SCENE
6: -
JUMAMOSI
(Jioni
nyingine tulivu kabisa…kuna upepo Fulani mwanana unavuma, mbali na upepo kuna
hali ya kama mvua kutaka kunyesha, Patrick na rafiki yake kipenzi wamekaa
katika mgahawa Fulani na unaonekana kuwa ni wa gharama, wanaongea huku wanapata
vinywaji taratibu)
(Simu
ya Patrick inaita)
Patrick
:( anatabasamu kidogo)
Edwin:
vipi? Mbona unatabasamu mwenyewe?
Patrick :(
anapokea simu) honey…vipi mmeshafika?
Olivia:
ndio baby mpo wapi?
Patrick:
ngoja natoka kuja kuwachukua…
Olivia:
poa tunakusubiri hapa getini
Patrick:
sawa my Queen… (Anakata simu kisha anamgeukia Edwin) mwanangu tayari
wameshafika…ngoja nikawachukie nakuja sasa hivi
Edwin:
poa hamna noma (anaendelea kunywa kinywaji chake)
Patrick
:( anatoka nje moja Kwa moja anaenda mpaka walipo Olivia na rafiki yake)
Monica :(
anaangalia huku na huku anaona kwa mbali mtu kama Patrick) shemeji huyo
Patrick :(
anatokea anaachia tabasamu mara baada ya kumuona mpenzi wake) baby (anambusu
Olivia mdomoni)
Monica
:( anamuangalia Patrick Kwa tamaa kisha anajisemea moyoni) dah…huyu
mwanaume mzuri jamani
Patrick
:( anamshika mkono Monica) shemeji mambo vipi?
Monica:
poa vipi?
Olivia
:( anatabasamu muda wote)
Patrick:
poa (anawaongoza njia) njooni huku maana sie tumejificha mbali Sana
(Kwa
pamoja wanaenda mpaka alipokuwa amekaa Edwin)
Patrick:
Wale tulikokuwa tunawasubiri Kwa muda wa masaa karibia mia hawa hapa
Olivia :(
anacheka) jamani baby kwani tumechelewa Sana?
Patrick:
vibaya Sana… (Anafyonza kisha anacheka) muone (Anacheka tena)
Edwin :(
anamuangalia Olivia Kwa tamaa pia na yeye anajisemea moyoni) mrembo Sana…duh...Sasa
huyu anafaa kuwa mke wangu na sio mwingine…Patrick jiandae kumpoteza huyu
mwanamke…she is mine
Patrick:
warembo karibuni mketi
(Wanawake
wanakaa, Olivia anakaa pembeni ya Patrick na Monica anakaa pembeni ya Edwin)
Patrick:
hii inaitwa double date…
Edwin :(
anacheka huku anamuangalia Sana Olivia)
Monica :(
anamuangalia Sana Patrick)
Patrick:
ok naomba niwe ndo msemaji maana naona wote mnaogopa ogopa…ok…baby huyu (anamuonyeshea
Edwin) ni rafiki yangu wa pete na kidole anaitwa Edwin…yaani ni kama kaka yangu,
tumesoma wote tumehangaika wote (kwa Edwin) eti si tumehangaika ee (anacheka)
Edwin :(
anaguna) tumehangaika wapi huku wewe ulikuwa mtoto wa kishua usinitanie (anacheka
kidogo)
(Wanacheka)
Patrick:
unaniaibisha brother
Edwin :(
anacheka) pole mwaya
Olivia
:( anaachia tabasamu Safi linalowachanganya wanaume wote hapo) nashukuru
kukufahamu Shem (anampa mkono)
Edwin :(
anaupokea kisha anamuangalia usoni na kumpa tabasamu la kichokozi)
Olivia
:( anakuwa hayuko huru na tabasamu hilo)
Patrick:(anacheka)
mzoee tu… (kwa Edwin tena) brother… (anamuangalia Monica) huyu ni
rafiki wa mke wangu anaitwa Monica
Monica
:( anaachia tabasamu)
Edwin:
Oh, she is beautiful
Monica
:( anacheka)
Olivia
:( anatabasamu) jamani dah!!!Mnafaa kweli kuwa mtu na mtu wake (anacheka)
au nasema uongo baby boo
Patrick:
(anatabasamu) sawa kabisa (anamuangalia Monica) na shem…kwa kuwa
rafiki yako hajataka kunitambulisha naomba nijitambulishe…naitwa Patrick
Kalenzi ni mume wa miss Olivia
Olivia :(
anatabasamu) jamani nilikuwa najiandaa kukutambulisha mbona umejiwahi (anacheka)
(Wote
wanacheka)
Monica
:( anampa mkono Patrick huku na yeye anaachia tabasamu Fulani la kitata)
Patrick
:( anakuwa Kama anashangaa kidogo ila anaona apotezee tu)
Edwin:
karibuni ladies na agizeni chochote, hapa ni kuparty mpaka majogooo… (Anakunywa
kinywaji kidogo)
Patrick :(
anatania) boss kasema (anamshika mkono Olivia wake)
(Monica
na Edwin wanaangalia chinichini na wanaonekana hawafurahii kitendo kile cha
wawili wale kuonyesha mapenzi yao vile maana kila mmoja amevutiwa na shemeji
yake, yaani Monica amempenda Patrick na Edwin amempenda Olivia)
Patrick:
Shem agizeni…Olivia agiza…mbona mmepooza jamani…
Olivia:
hatujapooza honey...Tunasubiri mhudumu…
Edwin :(
anamuangalia Sana Olivia)
Patrick:
ok my dear…hamna shida (anamshika Olivia kidevu)
Mhudumu
:( anakuja kuwasikiliza) karibuni jamani
Patrick
:( anamuangalia Olivia kisha anatabasamu)
Olivia:
ah…Mimi nitakula chipsi na kuku na coca zero
Patrick:
eeh…kuna watu hawanywi pombe kabisa…walokole
Olivia:
umeanza uchokozi wako
Patrick:
pole mama…(anacheka)
Olivia
:( anajifanya kudeka)
(Wanacheka)
Monica:
Na Mimi hivyo hivyo
Patrick:
Mimi nataka ugali na samaki freshi kabisa najua ndo mahali pake hapa (anacheka)
Edwin:
naomba ugali pia na nyama kavu
Mhudumu:
sawa (anaondoka kuelekea jikoni)
Patrick:
sasa…Edwin vipi brother?
Edwin :(
anatabasamu huku macho yote yapo kwa Olivia) kuhusu nini…?
Patrick:
Monica huyu hapa
Edwin:
she is very beautiful…ningependa kuwa nae (anamuangalia Olivia Kama ni
kwamba anamaanisha Olivia)
Patrick:
she is mine…naona unamuangalia Sana Olivia
Edwin:
hapana mi naongea tu wala simaanishi yeye…natamani ningekuwa na Monica
(Wote
wanacheka)
Olivia:
wow…hiyo nzuri--nimependa
Edwin :(
anajisemea moyoni) ungejua kwamba nimevutiwa Na Olivia na nipo radhi
kufanya kitu chochote ili niwe nae
Olivia:
(Kwa Monica) vipi kuhusu wewe best…?
Monica:
Ni mzuri hata Mimi ningependa kuwa nae
(Wote
wanafurahi tena)
Monica
:( anajisemea moyoni) nakupenda Patrick, nakupenda wewe tu…wewe ni mzuri
sana
Patrick:
kwahiyo Mimi na mke wangu tumewaunganisha marafiki zetu wawe mke na mume…
(Wote
wanacheka)
Mhudumu
:( analetea chakula mezani na kuwapa kila mtu jinsi alivyoagiza)
Patrick:
sasa Leo wote mnaenda kulala kwangu, msidanganye maana kesho hakuna anayenda
kazini…si ndio Olivia mama?
Olivia:
yes...ni wazo zuri sana (kwa Monica na Edwin) eti mnalionaje?
Edwin:
Ni wazo zuri
Olivia:
ila ubaya sijamuaga mama…
Edwin:
utamuaga tu…
Patrick:
hakuna kitu kibaya kitakachotendeka hatukuui wala kukuchuna ngozi kuwa na Amani
Olivia:
sawa sijakataa...ila mama ni lazima nimwambie
Patrick:
nitamwambia
Olivia:
usisahau…
Patrick:
siwezi (anaendelea kula) siwezi kuacha kumwambia mama yangu mrembo yule
Olivia
:( anaguna kisha anacheka)
Monica:
kwahiyo mlikutana mtandaoni…
Patrick:
yes…
Monica:
hivi watu wanaokutana mitandaoni huwa wanadumu na wao?
Patrick:
mapenzi ni upofu, unaweza ukampenda mwanamke uliyekutana nae njiani tu
ukamsalimia akakuitikia vizuri ukamgeukia na kumuangalia ukajikuta unampenda
sembuse iwe kwa watu wanakutana instagram wanachat sio chini ya mwaka mzima
wataachaje kupendana
Edwin:
mna bahati mmekutana…mkapendana, kuna watu wanakutana hivyo halafu
wanadanganyana
Patrick:
nampenda…she is just perfect for me na sioni wa kunifanya niachane nae
Edwin :(
anaangalia chini)
Olivia:
nakupenda pia my baby…
Patrick:
asante love…
Monica;
mapenzi mubashara eti eeh
Olivia :(
anacheka)
Patrick:
kuleni tuondoke maana tumekaa muda mrefu Sana
(Wanaendelea
kula huku kila mmoja akionekana na furaha isipokuwa kwa Monica na Edwin maana
mara nyingi wanaonyesha kuchukizwa na kitendo cha Olivia na Patrick kuonyesha
mapenzi yao hadharani, wanaendelea kunywa na kula huku wakiburudika na miziki
mbalimbali iliyokuwa ikisika mgahawani hapo)

0 Comments