SCENE 45: -
BAADA YA MWEZI MMOJA: -
NYUMBANI KWA BIANCA: -
(Majira ya saa mbili usiku,
Bianca pamoja na mchumba wake wamekaa sebuleni huku wanaonekana kuwa na
mazungumzo ya kawaida, mkao wao ni wa kimahaba, Bianca amemlalia mjomba
kifuani)
Bianca:
baby mbona huwa unaogopa kuja akiwepo Liliana? na ukija unakuwa ni muoga…(anacheka)
Mjomba:
(anacheka kidogo) nitazoea tu bwana
wala usijali
Bianca:
haya wewe ogopa tu ona sasa hivi umekuja maana nimekuambia yupo kwenye sherehe
ya rafiki yake ukisikia tu gari linaingia mbio unakaa kama mimi ni dada yako
Mjomba:
(anacheka)
(Kuna sauti ya gari linaingia ndani ya geti)
Mbise:
(anachungulia dirishani)
Mjomba:
(kwa Mbise) Mbise Liliana huyo?
Mbise:
hapana sio Liliana ni yule shemeji
Bianca:
Robert?
Mbise:
ndio
Bianca:
(ananyanyuka) anataka nini usiku huu?
Mbise:
sijui
Robert:
(anashuka kwenye gari na moja kwa moja
anauendea mlango)
Bianca:
huyu mwanaume vipi jamani
Robert:
hodi… (anagonga)
Mjomba:
(anafungua)
Robert:
(anaingia)
Bianca:
unafanya nini? Unataka nini Robert…
Robert:
Bianca usiolewe mpenzi
Mbise:
(anaweka mikono mdomoni ishara ya
kushangaa)
Rober:
nakupenda sana Bianca nipe nafasi
Bianca:
(anamsukuma) embu nenda zako
Robert:
kama hautakuwa wangu basi hautakuwa wa mtu yeyote (anatoka nje anaenda moja kwa moja mpaka kwenye gari yake anachukua dumu
la mafuta ya taa na kiberiti na kurudi nayo ndani)
Bianca:
(anamuona) Robert unafanya nini?
Robert:
nakuua Bianca
Mjomba:
(anashangaa) embu acha ujinga ndugu
yangu huu ni utahira
Robert:
sitanii
Bianca:
Robert,
Robert:
nikubalie Bianca I swear sitakuua yaani siwezi tu kukuona unaolewa na mwanaume
mwingine huku mimi nakupenda nikubali mpenzi hii ndoa itakuwa yetu mpenzi...
Bianca:
Robert umelewa embu tulia
Robert:
(anamwaga mafuta) nikubalie mpenzi
Bianca:
wewe ni kichaa
Robert:
(anamaliza kumwaga mafuta) nikubalie
mpenzi ili nisikuue
Bianca:
siwezi Robert… siwezi kukukubalia (kwa
Mbise) kimbia kaombe msaada huyu mjinga atatuulia humu ndani
Mbise:
(anataka kukimbilia nje)
Robert:
(anamrudisha) embu rudi hapa
Bianca:
get out Robert
Robert:
inaonyesha hunitaki kabisa sasa kama ni hivyo nakuua (anawasha kiberiti na kukitupia kwenye mafuta kisha anaondoka anachukua
ufunguo na kufunga kwa nje)
Bianca:
(anapiga kelele) tusaidieni
Lupemba:
(anashtuka na kujaribu kuokoa jahazi)
(moto umezidi nguvu)
Bianca:
(anateketea kwa moto)
Mjomba:
(anateketea kwa moto)
Mbise:
(anateketea)
Lupemba:
(anakimbilia nje kuomba msaada)
(Nyumba inateketea kwa moto)
(Majirani wanajaa)
Lupemba:
(anapiga simu kwa gari zima moto)
(Baada ya muda kidogo zima moto
linafika)
Lupemba: (anapiga simu kwa Liliana) njoo nyumbani sasa hivi kuna tatizo (anakata simu) eh Mungu watu wote
wamekufa… Husna, Siwema Mbise wote wamekufa (anasiktika sana) ni Robert huyo ndo kawaua
0 Comments