SCENE
7: -
(Usiku
wa siku hiyohiyo ya jumamosi, Patrick na mpenzi wake wameshafika nyumbani kwa
Patrick, wao pamoja na marafiki zao, kila mtu yupo kwenye chumba chake isipokuwa
Patrick na Olivia wamekaa chumba kimoja)
Olivia:
baby… (Anaweka kichwa chake begani kwa Patrick) umemwambia mama kuwa
nitalala huku?
Patrick:
nishamwambia baby
Olivia:
Asante nime enjoy sana leo…
Patrick:
usijali nipo kwa ajili yako
Olivia: asante…nina
kiu…naomba maji ya kunywa...
Patrick
:( anaiendea friji ndogo iliyopo chumbani humo) huwa kuna maji humu
ngoja nikupe (anaifungua anagundua kuwa hakuna maji) kumbe hawajaweka
Olivia:
kachukue…
Patrick
:( anacheka kisha anaelekea jikoni, baada ya hatua chache anafika jikoni
anafungua friji)
Monica
:( anakuja akiwa amevaa khanga moja nyepesi Sana iliyomfanya kuonyesha
asilimia kubwa ya maungo yake ya ndani) ah…samahani Shem…sijui nimekosea?
Patrick
:( anaonekana kutojali anachokiona mbele yake) unataka nini Shem?
Monica:
natafuta maji ya kunywa Shem...
Patrick:
yapo chumbani huko angalia kwenye friji
Monica
:( anabana sauti inakuwa Kama ya mtoto anayemdekea mama yake) hamna maji
kwenye friji
Patrick:
ah! Itakuwa dada Halima alisahau kuweka ngoja nimwambie
Monica
:( anamvuta mkono)
Patrick
:( Kwa mshangao) vipi?
Monica:
nyumba yako nzuri kweli Shem
Patrick:
nashukuru
Monica:
(anang’ata midomo yake) nzuri kweli Kama wewe
Patrick
:( anaondoka kuelekea chumbani kwake)
Edwin:(anapita
maeneo ya chumba cha Patrick, anakuta mlango wa Patrick uko wazi kidogo na
Olivia yupo anabadilisha nguo ingawa haonekani vizuri ila mwili wake kwa nyuma
unaonekana vizuri sana, Edwin anabaki anashangaa kuona umbo zuri vile) wow…
Patrick
:( anatokea kwa nyuma yake) Edwin…vipi?
Edwin :(
anashikwa na kigugumizi) ha…mna kitu, nilikuwa natafuta maji
Patrick :(
anacheka) masihala mengine hayafai unajua eeh...
Edwin:
kwanini…
Patrick:
maji chumbani kwangu na mpenzi wangu kwani wewe ni mara yako ya kwanza kuja
katika hii nyumba usijue maji yanakaa wapi? anyways kaa tu chumbani da Halima
anakuletea sasa hivi
Da.
Halima :( anaweka maji kila chumba)
Patrick:
nadhani yapo tayari
Edwin:
poa usiku mwema (anaenda chumbani kwake)
Monica
:( anapita na khanga yake moja mbele ya Patrick)
Patrick
:( anaingia chumbani kwake, anakaa pembeni ya Olivia)
Olivia:
vipi?
Patrick:
ah…poa (anajisemea moyoni) yaani hawa watu siwaelewi…sijui nimwambie
Olivia…ah ngoja nipotezee ikiendelea ndo nitamwambia
Olivia:
Patrick hauko sawa
Patrick:
kwanini…
Olivia:
sijui ila nakuangalia usoni nakuona umebadilika mara baada ya kutoka kuchukua
maji kuna tatizo?
Patrick:
ah usijali my darling nipo poa …
Olivia:
hujapenda nini baba nambie
Patrick:
usijali mbona Mimi nipo poa…labda itakuwa usingizi
Olivia
:( anatabasamu kisha anadeka kidogo) lala basi baba
Patrick
:( anatabasamu) Kwa kudeka (anacheka)
(Olivia anamlalia kifuani wanaendelea kuzungumza
huku kila mmoja wao akionekana kufurahia faragha ile)
Patrick:
lala na wewe…mbona umekodoa macho tu
Olivia
:( anacheka)
Patrick:
Olivia mke wa Patrick…naitamani hiyo siku
Olivia:
hunishindi Mimi jinsi navyotamani kuwa mkeo
Patrick:
ifike bwana maana hapa tunamkosea bwana tunazini
Olivia
:( anainuka) chumba cha wageni kiko wapi nikalale huko
Patrick
:( anacheka) wewe embu lala
Olivia:
au nilale chini
Patrick
:( anacheka) lala
(Wanaendelea kutaniana huku kila mmoja wao
anafurahia faragha hiyo)

0 Comments