SCENE 6: -
BAADA YA MIAKA 18: -
(Usiku mwingine mtulivu sana,
nyota zinaonekana kwa wingi angani kila mtu anaonekana kalala, Ariana ambae kwa
sasa amekuwa mtu mzima kidogo anaonekana yupo disko anacheza huku anakunywa pombe,
yupo na vijana wengi wanaonekana kutapanya pesa bila mpangilio. Kwakuwa amekuwa
mtu mzima sana amebadilika sana pamoja na njia zake mbaya anaonekana mrembo
sana)
Rafiki
yake: ila unawatesa wazazi wako…huna mwelekeo rafiki yangu
Ariana:
Angelica we kunywa kama umechoka kalale…usinichoshe…wazazi wangu waliamua
kuniletea kitoto eti mdogo wangu na wakafanya kila kitu kuonyesha kuwa
wanampenda yeye na sio mimi mtoto wao waliomzaa wenyewe, sasa unadhani nina
faida gani kwao kama kwa midomo yao wamekuwa wakimsifu huyo mpumbavu mbele
yangu…kila kitu nilichofanya ni kosa sana kwao unadhani nitafanyaje…acha
niponde raha mama zikiisha nitaongeza
Angelica:
lakini rafiki yangu unajikomoa mwenyewe na sio wazazi wako kwanini usitafute
njia nyingine…wewe fanya yaliyo mema hata kama wazazi wako hawaoni…Mungu
atakusaidia rafiki yangu lakini unavyofanya hivi unawaudhi wazazi wako na Mungu
pia
Ariana:
umemaliza? okay tutaonana kesho… (anatoka
nje na kupanda gari lake alilokuwa ameliegesha nje na kuliondoa, anaenda kwa
muda na hatimaye anafika nyumbani)
Miriam:(binti mrembo sana na anaonekana kuwa ni mcha
Mungu, ni yuleyule mtoto aliyeokotwa nje ya geti miaka 18 iliyopita na kulelewa
kwa upendo mkubwa kama mtoto aliyezaliwa kwenye familia hiyo) dada... (anafungua mlango)
Ariana:
embu nipishe huko (anamsukumia pembeni)
Keddy:(amebadilika anaonekana ni mama wa makamu na
mvi zinaanza kutokea) Ariana… (anamfuata
alipokuwa amesimama) unatoka wapi sasa hivi?
Ariana:(anafyonza) acha kunizingua, wewe unajali
nini? wewe si unamjali sana huyo zawadi uliyopewa na Mungu…sijui mimi ni zawadi
uliyopewa na shetani
Mary:(na yeye anaonekana ni mama wa makamu na mvi
zinaanza kutokea) Ariana...
Ariana:
kelele…na wewe mfanyakazi uliyeishi kwetu miaka 18 utasema ndo nini
sijui…usiniongeleshe sina muda huo wa kusikiliza ushenzi...
Ken:(anaonekana ana mvi) Ariana (anamzaba kibao)
Ariana:(anashika shavu) embu niacheni… (anaingia chumbani kwake kwa hasira)
Ken:(anakaa kwenye sofa) sijui tumfanye nini
huyu mtoto jamani jinsi miaka inavyoenda ndo anazidi kuwa mtata
keddy: mume wangu acha kufikiria haya…
Mary:
tumsamehe tu
Keddy:
Mungu alitupa zawadi ya mtoto tena wakati ambao ulikuwa muafaka (anamuangalia Miriam) mwanangu, mvumilie
dada yako…ni dada yako wa tumbo moja embu sahau yote na umpende hivyo hivyo
Miriam:
sawa mama (anaachia tabasamu zuri)
Mary:(anajisemea moyoni) mwanangu nimzuri sana,
ingekuwa vipi kama ningetoa mimba, au ningekuacha tu upate tabu mpaka ufe
mwanangu…kweli Mungu ni mkuu alinielekeza mpaka kwa hawa wazazi wenye upendo
mwingi…nakupenda mwanangu na ninawapenda hata wazazi wanaokulea kukusomesha na
kukupa malezi mazuri
Keddy:(anamshtua) mwenzangu vipi mbona
unaonekana una mawazo mengi tatizo nini mama?
Mary:
hapana dada…ni kawaida tu
Keddy:au
unamuwaza Ariana?
Mary:
Ariana muacheni tu atakuja kuwa mtulivu
Keddy:
mpaka lini…leo hii ana miaka 30 lakini hajishughulishi kwa chochote katika haya
maisha jamani atakuwa mgeni wa nani? siku tukitoweka hapa duniani?
Ken:
basi kwa maana hiyo aondoke nyumbani kwangu...
Miriam:
baba…tafadhali usimfukuze dada (anapiga
magoti pembeni ya baba yake) tafadhali baba…
Ken:
ndo uamuzi wangu…mimi ni mtumishi wa Mungu na nyumba yangu inatakiwa imtumikie Mungu
na sio anachofanya Ariana binti yangu mkubwa
Miriam:
baba tafadhali… (machozi yanamlenga)
Mary:(anajikuta anamuonea huruma mwanae) basi
mwanangu baba yako atamsamehe
Keddy:
baba Ariana msamehe mwanao tafadhali
Ken:
hapana…siwezi, unless abadilishe mienendo yake ndo nitamsamehe nampa wiki hii nzima...
Ariana:(anatokea chumbani kwake na mabegi) wala
usijisumbue wiki nzima ya nini…?
Miriam:(anamfata Ariana) dada
Ariana:
mimi sio dada yako…wewe mbwa
Mary:
Ariana…
Keddy:(Analia) mwanangu jamani…mbona umekuwa
hivi nilikuzaa ukiwa ni mtu mwenye upendo hukuwa mjeuri
Ariana:(anawapuuzia wote)
Ken:
kwanini uko hivyo…?
Ariana:
nipoje? niwatendee nini…miaka hii yote nimewaridhisha kwa nguvu zangu zote lakini
hamjawahi kuridhika kila mara huyo mtoto wenu ndo kawa kipaumbele…kila kitu
kizuri ni yeye na kila kitu kibaya kimefanywa na mimi…niwafanyeje…ndo maana
nimechagua kupita hii njia sijali chochote nafanya nachojisikia naondoka na
kama huyo Mungu wenu mnaomuabudu kila siku humu ndani yupo basi atanisaidia na
mimi hata kama ni mbaya na sina utakatifu wa huyu mtoto wenu mpendwa
Keddy:(anamshika
mkono) mwanangu nisamehe mimi mama yako yamkini ni kweli kabisa, nilikusahau
naomba msamaha na kukuahidi sitarudia tena nitakujali nitakuheshimu
mwanangu…yamkini ni kweli kabisa napitiwa kibinadamu naomba msamaha wako
mwanangu na ninakuahidi kuwa utaishi vizuri tu mama
Ariana:
mumeo amenifukuza…na mimi natii sheria ya mfalme na kukuahidi kuwa nitafanya
kama ulivyamrisha
Ken:(anaamua kujishusha) mwanangu sasa hivi
ni usiku mama unadhani utaenda wapi? naomba unisamehe mimi baba yako kwa haya
niliyosema nimetumia hasira tu
Miriam:
dada msamehe baba, nisamehe hata na mimi
Ariana:(anamsukuma) usizoee kuniita mimi
dada…umeelewa?
Mary:
Ariana…usifanye hivi…huyu ni mdogo wako…
Ariana:(anakaa kimya)
Keddy:
sawa mama…rudisha vitu vyako ndani ikapumzike tutazungumza kesho asubuhi…
Ariana:
nendeni tu…nimeshawaelewa nitakaa tu hapa nyumbani…mpaka
Ken:
pale utakapoolewa
(Kila mtu anaonekana amesahau
lililotokea kwa muda kidogo)
Mary:
walisema watakuja…kutoa mahari hivi karibuni
Keddy:
tunawasubiri kwa hamu
Ken:
harusi yako itakuwa nzuri sana mwanangu na ya kifahari sana
Miriam:
nitacheza sana…siku hiyo jamani
Ariana:
lakini sikuwapa jibu kama nataka kuolewa au lah…
Keddy:
mimi ukiniahidi kuwa utaolewa ukifika miaka 30…yule kijana anakupenda sana na
ana haraka ya kukuoa…
Ariana:(anaweka mizigo pembeni yake kisha anakaa
maana muda wote huo alikuwa amesimama) sijawahi kuwa na mahusiano na huyo
mtarajiwa wangu mnaniambiaje niolewe nae?
Ken:
yeye anakujua na anataka kukufanya uwe malkia katika himaya yake
Ariana:
haya, sawa nitamuona…
Keddy:
utanipa jibu mwanangu…anakuja nahisi kesho…wanakuja na washenga…kuomba undugu
Ariana:(anaguna kidogo) bado sijampenda sasa
atakujaje na washenga
Miriam:
nina uhakika kuwa utampenda, ni mwanaume wa dizaini unayoipenda, mrefu, mzuri
na Zaidi ya yote ana hofu ya Mungu
Ariana:(anajisemea moyoni) yaani huyu nae sijui
nani kamwambia nataka mwanaume mwenye hofu ya Mungu?
Miriam:na
pia ana uwezo wa kimaisha kwa kweli yupo vizuri ni mtoto wa rafiki wa baba
Ariana:
okay…nimewaelewa (ananyanyuka na kwenda
chumbani kwake)
(Wanaobaki
sebuleni wanaonekana wana furaha na kusahau ugomvi uliotokea muda mfupi
uliopita)
Ken:ni kumvumilia tu…ni mtoto
wetu hatuna jinsi… (anacheka kisha ananyanyuka na kuingia chumbani kwao)
(Miriam,
Keddy na Mary nao wanaingia kila mmoja wao chumbani kwake)
Mary: kila kitu kitakuwa sawa
hata sijali (anajifunika shuka na kulala)
0 Comments