SCENE 4: -
(Ni asubuhi nyingine ya siku
nyingine wiki kadhaa zimepita tangu binti Liliana akamatwe na kuwekwa rumande,
anafika mahakamani yeye pamoja na mwanasheria wake pamoja na maaskari
waliomshika mmoja mkono wa kulia na mwingine mkono wa kushoto, baada ya
kumfikisha kizimbani, anakaa na kusikiliza mashtaka yanayomkabili)
Msoma
mashtaka:(kwa hakimu ambae amekaa kimya
katika kitu chake) mheshimiwa hakimu, mbele yako ni bibi Liliana Kadoke
mkazi wa mpanda na mkoa wa Katavi, anashtakiwa kwa kosa la kumuua Bw. Robert
Michael kisha kuchoma nyumba yake mnamo tarehe moja mwezi wa tano...hii
imethibitishwa na uchunguzi wa polisi nay eye mwenyewe mshtakiwa kukiri kosa hilo
(anakaa kimya)
Hakimu
:( kwa mshtakiwa) je umesikia
mashtaka yako?
Liliana:
ndio…
Hakimu:
je unakubaliana nayo au hapana?
Liliana:
ndio nakubaliana nayo
(Watu waliopo mahali hapo
wakiwemo majirani na familia ya marehemu Robert wanaanza minong’ono ya chini
chini)
Hakimu
:( anagonga meza kuamuru utulivu)
order, order naomba utulivu
(Kuna utulivu wa ghafla)
Hakimu
:( Kwa Liliana) unaweza kuiambia
mahakama kwanini ulifanya vile…
Liliana:
Ni hadithi ndefu sana nyie toeni tu hukumu msiniulize chochote maana ni maelezo
marefu sana
Hakimu:
tunataka tuyasikie maana hatuwezi kutoa hukumu huku hatujasikia upande wako
Lydia
:( yupo kimya wakati wote huo)
Liliana:
hapana, mengine ni ya siri sana
Hakimu:
ndo tunataka kuyasikia tafadhali toa ushirikiano, kwanza swali ambalo
nilitakiwa kukuuliza tangu mwanzo ni kwanini ulimuua Robert Michael?
Liliana:
ilikuwa hasira…
Hakimu
:( anaandika kitu kwenye karatasi yake)
Liliana:Robert
alikuwa ni bwana wangu,alinipenda na kunithamini sana atleast hilo ndo lilikuwa
ndo tumaini na mawazo yangu kuwa alinipenda sana,alinipa kila kitu nilichotaka…alinipeleka
sehemu mbalimbali nilizotaka (anakumbuka
kitu kisha anasikitika sana)kwa kifupi alinipa kila kitu na kuniahidi kuwa
atanioa,baadhi ya ndugu zangu walimjua na kumheshimu na kumpenda
sana,nilimpenda na yeye akanionyesha
kuwa ananipenda(kimya kidogo huku
anakumbuka kitu)…kimbembe kilikuja nilipobeba ujauzito na kwenda kumwambia
kuwa nina ujauzito wake alinikataa katakata na kusema hayuko tayari kuipoteza
familia yake yaani mke na watoto wake huku ni kwamba wakati tunaanza mahusiano
alinihakikishia kuwa hana mke wala watoto na alisema mke na watoto wake
walikufa katika ajali
(minong’ono)
Mama
Neema: kumbe alikuwa na yeye ana
mapungufu yake loh…
Lydia
:( anamuangalia mama Neema bila kusema
jambo lolote)
Hakimu
:( anagonga meza kuamuru utulivu)
endelea…nini kilitokea baada ya hapo…?
Liliana:
ilinisumbua sana maana ukiangalia mimi ni yatima sina mama wala baba…yaani nipo
peke yangu katika hii dunia
Hakimu
:( anamsikiliza kwa umakini mkubwa sana)
Liliana:basi
alipoikataa mimba nikaamua tu niondoke maana tayari nishakataliwa unadhani
nitafanya nini tena,nilipoanza kliniki ya mama wajawazito nilijigundua kuwa
nina maambukizi ya virusi vya UKIMWI,nikaja kumwambia basi angalau anilee
mimi(anaanza kulia)na mtoto
sitamuingilia katika maisha yake na familia yake….alinijibu vibaya a kunifukuza
kama mbwa…sikuwa na kitu cha kufanya niliondoka na kuanza kufanya kazi nyingi
ilimradi nipate kula maana natumia dawa…kila mara nilimpigia simu akawa hapokei
hata nikipiga kwenye namba mpya anapokea akisikia sauti yangu haraka anakata
simu na ananiambia nisimtafute maana mke na watoto wake wanakaribia
kuja,nilichomwambia ni kwamba nahitaji tu msaada na sio vinginevyo,akawa
hataki…hiyo ndo sababu ya hasira yangu nikaamua tu nimuue(anafuta machozi)maana ndo niliona ni njia nyepesi ya kupunguza
maumivu yangu,tafadhali nimeshawaeleza mengi naomba nikapumzike mnihukumu kifo
nife…maaana sina maana tena ya kuishi duniani nimepoteza mtu muhimu sana katika
maisha yangu(Analia)
Hakimu:
Hilo litaamuliwa na mahakama hata hivyo hujatueleza maisha yako ya utotoni
labda tukisikia tutaelewa kwanini ulipata hasira mbaya na kufikia kumuua
mwanaume kikatili vile maana mimi nilivyoambiwa kuwa Robert alikuwa ni baba
mwenye nguvu zake na kila mtu alimjua kwa ukakamavu sasa kuja kuuliwa na binti…
(Anaguna) hiyo imeshangaza wengi na
jinsi kifo kilivyotokea hata polisi walijua kuwa ni mwanaume ndo kaua sasa
ulipojitokeza wewe ndo hapo watu wakabaki midomo wazi…labda nini tatizo…
Liliana:
halipo tatizo (anaanza kulia tena)
nataka tu kufa mheshimiwa (Analia sana)
naomba nife
Hakimu:
hatuwezi kuhukumu bila kusikia chochote
Liliana:(Analia sana)
Hakimu:
ukilia hatutaweza kukusaidia tafadahali elezea kila kitu, tangu ulipokuwa mdogo
na kadhalika
Liliana:
sipo vizuri…
Lydia
:( anamkaribia na kumshika bega) binti
Liliana:(anamgeukia Lydia huku Analia)
Lydia:
jikaze na utuelezee
Hakimu:
mama, hairuhusiwi kuja hapa labda mpaka uruhusiwe
Lyidia:
samahani mheshimiwa...
Hakimu:
usijali
Liliana:
ninajisikia vibaya Sana
Hakimu:
tafadhali mpeni maji ya kunywa…
Liliana
:( anasikia kizunguzungu)
Msoma
mashtaka :( anampa maji kwenye glasi)
Liliana
:( kabla hajayapokea anaanguka chini)
Hakimu:
mkimbizeni hospitali
(Haraka polisi na wahusika
wengine wanambeba na kumtoa nje kwa ajili ya kumpeleka hospitali)
Hakimu
:( anagonga meza) order,
order…tutaendelea kipindi kingine…twendeni tukaendele na shughuli zetu tukutane
hapa tena ijumaa saa nne kamili asubuhi tuendelee na kesi (anagonga meza kisha ananyanyuka na kuondoka zake)
(Watu huo watu wamesimama Kama
ishara ya heshima Kwa hakimu, hakimu anapokuwa ameondoka kabisa kila mmoja
wakiwemo familia ya marehemu Robert wanatawanyika, wakati huo watu mbalimbali wanawateta
mke na watoto wa Robert)
Gabriel
:( anamuendea mmoja wa watetaji) dada…tambua
kuwa hakuna mkamilifu Zaidi ya Mungu…hilo kumbuka na utambue
Dada
:( kimya huku anaangalia chini Kwa aibu)
Raphael:
kaka twende
Lydia:
Gabriel…naomba twende mwanangu
Gabriel
:( anatangulia nje)
Raphael
:( anasikitika Sana)
(Kwa pamoja wanatoka nje na
kwenda kwenye gari lao)
Lydia
:( huku anakaa kwenye gari) wanangu
tulieni mkiendekeza hasira mtagombana na kila mtu…nyie poeni sawa wanangu
wazuri
Michael:
sawa mama…
Gabriel
:( anaanza kuendesha gari)
Lydia:(anawaza moyoni) mume wangu nakupenda
sana na ninakukumbuka kila dakika tangu umefariki ila hii ya kutembea na mtoto
wa watu na kumuambukiza ugonjwa tuliokuwa nao miaka mingi sio vizuri ona sasa
watoto wanashikwa na hasira kutokana na kwamba watu wanawasema vibaya sana kwa
kosa dogo sana ulilolifanya wewe kwa tamaa zako…kila mmoja anamuonea huruma
yule mtoto wa watu uliyempa mimba na kumterekeza labda ungekubali huyo mtoto
pengine mpaka sasa ungekuwepo hai mume wangu
Raphael:
Mama mbona uanaonekena na mawazo?
Gabriel:
sasa ataacha kuwaza baada ya kusikia mume wake aliharibu maisha ya mtoto wa
watu?
Michael:
nakubali daddy…alifanya kosa ila the fact kwamba auawe kisa kitu
kinachozungumzika Kama hicho?
Gabriel:
inategemea dad…alimsukuma vipi mpaka mwisho akaamua kuua…
Raphael:
exactly
Lydia:
sawa nyamazeni kila kitu tutajua hiyo ijumaa
(Wote wanakaa kimya na kuendelea na safari yao ya kuelekea nyumbani kwao)
0 Comments