SCENE 10: -
(Asubuhi nyingine njema, Miriam
anaonekana ndo ametoka kuamka maana anajiandaa na usafi wa asubuhi hususani,
usafi wa mwili wake, anapiga mswaki huku anajiangalia kwenye kioo, anacheza, anafurahi,
wakati huo mama yake anakuja, kwakuwa anacheza na kuimba kwa sauti hasikii na
wala hagundui kama kuna mtu kaingia)
Keddy:(anasimama mlangoni na kumuangalia mwanae)
yaani huyu mtoto sijui nini kimemfurahisha asubuhi yote hii
Miriam:(anaendelea kucheza na kufurahi)
Keddy:
Miriam…
Miriam:(anaendelea kucheza)
Keddy:(anamkaribia na kumshika bega) Miriam
Miriam:(anageuka) mama(anamkumbatia)
Keddy:(anamkumbatia pia) nini mwanangu mbona
una furaha sana …. nishirikishe nami nifurahi
Miriam:
hapana mama kawaida…leo nimeona niamke hivi…si kwa jambo lolote la msingi
Keddy:
eti ee
(Wakati huo simu ya Miriam inaita
na jina linaonekana kuwa ni Jeremy)
Keddy:
mbona shemeji yako anakupigia simu wewe?
Miriam:
hapana mama huyu sio shemeji ni kaka Fulani tunasoma nae nae anaitwa Jeremy
Keddy:ni
rafiki yako?
Miriam:
hapana mama nadhani anataka labda notes kidogo
Keddy:
pokea sasa
Miriam:(anaangalia inaelekea kukata anaiacha)
hata hivyo imekata nitampigia nikimaliza kuoga
Keddy:
sawa... (anaanza kupiga hatua ilia toke
nje ya chumba cha binti yake) fanya haraka leo baba yenu anataka kujumuika
nanyi katika kifungua kinywa…katuamsha mapema tumepika kama wajinga kwahiyo
fanya haraka
Miriam:
haya mama
Keddy:(anatoka)
(Simu ya Miriam inaita tena ni Jeremy)
Miriam:(anaipokea haraka) shemeji…shikamoo?
Jeremy:
marahaba…hujambo…uko wapi mbona hupokei simu?
Miriam:
nipo nyumbani leo sina kipindi chuo hivyo nitakuwa nyumbani tu kwani vipi
shemeji
Jeremy:
naomba tujumuike pamoja katika chakula cha mchana
Miriam:
haiwezekani shem...…siwezi wewe ni shemeji yangu watu watachukuliaje?
Jeremy:
sijali kuhusu watu…naomba nikupitie mchana…tafadhali
Miriam:
hapana…. shemeji wewe unatarajia kumuoa dada yangu…mpigie yeye ndo mjumuike
pamoja na sio mimi
Jeremy:Miriam
nakupenda sana…nakupenda mno…
Miriam:
ah…ah hapo sasa umevuka mipaka unajua ee
Jeremy:
tangu siku ya kwanza nakuona haki ya Mungu nafsi yangu ilikiri kuwa nakuhitaji
wewe na sio Ariana ni wewe ndo nataka kukuoa ni wewe ndo nakupenda please nipe
nafasi najua familia zetu hazitakubali ila kila kitu kitawezekana kwa
Imani…please Miriam nikubalie
Miriam:
samahani kwa kusema haya ila nahisi una wazimu
Jeremy:
wazimu wa mapenzi juu yako Miriam…
Miriam:
Mungu akusamehe sana kwa kutaka kumuoa dada yangu huku wakati huo huo
unanitongoza mimi
Jeremy:
nipo tayari kuwaambia wazazi wangu kuwa nakupenda wewe na nitakuoa wewe mpenzi
wangu mzuri jamani naomba nafasi
Miriam:
nina mpenzi wangu na tafadhali sana acha kuwa unanipigia isije ikawa msala kwangu
(anakata simu kwa hasira)
Jeremy:(bado anaongea) baby nao… (anagundua simu imeshakatwa) hello…Miriam
hello (ananyanyuka kutoka kwenye kiti
chake alichokuwa amekalia ofisini hapo) oh shit… (anapiga tena)
Miriam:(simu ya Miriam inaita ila hapokei)
Jeremy:
Miriam naomba upokee simu yangu tafadhali jamani dah…na mimi ni mpumbavu sijui
kwanini nimemuambia mapema yote hii…ila nampenda sana...nampenda mno…she is the
love of my life…I don’t care namzidi mbali sana, I don’t care itabidi nimsubiri
mpaka amalize shule sitajali…nitamuoa Miriam na si mwingine
(Upande wa Miriam)
Miriam:yaani
vanessa aliniambia wanaume ni mbwa leo nakubali itakuwaje unataka kumuoa dada
yangu wakati huohuo unataka kuniaoa mimi halafu iweje…anataka atuonje wote huyu
mwanaume mjinga sana…na heshima yangu kwake ndo imefika mwisho sitaki hata
kumuona(anaingia bafuni kuoga baada ya
kama dakika 15 anatoka kuoga anachukua simu yake kuangalia anakuta kuna missed
calls nyingi sana za Jeremy)yaani
huyu jamani ananitafutia matatizo mimi jamani…(meseji inaingia anasoma)jamani naomba tuonane tuongee kidogo
tafadhali (anajisemea moyoni)yaani huyu ananitafutia shida kabisaaaaa yaani
mimi sitaki(anampigia rafiki yake simu
inaita mwisho inapokelewa)hello…wewe vanessa yule kaka anataka kuniletea
shida nyumbani hapa
Vanesa:
kafanyaje na kaka gani mbona sikuelewi?
Miriam:si
shemeji
Vanessa:
ah mimi nilijua tu tangu siku ile kuwa nyinyi ni wapenzi mnapendana
Miriam:
what do you mean tunapendana jamani? mimi sipendani nae hata kidogo na wala
sitaki kupendana nae
Vanessa:
okay amefanyaje?
Miriam:
ananitongoza…
Vanesa:
mkubali…kwani wewe unaogopa nini?
Miriam:
una kichaa
Vanessa:(anacheka) sasa unadhani utafanyaje
mwenzio ndo tayari keshakuzimikia?
Miriam:(anakata simu ghafla) yaani namwambia
vanessa anacheka na kuona ni utani kweli jamani hii ni haki
(Mama yake anakuja kwa mara
nyingine)
Keddy:
wewe bado unafanya nini? baba yako anakutafuta…halafu shemeji yako amekuja
Miriam:(moyo unalipuka)
Keddy:
vaa haraka tunakusubiri(anatoka)
Miriam:
Mungu wangu amekuja kufanya nini jamani haya nayo si mateso? (anavaa haraka haraka kisha anatoka bila
kupaka chochote si mafuta wala nini) shikamoo baba…
Ken:
marahaba mwanangu…Hujambo?
Miriam:
sijambo(anatabasamu)
Jeremy:(anatabasamu pia)
Miriam:(kwa Jeremy) shikamoo shemeji
Jeremy:
marahaba
Miriam:
shikamoo dada Ariana
Ariana:(amekaa pembeni ya Jeremy) marahaba
Miriam:(kwa Mary) shikamoo ma mdogo…
Mary:
marahaba mwanangu hujambo?
Miriam:
sijambo
Keddy:
bora umekuja kila mtu hapa anakusubiri wewe
Ariana:(anabenjua
midomo)
Miriam:
samahani kwa kuwachelewesha
Ken:
usijali mama
Jeremy:(anamuangalia sana Miriam)
(Haraka
Miriam anamsaidia Mary kutenga kifungua kinywa mezani, na baada ya muda
wanamaliza na kukaribisha watu kwa ajili ya kifungua kinywa hicho, watu wote
wanaamka na kwenda mezani kwa ajili ya kifungua kinywa hicho)
Ken:(anawaita wanae ili waje wakae pembeni yake)
naomba mniweke katikati yenu nimewakumbuka sana wanangu na cha kushangaza mkwe
wangu mtarajiwa nae amekuja kuungana nasi katika kifungua kinywa hiki
Jeremy:(anacheka sana)
Mary
na keddy:(wanaangaliana kisha wanacheka)
Ariana:(anaonyesha chuki na hasira)
Miriam:(anafurahi)
0 Comments