitali yetu mwanangu
Raymond: haswa…
Mr. Bembele :( anamuwashia
runinga kubwa iliyokuwa imebandikwa ukutani mara baada ya kufanya hivyo
anamuwashia laptop KISHA anamvutia kiti) tafadhali keti boss…nakukabidhi
rasmi ofisi yako
Raymond: oh...Dad…Asante Sana mzee wangu
Mr. Bembele: usijali mwanangu...Please enjoy sasa
acha Mimi niende…nikapumzike nyumbani
Raymond: ok dad…Asante dad, ofisi nzuri Sana…nimependa
samani zote zilizopo humu ni nzuri sana
Mr. Bembele: usijali tupo pamoja mwanangu (anatoka na kwenda zake nyumbani)
Raymond; oh…my God…am I in heaven? mbona ofisi
nzuri hivi? (anatabasamu mwenyewe) nakushukuru Mungu wangu kwa
Baraka hii ya wazazi wanaonipenda kiasi hiki…ingawa huwa tunagombana gombana
sana na dad…hiyo ni kawaida maana hakuna aliye mkamilifu ila wewe tu Mungu
wangu…asante sana (anachukua simu yake
anampigia Edmond)
(Simu inaita mwisho inapokelewa)
Raymond: Yes, Mond...Guess what?
Edmond: what?
Raymond: nipo kwenye ofisi yangu mpya rafiki yangu
nakula kiyoyozi tu…
Edmond; wacha we…kula bata baba mpaka kuku waone
wivu
Raymond :( anacheka
Sana) yaani acha tu, sifa na utukufu tumrudishie yeye aliyeziumba mbingu na
dunia na Zaidi alinipa wazazi wanaonipenda kama hawa
Edmond: haswaaaa….
Raymond: ngoja nikutumie whatsApp picha ya ofisi
yangu mpya upaone
Edmond: poa Mond
Raymond :( anajipiga
picha anapiga ofisi yake KISHA anamtumia picha rafiki yake) nishakutumia
Mond
Edmond: poa… (Anaingia
whatsApp anaangalia KISHA anampigia simu tena)
Raymond: nambie
Edmond: mwanangu bonge la ofisi duh…
Raymond; kidogo Sana tu…
Edmond: kidogo hiyo, ukubwa Kama chumba na sebule
yangu
Raymond: umeanza Mond si unajua huwa sipendi
unavyoyaangea hayo maneno usiwe unasema hivyo
Edmond: hiyo ndo reality ya maisha yangu, ila poa
basi haina noma wangu tuyaache hayo
Raymond; poa
Edmond: poa ngoja naingia kipindi sasa hivi kwahiyo
nazima simu tuonane baadae Kama kwenye saa kumi na moja hivi tubadilishane
mawazo, mdogo wangu
Raymond: hamna noma kaka yangu ngoja nianze
majukumu ya siku huku
Edmond: poapoa
Raymond :( anakata
simu) Ah…Nina Amani Sana jamani sasa nina kazi ya kutafuta true love
Christina sio true love wangu (simu yake
inaita haraka anapokea) nambie
Sauti: poa…honey hujanimisi.
Raymond: dah!! Christina nipo ofisini hapa nina
kazi sana mtu wangu…ungeniacha kidogo tutaongea badae
Christina: yaani siku hizi sikuelewi kabisa my love
yaani tangu siku ile imetangazwa kuwa tutafunga ndoa baada ya miezi miwili
nakuona kabisa huna raha na mimi kabisa kwanini?
Raymond: huo ni wasiwasi wako tu Tina mi mbona sina
chochote anyway Kama nilivyokuambia nina kazi tafadhali tuonane baadae kidogo
Christina: ila tambua kuwa ninakupenda sana mchumba
wangu na ninamuomba Mungu atufikishe tunapopataka
Raymond; poa (Anakata
simu) yaani huyu mwanamke yaani hana kabisa sifa za kuwa mke wangu ingawa
nimekaa nae huu mwaka wa sita ila nafsi yangu tu haimkubali tena mara baada ya
kujua kuwa ni mzinzi na msaliti ndo kabisa sitaki hata kumsikia ila sasa
unadhani nitafanyaje ndo tayari baba keshamchagua inabidi tu niwe mpole nitulize
tu kipapa (anasogeza laptop yake karibu
anaanza kufanya kazi) Mungu tu anaisaidie
Sekretari (anabisha
hodi) habari za kazi boss, Mimi naitwa Glory ni sekretari wako samahani
sikuwepo kukupokea maana kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi
Raymond: usijali Glory wajina wa mama yangu…tupo
pamoja mi naitwa Raymond Bembele
Glory: nashukuru kukufahamu boss (anacheka kidogo)
sawa boss karibu sana ofisini kwetu
Raymond :( anaachia tabasamu zuri) Asante mami
Glory
:( anatoka huku akimuacha Raymond
anaendeleea na kazi zake)
Raymond
:( anaonekana ni mtu mwenye furaha kila
mara anaiangalia ofisi yake na anaifurahia sana)
1 Comments
Inaendelea baadae kidogo
ReplyDelete