I KILLED MY LOVER 46

 


SCENE 46: -

USIKU HUOHUO:

NYUMBANI KWA BIANCA: -

(Liliana anafika nyumbani akiwa ameambatana na binamu zake, wanapofika wanapigwa na butwaa kuona nyumba yao imeteketea kwa moto, anahisi miguu inaishiwa nguvu)

Anna: (anamshika bega) mdogo wangu jikaze

Lupemba: (anakuja anamkumbatia Liliana)

Liliana: (anatoka machozi) mama yangu yuko wapi?

Lupemba: Liliana… (Analia)

Liliana: nini?

Bella: (Analia)

Lupemba: kila mtu

Liliana: nini? (anaanza kuchanganyikiwa)

Lupemba: amekufa…wamefariki

Liliana: (anapiga kelele) maaaaaammaaaaaaaaaa…uwiiiiiiiiii (anaweka mikono kichwani)

Jirani: maskini huyu mtoto

Liliana: mama yangu mimi… (machozi yanamtoka)

Anna: (Analia sana) babaaaaaaa

Bella: baabaaaaaaaa

Lupemba: (Analia sana)

Liliana: (anachanganyikiwa)

Polisi: tunaomba utulivu…miili haipo yaani ni majivu moto ulikuwa mkali sana

Liliana: (Analia sana)

Polisi: (kwa Lupemba) wewe ndo shahidi tunaomba kama hautajali twende wote kituoni

Lupemba: sawa

Liliana: (kwa hasira) Lupemba

Lupemba: naam…

Liliana: njoo

Lupemba: (anarudi alipo Liliana)

Liliana: nani ameunguza nyumba ya mama yangu na kumuulia mama yangu ndani?

Lupemba: Liliana tulia kwanza

Liliana: (kwa hasira) nani?

Lupemba: Robert

Liliana: (anapiga magoti) Robert… (anapiga chini kwa hasira) lazima ufe sitasubiri sheria mimi nitakuua kwa mikono yangu miwili Robert I swear you will pay dearly…I swear... (kwa Lupemba) usihangaike kwenda wapi wala wapi hii shoo niachie mimi nitaisimamia

Polisi: binti acha sheria ichukue mkondo

Liliana: sina muda wa kusubiri sheria… (anaanza kulia tena) mama yangu amekufa mwezi mmoja kabla ya ndoa yake mama yangu alikuwa ana furaha sana leo hii amekufa mama yangu mimi na mnaniambia nisubiri sheria? Siwezi

Lupemba: punguza hasira Liliana

Liliana: hasira zangu zitaisha pale nitakapomuua Robert…lazima afe I swear lazima afee

Anna: (Analia sana)

Bella: (Analia)

Liliana: msijali dada zangu huyu Robert kwangu mchache sana nitamuonyesha joto ya jiwe mjinga sana huyu baba

Polisi: (anaona aondoke zake)

Lupemba: nipo na wewe Husna amefia humo…kipenzi changu amefia humo…siwezi kumsamehe Robert halafu baada ya kuchoma nyumba akaondoka kwa madaha na dharau hata hakujutia

Liliana: ninaenda kumuona

Anna: huwezi kwenda ukiwa na hali hii

Liliana: hii hali ndo nzuri sasa nikienda nimepoa sitamuonyesha upande wangu wa pili (anapanda gari na kuliondoa)

Bella: Liliana

Liliana: (analiondoa kwa fujo sana, baada ya mwendo wa muda kidogo anafika katika jumba safi na la kifahari la Robert) nimefika sijui ataniambia nini mimi… (anashuka na moja kwa moja anaingia ndani)

Robert: (anamuona anacheka kwa dharau) nilijua tu utakuja…una ujasiri…vipi kafa au kaokoka kwenye ule moto?

Liliana: wewe ni mpumbavu tena mpumbavu mkubwa

Robert: I don’t care…Bianca kama hakuwa wangu ni bora nilivyomuua kuliko kumuona na mwanaume mwingine hiyo ni adhabu yake kwa kunikataa mimi...kwani mimi nina kasoro gani kwani hukumwambia uzuri wangu?

Liliana: nitakuua Robert… I swear to you nitakumaliza kama ulivyomuua mama yangu na mimi nitakuua Robert

Robert: (anacheka kwa kejeli) maskini anaota ndoto za saa nne usiku...huwezi hata kunisogelea sasa hivi unaongelea kuniua?

Liliana: wanaume mna roho mbaya sana

Robert: sana…hata Mungu alijua ndo maana hakutupa jukumu la kubeba mimba maana kama tungebeba hao watoto wasingekuwa wanafikisha miezi tisa ingekuwa wanatusumbua kidogo tunawaua… (anamalizia na kicheko cha dharau)

Liliana: I will kill you…

Robert: rubbish (anacheka kwa kejeli)

Liliana: you killed my mama… I will kill you

Robert: whatever…I don’t care

Liliana: mwezi mmoja baadae tarehe kama leo nitakuua Robert

Robert: (anacheka kwa dharau) huniwezi halafu kwa taarifa yako nimeona nimuue Bianca ili nafsi yangu iridhike…nilimpenda sana Bianca nilikuwa tayari kumuacha mama Gabriel ili nimuoe Bianca lakini kila mara nikimuangalia alikuwa hanitaki na pia alikuwa ananichukia sana…nikaona isiwe kesi afe tu

Liliana: nitakuua

Robert: (anacheka) huniwezi Liliana…huniwezi kiserikali huniwezi kichawi wala vyovyote hata ukienda polisi huniwezi Liliana

Liliana: nani amekuambia naenda polisi? Wewe nacheza na wewe mwenyewe umeniulia mwanamke aliyeyapa maisha yangu nafasi ya pili mwanamke pamoja na kujua mimi sio mwanae wa kuzaa alinibeba na kunipenda kwa dhati

Robert: embu toa blah blah zako hapa yaani hata kunisogelea unshindwa unawaza kuniua (anacheka kwa dharau) usinichekeshe bwana

Lilian: time will tell

Robert: mimi nikwambie tu kuwa pole sana kwa msiba ndugu yangu (anacheka kwa dharau)

Liliana: wa kwako unakuja usubiri

Robert: tutaona

Liliana: we will see about that

Robert: okay dogo... (anacheka kwa dharau)

Liliana: (anafura kwa hasira) nitakuua I swear

Robert: huwezi…tupinge na usiponiua nitakuua wewe

Liliana: sawa…nitakuua mwezi mmoja baadae

Robert: in your dreams baby

Liliana: (anatoka kwa hasira)

Robert: eti nitakuua… (anacheka sana) Mtu hata huwezi hata kunisogelea unaanzaje kuniua?

Liliana: (akiwa nje) I will surely kill him…. Nitamuua haki ya Mungu (anaondoka)

Robert: (anaendelea na shughuli zake)

Post a Comment

1 Comments

  1. Usiondoke mdau mpaka uone mwisho WA mkasa huu... Asanteni kwa kuendelea kunisapoti

    ReplyDelete