SCENE
10: -
(Asubuhi
ya kesho yake siku moja baada ya Monica kuja kumwambia Olivia maneno mengi
yamhusuyo Patrick, Olivia amekaa sebuleni kwao huku akionekana hana raha hata
kidogo na Mawazo mengi yanaonekana kuwepo kichwani kwake)
Olivia:(anajisemea
moyoni)yaani wanaume(anasikitika kidogo)wapo kama wamezaliwa na mama
mmoja yaani wana uongo mwingi sana mioyoni mwao sijui wana shida gani jamani(ananyamaza
kidogo)yaani Patrick ni wa kunificha na kunidanganya kuwa hajawahi kufanya
kosa lolote kwamba yeye ni msafi…yote hiyo ni uongo mkubwa yaani sitaki hata
kumuona,alikuwa anauza madawa ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo
na kuua kabisa inamaana Patrick ni muuaji…(anasikitika)kwahiyo ni muongo
aliposema yeye ni mlokole alidanganya pia(anasikitika)
Mama :( anakuja
mahali pale) Olivia… (Anakaa pembeni yake) nakuona tangu Jana huna
raha nini tatizo mama yangu
Olivia:
sina shida mama…kuwa na Amani mama mimi nipo poa tu mama usijali mama yangu
Mama:
hauko sawa mrembo wangu
Olivia:
wasiwasi wako tu mama
Mama:
nimegundua kuwa tangu Monica aondoke umekosa raha kabisa mama, mimi ni mama
yako nan do mtu na rafiki yako wa karibu na wa kweli naomba uniambie tafadhali
Olivia:
Patrick…ni muuza madawa ya kulevya…sio kuuza tu anayatumia mama
Mama :( anabaki
mdomo wazi) hapana Olivia huo ni uongo mkubwa…wewe nani amekwambia?
Olivia:
Monica…ameambiwa na mpenzi wake ambae ni rafiki wa karibu wa Patrick…anasema
lakini alikuwa anayauza zamani na mpaka akafungwa
Mama:
sasa mwanangu hiyo si ilikuwa ni zamani kwani bado anayauza?
Olivia:
hata Kama hayauzi mama ilikuwa ni jukumu lake kuniambia mi mbona sijamficha chochote?
na isitoshe kwanini anaficha? inamaana anayauza bado...
Mama:
Olivia…
(Anakatishwa
na sauti ya kengele ya mlangoni)
Mama:
nani tena?
Olivia:
ngoja nikafungue (ananyanyuka kwenda kufungua) oh…Shem karibu…
Edwin:
Asante…mambo vipi shemeji yangu.
Olivia:
Safi… (Simu yake inaita anaiangalia anagundua kuwa ni Patrick anakata)
karibu ndani shem
Edwin :(
huku anaingia) Asante
Olivia
:( simu inaita tena anaamua kuipokea) unasemaje Patrick…nimeshakuambia
kuwa tuachane…sikutaki tena
Patrick:
naomba nafasi nyingine nitayarekebisha yote hayo mke wangu…nakupenda Olivia…
Olivia:
usiniite mke wako Patrick maana Mimi sio mke wako (anakata simu kwa hasira)
Mama:
samahani Kwa kukuingilia lakini hivyo sio jinsi ya kumjibu mwanaume
aliyekusaidia na mengi Olivia…nakuomba umuombe msamaha hata kama amekosea
hutakiwi kumjibu hivyo
Olivia:
hapana mama simuombi msamaha Patrick
Mama:
Olivia...
Edwin:(anajisemea
moyoni) huyu maza nae vipi…anataka kumshawishi Olivia amsikilize Patrick na
akimsikiliza tu wanasamehana na kurudiana na mimi sitaki hivyo hata kidogo (kwa
mama) shikamoo mama
Mama:
marahaba baba hujambo na wewe ni…
Olivia:
rafiki wa karibu wa Patrick
Mama:
sawa karibu…ungependa nini asubuhi hii maji, kahawa, juisi au chai
Edwin: Asante
mama ila mimi tayari nimeshakunywa chai, asante mama labda siku nyingine
Mama:
sawa baba ngoja niwaache... (Anaondoka na kuingia chumbani kwake)
Edwin:
iam so sorry…mi nilijua tayari Patrick keshakuambia kuwa alikuwa muuza na
mtumiaji wa madawa ya kulevya ndo maana nikaropoka…samahani
Olivia:
haina shida shemeji… (Anakaa kimya)
(Upande
wa Patrick amekaa na Monica na Monica anaonekana kumpa faraja shemeji yake kwa
kumshika bega)
Patrick
:( anampigia tena Olivia) dah…hakuna mtu mbishi Kama Olivia…yaani mpaka
aniruhusu kuongea nae ndo nitakuwa na Amani
Monica:
yaani navyomjua rafiki yangu akishatema harudishi tena kinywani…yaani ni mbishi
sana huyu mtoto
Patrick
:( anaiweka simu sikioni inaita mwisho inapokelewa)
Monica
:( anaongea kwa sauti ya mahaba Fulani kama mtu ambae yupo na mtu wake)
Patrick…
Olivia: Oh,
umenipigia simu kuniringishia kwamba una demu mpya kwamba unabandika na
kubandua…ok baba maisha mema…
Patrick:
come on Olivia…acha utoto basi…naomba unisikilize mpenzi wangu…
Olivia :(
anakata simu Kwa hasira)
Edwin:
nini tena?
Olivia:
yupo na demu mwingine yaani bandika bandua…
Edwin :(
anajisemea moyoni) good job Monica…sasa ngoja nicheze nafasi yangu…tuone
yatatokea yapi… (Kwa Olivia) yaani hawezi kubadilika Patrick…bado tu ni
playboy…si ana hela…?
Olivia:
kwahiyo Mimi ananipigia ili iweje?
Edwin:
labda Kama ulivyosema kuwa anajaribu kukuringishia kuwa humbabaishi kwa lolote
ana pesa na akitaka mwanamke hata kutoka uarabuni anapata
Olivia
:( anashikwa na hasira)
(Upande
walipo Patrick na Monica)
Patrick:
sijakuelewa kwanini umeniita Kwa hiyo sauti tena hasa pale ulipogundua kuwa
Olivia kasha pokea simu?
Monica
:( anacheka) Shem…una stress kaa utulie mi mbona nimekuita kawaida Sana
Patrick:
hii ni mara ya pili unafanya vituko mara ya kwanza ulikuja jikoni kwangu umevaa
khanga moja huku maungo yako yanaonekana vizuri na unajua mimi ni mwanaume…
Monica
:( anacheka tena) shemeji bwana…Mimi sikujua Kama nitakukuta
jikoni…kwani Mimi ni malaika kujua leo majira ya usiku nitamkuta shemeji yangu
jikoni
Patrick
:( anamkazia macho) Olivia ni mpenzi wangu na ni Mungu mwenyewe ndo
kapanga awe wangu…na atakuwa mke wangu…sio wewe sio nani atakayeweza
kunitenganisha na Olivia…haya nayo yatapita….na mimi na yeye tutakuwa wapenzi
tena sio wapenzi tu wachumba ambao tutakuwa tayari kuoana
Monica :(
anachukia Sana)
Patrick:
sasa dada…kwanza sijui kwanini upo hapa ila wakati huu nataka uondoke na sitaki
kukuona tena labda uje na Olivia na ikijitokeza hii tena nitamwambia
Olivia…now…get out…
Monica:
mi sina nia mbaya lakini
Patrick
:( kwa sauti ya ukali kupita kiasi) leave…au huelewi? Ondoka mama yangu
sitaki nikuone hapa mama…kabla sijachukia Zaidi toweka
Monica
:( anatoka nje)
Halima:
vipi mdogo wangu…tatizo nini…mbona umechukia Sana?
Patrick:
nimegombana na Olivia na hanitaki tena…
Halima:
kisa nini?
Agnes :(
huku anakuja) ila mi Patrick ninakuambia kila mara tena tangu nimemuona
huyu dada…yaani huyu dada ni kimeo ndo aliyekuharibia mahusiano yako na mpenzi
wako
Halima:
yaani siwaelewi kwani kuna nini?
Agnes:
kuna mtu tena Nina uhakika kuwa ni huyu dada alienda kwa Olivia na kumwambia
kuwa Patrick aliwahi kuuza madawa ya kulevya…na alikuwa anayatumia pia na
kikubwa alifungwa…
Patrick :(
yupo kimya)
Halima:
na wewe huyo mpenzi wako bado ana akili za kitoto sasa hapo tatizo ni lipi
mpaka likamfanya achukie na kukuacha
Agnes:
Point Ni kwamba Olivia anasema kuwa Patrick hakumwambia Hilo
Halima:
hamna bwana hizo ni hasira tu za kawaida zitaisha na atakupigia simu…sasa
kilichokufanya umfukuze shemeji yako kama mbwa ni nini?
Patrick:
huyu demu mjinga Sana…yaani Mimi naongea na Olivia yeye ananiita utasema mimi
ni bwana wake…Olivia amekasirika kweli amedhani mimi nimeingiza mwanamke…
Halima:
kumbe mjinga eeh…yaani
Agnes:
mi nilimuona tu tangu mwanzo anakuja hapa yaani anamuonea wivu mwenzie bila
hata kujificha…
Patrick:
hanipati…kwanza dada zangu tunatakiwa tujiandae kwenda kumtolea Olivia mahari
Halima:
hallloooooooooo
Agnes :(
anapiga vigelegele) hayo ndo maneno leta mke hapa
Patrick :(
anacheka) ILA sasa ndo nitafute namna ya kumrudisha huyo mke…kimke chenyewe
kina hasira (anacheka) tufanye mpango turudishe jiko Hilo…lituivishie
vyakula sie
Agnes:
ndo hivyo…tufanye mpango arudi tu
Halima:
atarudi tu, yaani wewe ukishindwa niite…
(Wote
wanacheka)
Patrick:
oh…Olivia my queen…hakuna wa kututenganisha
(Upande
wa Olivia na Edwin)
Olivia:
Shem…Kama hautojali naomba uniache nikae peke yangu…siko vizuri…
Edwin:
sawa usijali my dear…na ukiwa na shida yoyote tafadhali niite…
Olivia:
Asante
Edwin :(
anatoka na kuondoka zake)
Olivia:(machozi
yanamlenga)yaani Patrick ni wa kuniacha na kuchukua mwanamke mwingine hata
siku mbili hazijaisha tangu tuachane kweli ng’ombe wa maskini hazai…(machozi
yanamtoka)sawa bwana…na mimi Mungu atanijalia nitapata wa kunipenda…(anachukua
simu yake na kufuta namba ya Patrick)maisha mema Patrick wangu…nakupenda
lakini inaonekana huwezi kuacha tabia zako za kuchezea na kutupa wanawake kama
takataka mara baada ya kuwachezea…yaani umenichezea mwisho umenitupa kama
takataka(anaendelea kulia kimya kimya bila hata mama yake kujua kuwa analia)
Edwin:(amesimama
dirishani anamchungulia Olivia kwa mbali) Olivia… (anacheka huku
anatikisa kichwa) nimegongea msumali wa moto moyoni mwako nataka hasira
zikupande ili umchukie Patrick na kunitaka mimi peke yangu
Olivia
:( anaendelea kulia Sana)
Edwin:
good job Monica…umenirahisishia kazi...Nitakuwa karibu Sana na Olivia kiasi cha
kumfanya amsahau Patrick…nitamfanya aone kwamba mimi ndo mwanaume nimpendae kwa
dhati na sio Patrick
Olivia
:( anaangalia picha ya Patrick) Patrick but why baby…kwani nilikosa wapi badala
uje tuyamalize wewe umeamua kuwa na mwanamke mwingine
Edwin
:( anacheka Sana) oh… (Anapiga simu Kwa Monica)
(Simu inaita kisha inapokelewa)
Edwin:
mchezo kwisha yaani hapa wala hawatatafutana tena…cheza nafasi yako vizuri
usije ukapokonywa tonge mdomoni
Monica:
usisahau kufanya hivyo pia(anacheka)

0 Comments