SCENE 47: -
BAADA YA MSIBA: -
(Liliana na binamu zake wamekaa
katika nyumba nyingine ya Bianca na kila mmoja anaonekana kuwa na huzuni sana)
Anna:
tumebaki yatima sasa…
Bella:
(Analia) baba na aunt Bianca walikuwa
wanategemea kufunga ndoa walikuwa na furaha sana
Liliana:
nitamuua Robert
Anna:
(anafuta machozi) no mdogo wangu
usifanye hivyo
Liliana:
nilikuwa yatima Mungu akanipa nafasi ya pili niishi kwa kunipa Bianca kama mama
yangu Robert kwasababu ya ujinga wake amekuja kumuua (kwa hasira) I swear I will kill him
Anna:
acha sheria ifate mkondo wake
Liliana:
sheria? Sheria gani unayoongelea wewe Robert ameniambia simuwezi kiserikali
kwahiyo anaweza kuhonga halafu kesi ikazimwa
Anna:
lakini Liliana embu mfikirie mtoto wako tumboni
Liliana:
namfikiria sana sitaki mwanangu aje akutane na baba yake ambae alimuulia bibi
yake
Bella:
Liliana achana na Robert msamehe na uache sheria ichukue hatua zake
Liliana:
katika maisha yangu nimeshasamehe sana mara ya kwanza niliwasamehe wazazi wenu
kwa kuniulia wazazi wangu nikaja nikamsamehe mjomba wangu kwa kunibaka
mfululizo nikaja nikakusamehe wewe Bella na nikaja nikamsamehe Robert kwa
kunibaka utotoni huyohuyo Robert nimemsamehe kwa kuniambukiza HIV kwa hili la
kumuua mama yangu simsamehi lazima nimuadhibu…lazima afe (anaonekana kuwa na hasira sana)
Anna:
(anashusha pumzi) unapanga kufanya
nini?
Liliana:
ni siri yangu
Anna:
be careful vipi polisi waikijua
Liliana:
nipo tayari kutumikia kifungo au hata kunyongwa ila tu niacheni nimuue Robert
Bella:
binamu hatukubaliani na wewe
Liliana:
sijali
Anna:
Liliana
Liliana:
ndo nakwambia sasa sijali kesho nahama naenda kuishi jirani kabisa na Robert
naenda kupanga
Anna:
Liliana mdogo wangu
Liliana:
nimeshaamua sina mjadala kwa hili…nahama hapa maana nikikaa hapa nitakuwa
namkumbuka mam yangu sana sitaishi kwa Amani
Bella:
(anashusha pumzi) basi sawa
(Mlango unagongwa)
Anna:
nani tena? (ananyaanyuka ili kwenda
kuufungua mlango) oh karibuni sana
Liliana:
nani?
Anna:
wafanyakazi wa ofisini kwa marehemu Bianca
Liliana:
(machozi yanamtoka) mama yangu
anaitwa marehemu sasa kisa Robert (analia
sana)
(Wafanyakazi wanaingia)
Mfanyakazi
1: oh, Liliana acha kulia umeshalia sana…kazi ya Mungu haina makosa yeye
alipanga iwe hivyo angeamua aunt apone angepona ila ndo kaamua iwe hivyo
usijali nyamaza kulia
Liliana:
(Analia kwa uchungu uliochanganyika na
hasira) aliyefanya haya atalipa haki ya Mungu naapa
Mfanyakazi
2: (anampigapiga) basi tulia mama
tulia usije kuingia matatizoni
Liliana:
I don’t care ni lazima nifanye kama alivyo fanya kwa mama yangu I swear
Anna:
binamu yangu tulia naomba ukapumzike
Lilian:
nitapumzikia jela
Mfanykazi
3: hali yako hairuhusu uwe na hasira au mawazo, relax Liliana
Liliana:
ndo nasema mwanangu atanisamehe ila ni lazima nimuue huyo baba
Mfanyakazi
1: usiseme hivyo unaongea kwa hasira hujui unachoongea Liliana nakusihi utulie
Liliana:
sitatulia kwa lolote mpaka pale nitakapoona Robert amekufa tena kama alivyokufa
mama yangu (Analia) ni lazima nimuue
Anna:
mdogo wangu
Liliana:
sitaki kusikia kitu
(Wanabaki wanamuangalia kwa
hasira alizo nazo)
Bella:
(anashusha pumzi) najua una hasira
sana binamu naomba upumzike
Liliana:
naona hatusikilizani naomba mniache kila mtu aende kwao nina maandalizi mengi
sana ya kufanya
(Kila mmoja ananyanyuka na kuanza
kuondoka)
Anna:
ukiwa na shida nipigie
Liliana:
(anakaza macho) sawa
(Wanaondoka)
Liliana:
(anabaki peke yake hali ya huzuni na
uchungu inamuandama pale anapomkumbuka mama yake kipenzi) mama nakukumbuka
sana…natamani mjukuu wako azaliwe umuone ila yule mshenzi amekatisha maisha
yako kisa tamaa zake za kimwili nitamuonyesha kuwa mimi ni Liliana and no body
messes with me…nitamuua haki ya Mungu naapa majira kama haya Robert atakufa I
swear lazima afeeee (anakaza macho huku
machozi yanatiririka mfano wa maji kwenye mfereji) nitamuua sitamuacha (anaukumbatia mto huku Analia sana)
0 Comments