SCENE 11: -
(Jioni ya siku nyingine tena,
Jeremy yupo chuoni kwa kina Miriam anamsubiri Miriam amesimama nje ya gari yake
na anaonekana hana haraka kabisa hata ikitokea Miriam amechukua muda mrefu,
baada ya kusimama hapo muda mrefu hatimaye Miriam na rafiki yake Vanessa
wanatoka darasani)
Vanessa
:( anamuona Jeremy) ona baby kaja
Miriam
:( hajamuona) baby gani?
Vanessa:
Jeremy
Miriam
:( anamuona Jeremy baada ya kuangaza kwa
muda)
Vanessa:
Jeremy baby
Miriam:
sikiliza nikwambie kitu Vanessa Jeremy sio baby wangu na sitaki awe baby wangu
sijui nimeeleweka au bado?
Vanessa:
kamwambie sasa...ila sikia huyu kaka anakupenda na anachofanya sasa hivi
anakufuatilia sana na anataka uwe wake na anaonekana yupo serious wewe si
ulisema ana kampuni zake sasa embu jiulize kwanini anaacha kazi zake
anakufuatilia kasungura kama wewe…mpe nafasi
Miriam:
wewe una kichaa shoga yangu unajua kabisa Mimi na dada yangu tunahangaika
kuyaweka mahusiano yetu vizuri halafu sasa hivi unanishauri utumbo acha ujinga
huyu kaka ni shemeji yangu na sitawahi kuwa mpenzi wake hata iweje sitaki kuwa
mpenzi wake mimi ndo nimeamua
Vanessa:
sawa haina shida shoga yangu
Jeremy
:( anawafata) hamjambo warembo
Vanessa:
hatujambo shikamoo
Jeremy:
marahaba (kwa Miriam) Miriam?
Miriam:
shikamoo... (Huku anaangalia pembeni)
Jeremy:
marahaba…
Miriam
:( Kwa Vanessa) Vanessa twende
Jeremy:
wapi?
Miriam:
nyumbani kwani wapi tena?
Jeremy:
Miriam nimekuja kukuchukua
Miriam:
unipeleke wapi?
Vanessa:
acha kumjibu hivyo jamani
Jeremy:
Miriam, unajua ninavyokupenda wewe mtoto...kwanini usinipe nafasi? nakupenda na nipo serious
Miriam:
kaka hilo neno umeshaniambia mara nyingi sana ila sikutaki nina mpenzi wangu
naomba uendelee na maisha yako mimi sikutaki...huelewi nini? Sitaki mimi jamani
Jeremy:
Miriam…
Miriam:
wewe ni shemeji yangu naomba ibaki kuwa shemeji yangu kila mtu atashangaa kuona
eti shemeji ni hawara yangu
Jeremy:
sina mpango wa kuwa hawara yako nataka kuwa mumeo nataka uwe malkia wa himaya
yangu
Miriam:
dada yangu ndo malkia wa himaya yako sio mimi naomba basi uelewe jamani kwani
nini tatizo?
Jeremy:(kwa Vanessa) kwani kupenda ni kosa? (kwa Miriam) basi kama ni kosa niadhibu
nipo tayari kuchukua adhabu yeyote ila tu (anashusha
pumzi) …naomba nafasi
Miriam:
jamani kaka haiwezekani
Jeremy:
dah…Miriam…naomba please
Miriam:
(kwa msisitizo) no!!!
Vanessa:
Miriam, mpe mwenzio nafasi jamani kwani nini tatizo?
Miriam:(anajikuta anapandwa na hasira) wewe Vanessa
kama unamuonea huruma si umchukue? mimi sitaki matatizo na familia yangu,
ukweli ni kwamba huyu kaka ni mchumba wa dada yangu…na alikuja nyumbani ili
amuoe dada yangu yaani hapa walipo wapo kwenye hatua na maandalizi ya harusi…halafu
wewe leo unaniambia nimpe nafasi huyu
Jeremy:
dada yako sina mahusiano nae yeyote na yeye mwenyewe anajua hilo
Miriam:
dada yangu anakupenda sana Jeremy mno na mno na ndoto zake ni kuoana na wewe
Jeremy:lakini,sina
hisia zozote juu yake nakiri kwamba ni kweli mimi na wazazi wangu tulikuja
kwenu tukiwa na lengo la kumchumbia Ariana lakini nilipokuona I swear moyo
wangu ulikupenda wewe na sikuwa tayari kunyamaza kimya juu ya hili…hata wazazi
wangu nitawaambia,sio kosa nina uhakika hata dada yako ataelewa jamani kuwa
moyo huamua yote na sio kichwa,ni kweli kichwa changu kinasema nimuoe Ariana
lakini nini kitatokea baada ya mimi kumuoa Ariana?nitajuta maisha yangu yote
kwamba sikuwa tayari kupambana na akili yangu ili niishi kwa furaha…
Miriam:
familia yangu inanipenda Sana…na sitaki kuharibu uhusiano nilionao nao mimi na
familia yangu tafadhali sana
Jeremy:
wazazi wetu watatuelewa tu,
Miriam:
wewe ndo unaona kuwa watatuelewa, ila hakuna mzazi atakayekubali kuwa mwanaume
alikuja kumchumbia mtoto wake mkubwa halafu mwisho wa siku akawa na mahusiano
na mtoto mdogo…naomba uelewe kuwa hatuwezi kuwa na mahusiano hata kwa siri
Jeremy:
Miriam unaogopa nini?
Miriam:
kwanza wewe ni mkubwa sana kwangu hatuendani
Jeremy:
Miriam hiyo haijalishi mapenzi hayaangalii umri
Miriam:
nimekataa sitaki
Jeremy:
Miriam nampigia baba yangu simu sasa mbele yako namwambia kuwa sitaki kumuoa
Ariana
Vanessa:
maskini kaka wa watu mpaka anatia huruma
Miriam:
sasa unampigia simu ili iweje?
Jeremy:
ngoja (anatoa simu yake aina ya iphone 14
na kutaka kumpigia baba yake)
Miriam:
acha ujinga…Jeremy unadhani haya ni rahisi?
Jeremy:
nakupenda Miriam…
Miriam:
hatuwezi kuwa pamoja katika haya maisha
Jeremy:
Miriam
(Miriam anamvuta Vanessa ili waondoke,
Jeremy anapanda gari lake haraka kisha anawafata kwa nyuma)
Jeremy:
Miriam…ngoja nikwambie okay sitamwambia mtu, itakuwa siri yetu wawili please…na
sitafanya kitu chochote ambacho hutotaka…the fact kwamba wewe ni girlfriend
wangu itatosha sana
Miriam:(anasimama) siri??!!halafu…?
Jeremy:
ndugu zetu watajua tu mbele kwa mbele
Miriam:
hapana Jeremy
Vanessa:
mbona mwenzio katoa wazo zuri tu…mpe mwenzio nafasi
Jeremy:
ukinipa nafasi nitakutunza sana na utapenda
Miriam:
hapana…(anakimbia)
Jeremy:(anashuka kwenye gari kisha anamkimbiza)
sikiliza Miriam
Miriam:
nakuomba sana sitaki kugombana na dada yangu…nihurumie Jeremy
Jeremy:
wewe ndo unihurumie…hurumia moyo wangu, hurumia hata shughuli zangu…sasa
umekuwa kama ugonjwa umekuwa kama chakula siwezi kuishi bila kukuona…nakupenda
my queen(anamkumbatia)
Miriam:(anajikuta anamkumbatia pia) una kichaa
hujui baba anaweza kuja wakati wowote kuja kunichukua
(Gari la baba yake linakuja)
Miriam:
Kama niliota baba huyo hapo naomba niende…
Jeremy:
okay nitakupigia baadae mazungumzo yetu hajaisha
Miriam:
naomba usinipigie simu
Jeremy:
namwambia baba yako kuwa nakupenda sana...nitatoboa siri hapa sasa hivi sema
suu…
Miriam:
sawa nipigie…
Jeremy:
(anatabasamu kidogo) okay bye…
Miriam
:( anaondoka kuelekea gari la baba yake
lilipo) Vanessa twende
Ken:
nimemuona mtu Kama Jeremy anafanya nini?
Miriam:
ana ndugu yake hapa, amekuja kumpitia
Ken:
okay…Mimi nawahi sitamsalimia (anapanda
kwneye gari na kuliondoa)
0 Comments