SCENE 9: -
(Jeremy amesimama nje la gari
lake yupo chuoni kwa kina Miriam na anaonekana anamsubiria mtu)
Jeremy:(anatembeatembea kama mtu anayesubiri kitu
kwa shauku kubwa) mbona haji?
Miriam:(anatokea akiwa na marafiki zake)
Jeremy:(anamuona) eeh huyo hapo…
Rafiki
yake Miriam:(anagundua Jeremy
anamuangalia sana Miriam) eeh yule kaka anakuangalia sana….
Miriam:
yupi (anageuka kumuangalia) nani… (anagundua ni Jeremy) ah…kumbe
shemeji…shemeji yangu huyo anatarajiwa kumuoa dada yangu…
Rafiki:(anaguna) anakuangalia sana…mbona
Miriam:na
wewe kawaida tu … (kwa Jeremy)
shemeji
Jeremy:(anatabasamu)
Miriam:(anamuendea) shikamoo shemeji…
Jeremy:
marahaba…hujambo
Miriam:
sijambo
Jeremy:za
darasani?
Miriam:
nzuri… (anaangalia huku na huku) dada
yuko wapi?
Jeremy:
hayupo…nimekuja peke yangu…
Miriam:
kumbe
Rafiki:(anawaangalia chinichini)
Miriam:
okay naomba niwatambulishe...shemeji huyu anaitwa Vanessa ni rafiki yangu
kipenzi yaani tupo kama mtu na dada yake
Vanesa:(anatabasamu) nafurahi kukufahamu shemeji
yetu
Miriam:na
huyu anaitwa Jeremy…ni shemeji yetu
Jeremy:(anatabasamu kisha anajisemea moyoni) ipo
siku utasema mimi ni mpenzi wako na ni shemeji wa rafiki yako
Miriam:
shemeji sisi tuna haraka kidogo umekuja kumpitia rafiki yako?
Jeremy:(anababaika kidogo)
Miriam:
vipi? kuna mtu unamngojea?
Jeremy:
hapana…unajua nilikuwa naenda nyumbani kwenu nikaona nipitie hapa…nikupe lifti
au (anamuangalia Vanessa) au nimekosea?
Vanessa:
hapana shemeji hujakosewa, Upo sahihi kabisa
Jeremy:(anamuangalia Miriam usoni kisha anatabasamu)
nakupenda
Miriam:(anashangaa) nini?
Jeremy:
shemeji yangu…
Miriam:
aha!!
Jeremy:(anacheka) basi sawa kwanini msipande
gari twendeni?
Vanessa:
sawa…ila mimi mtanipitisha nyumbani sidhani kama nitafika huko kote
Jeremy:(haraka haraka) sawa haina shida
Vanessa:
sawa
(Wanapanda gari na haraka Jeremy
analiondoa kuelekea nyumbani)
Jeremy:je
mtapenda kupata icecream…kidogo au soda?
Vanessa:
ofcourse
Miriam:
wewe Vanessa mimi baba na mama watakuwa na wasiwasi sana…
Vanessa:
okay ngoja… (anachukua simu na kumuandikia meseji Mary) anti…Miriam atachelewa
kidogo tunaenda kula icecream na shemeji Jeremy
Mary:(anaipokea meseji na kuijibu) haya lakini
msichelewe sana…
Vanessa:(anapokea meseji na kuisoma kwa nguvu)
haya lakini msichelewe sana, (kwa Miriam)
unaona Miriam anti Mary huwa ana upendo na ni mwelewa sana…halafu nilisahau
kukuuliza mbona mnafanana sana na anti Mary…
Miriam:
hata mimi sijui kwakweli…
Jeremy:(anamuangalia Miriam kupitia kioo kidogo
kilichopo mbele) Miriam (anajisemea moyoni) wewe ni mzuri
Miriam:
abeee shemeji
Jeremy:
tunaenda kwenye icecream au soda au tunaenda nyumbani?
Miriam:
twende kwenye icream ila tusichelewe…
Jeremy:
haina shida (anaendelea kuendesha gari
huku kila mara anamuangalia Miriam kupitia kioo cha mbele)
Vanessa:(anagundua kuwa Jeremya anamuangalia sana Miriam)
mmmh (anajisemea moyoni) huyu shemeji
anampenda Miriam huyu…ona anavyomuangalia vizuri ila kama ni mchumba wa Ariana Miriam
hata asijaribu kumkubali huyu kaka ikitokea amemtongoza
(Hatimaye wanafika katika mgahawa
mmoja)
Jeremy:(huku anakaa) hapa sidhani kama kuna
icecream
Vanessa:
hapa hapa panatosha bwana…
Jeremy:
agizeni chakula...mimi sili
Vanessa:
mimi nitakula
Jeremy:(huku anatabasamu) wewe Miriam je?
Miriam:mi
nitakunywa soda
Vanessa:
yaani huyu muoga nyie…
Miriam:
hapana sijisikii tu kula
Vanessa:(kwa Jeremy) shem…hata hatujala tangu
asubuhi hapa unavyotuona
Jeremy:
sasa mwenzio mbona hataki kula?
Vanessa:
uoga tu (anamuita mhudumu) anti…
Miriam:(anamfinya)
Vanessa:(anamtoa mikono) wewe vipi…agiza huko
Mhudumu(anafika)karibu niwasikilize
Vanessa:mi
naomba chipsi kuku…na huyu hivyohivyo
Jeremy:(anatabasamu kisha anamuangalia Miriam)
Mhudumu:(anaondoka kuelekea jikoni)
Miriam:(anaonekana kuwa na wasiwasi)
Vanessa:
wewe...nini? si upo na shemeji yako? nani atakuuliza?
Miriam:
haya bwana (anajitahidi kuwa mchangamfu)
Jeremy:(simu yake inaita anaiangalia anaona ni
Ariana anaona asiijibu)
Miriam:
vipi? pokea simu shemeji…
Jeremy:si
ya muhimu ni ya kazi na muda wa kazi umeisha
Miriam:
aha kumbe
Jeremy:
yeah…
(Baada ya dakika kumi na tano
mhudumu anakuja na chakula cha Miriam pamoja na Vanessa)
Mhudumu:
karibuni…
(Miriam na Vanessa wanapokea
vyakula na taratibu wanaanza kula wakati huo Jeremy anaagiza kinywaji cha
baridi na kuanza kunywa huku Vanessa na Miriam wanakula taratibu, wakati
wanaendelea kula Jeremy anamuangalia sana Miriam, na Miriam akimtupia macho
anaangalia chini na kukwepesha macho, hali inaendelea hivyo hivyo)
Mirriam:
shemeji ndo umekataa kula?
Jeremy:
wewe kula tu shemeji yangu usiwe na wasiwasi na mimi
Mirriam:
(Anatabasamu)
Jeremy:
(anaonekana kupagawa na Mirriam)
Vanessa:
(anamuangalia sana Jeremy)
Jeremy:
(haachi kumuangalia Miriam)
0 Comments