I KILLED MY LOVER 5

 


SCENE 5: -

IJUMAA: -

(watu wamekaa mahakamani kwaajili ya kuanza kusikiliza kesi inayomkabili Liliana, mtuhumiwa anawasili akiwa na mapolisi na msoma mashtaka nae anawasili, familia ya bwana Robert nayo inawasili kwa ajili ya kusikiliza mashtaka yanayomkabiri Liliana, baada ya muda kidogo kila mtu kuingia hatimaye anaingia hakimu na kila mtu ananyanyuka ishara ya heshima kwa hakimu. hakimu anapofika kwenye kiti chake anawaruhusu watu kuketi nao wanatii)

Hakimu :(kwa msoma mashtaka) tafadhali endelea

Msoma mashtaka :( anainama kuonesha heshima) Asante mtukufu hakimu…siku ya jumanne tulikutana hapa kusikiliza mashtaka yanayomkabili bibi Liliana Kadoke mkazi wa Mpanda mkoa wa Katavi…tulisikiliza kidogo baade akawa ameugua kidogo na mahakama ikawa imeamua tusikilize tena leo ijumaa baada ya bibi Liliana kupata afadhali… (kwa mwanasheria wa upande wa kina Robert na familia) tafadhali karibu kama una maswali yoyote…

Mwanasheria: naitwa Bw. Bryson Lameck…ni mwanasheria upande wa washtaki… (anamsogelea Liliana) habari yako, dada Liliana

Liliana: salama…

Bryson: unaendeleaje? Maana ulipata mshtuko kidogo na tukakukimbiza hospitali…vipi hali yako leo?

Liliana: naendelea vizuri Sana…asante kwa kuuliza

Bryson: kwahiyo tunaweza kuendelea?

Liliana: ndio…tunaweza

Bryson: sawa (anaenda kuchukua karatasi Fulani katika dawati alilokuwa amekaa kisha anamrudia Liliana) ah…mara ya mwisho ulituambia kuwa ulikuwa na mahusiano na marehemu na alikufanyia mambo mabaya yaliyokusukuma kumuua

Liliana: ilikuwa ni hasira tu…mheshimiwa

Bryson: tunaomba tusikie labda na sisi tutaelewa hiyo hasira…maana kwa sasa hatuelewi kabisa hiyo hasira iliyokufanya kumuua Bw. Robert na kuchoma nyumba yake….

Liliana:ni hadithi ndefu sana

Bryson: tunataka kuisikia

(Familia ya Bw. Robert nao wapo hapo wakisikiliza Kwa umakini yote yanayoendelea hapo)

Liliana: labda nianze Kwa kuhadithia maisha yangu Kwa ujumla ili ilete maana kama nitaruhusiwa

Hakimu: unaruhusiwa…

Liliana: asante mtukufu (anainama kidogo kisha anainua kichwa) mimi naitwa Liliana nilikuwa ni mtoto wa pekee wa Mr. Peter na Mrs.Paulina Lukupe…wazazi wangu walikufa kwenye ajali mbaya na kuniacha chini ya uangalizi wa shangazi na mjomba wangu… (anainama na kuanza kulia)

Bryson: jikaze…

FLASHBACK: -

(Usiku mtulivu, kaupepo mwanana kanavuma na kila kitu kinaonekana kipo sawa, Mr. Peter yupo pamoja na mke na mwanae wa kike, wanasafiri maana wapo kwenye gari wanaongea na wanaonekana wanaifurahia sana safari hiyo)

Peter: vipi mbona mmenyamaza si muongee jamani au mnasinzia?

Paulina :( mke wa Peter) hatulali…basi tu hatuna cha kuongea…ndo maana tupo kimya…

Peter: pigeni tu hadithi zozote hata za chui na simba

Paulina :( anacheka) yaani wewe kwani Mimi nimekuwa Liliana

Liliana :( mtoto wa miaka kati ya sita na saba)

Peter :( kwa Liliana) eti mama na wewe huna cha kusema?

Liliana :( anatabasamu)

Peter: sawa ila mimi nina cha kukuambia nisikilize…

Liliana :( anaonyesha umakini kwenye kumsikiliza)

Peter: nakupenda sana mwanangu mzuri…sana…wewe ni malkia wangu…nakuombea maisha marefu sana…mwanangu…na mimi Mungu anijalie maisha marefu sana…ili nije niwaone watoto wako na wajukuu

Liliana :( anatababasamu)

Paulina: hata Mimi nakupenda Sana mama yangu…

Liliana :( anatabasamu)

Peter :( anamuangalia mwanae)

(Mara ghafla linakuja Lori linagonga USO Kwa uso na gari waliokuwepo Peter na familia yake)

Paulina: mwanangu (anamrushia Liliana nje kupitia dirishani)

Liliana: mamaaaaaaa

Peter :( anahangaika kuokoa maisha ila anashindwa na hatimaye gari linapinduka na kulipuka)

Liliana: babaaaaaaa, maaamaaaaaa (Analia Sana)

(Watu waliokuwa maeneo hayo wanakuja huku wanakimbia)

Mmoja ya watu: dah…ajali mbaya Sana yaani aisee…sijui kama kuna mtu amepona…

Liliana :( Analia)

Mwanamke 1: eh…kuna mtoto hapa…(anambeba)wewe umetokea wapi?

Liliana: mama Na baba yangu wamekufa…kwenye ajali

Mwanamke 2: dah…aisee pole sana, ngoja tuite polisi ili kwanza huyu mtoto apelekwe hospitali halafu baadae wampeleke nyumbani (anapiga simu polisi simu inaita mwisho inapokelewa) hello…. Mi ni raia mwema kuna ajali imetokea mbaya sana hapa katikati ya Tabora na singida…

Polisi: Asante Kwa taarifa tutawafikia hapo…

Mwanamke 2: Asante… (Anakata simu) polisi wanakuja baada ya muda tukae tusubiri kidogo…

Mwanamume 1: dah…pole Sana mtoto…kwenu wapi.

Liliana :( huku Analia) Mpanda…

Mwanamke 1: na ndugu zako je wako wapi?

Liliana: shangazi yupo Tabora…

Mwanamke 2: pole Sana Mungu akutete katika maisha yako ya uyatima

Mwanamke 1: pole

Liliana: Asante…

(Baada ya muda Fulani polisi wanafika)

Polisi 1 :( anawakaribia watu) habari zenu jamani

Wote :( wanaitikia) salama

Polisi: tumepata taarifa kuwa kuna ajali imetokea na imeua watu

Wote: ndio…

Polisi 1: imegongana nini na nini?

Mwanamke 2: imegongana Lori na gari ndogo (ananyooshea Kwa kidole) gari lenyewe lile pale limeungua na sidhani kama watu wamebaki…

(Mapolisi wanaendea gari na kujaribu kuangalia na wanagundua kweli watu wamebaki majivu tu)

Polisi2: aisee hii ajali ni mbaya sana yaani hata miili yao haikuonekana kabisa

Polisi 1 :( anamuangalia Liliana) Na huyu mtoto ni nani?

Mwanamke 1: ndo mtoto wa marehemu hao…amenusurika

Polisi 1: pole Sana…tutakufanyia mpango ufike Kwa ndugu zako, si unapajua nyumbani?

Liliana: ndio…

Polisi 2: usijali…tutakufikisha mpaka nyumbani na tutawaita ndugu zako waje wachukue hili gari… (Kwa mwanamke 2) yaani hakuna mwili ni majivu tu

Mwanamke 2 :( anasikitika Sana) aisee…

Polisi 2: lakini tutafanya mpango na kila kitu kitakuwa sawa (wanampandisha Liliana kwenye gari na kuondoka nae)

Polisi 1: tunamchukua tunaenda kufanya mpango wa kumfikisha kwa ndugu zake

Watu (wanatawanyika kila mmoja wao anarudi majumbani kwao)

 

Post a Comment

0 Comments