SCENE
26: -
JIONI
YAKE: -
(Wapendwa
wa Miriam wamekusanyika nyumbani kwa Mr. Ken na mkewe wakisubiri hatima ya Miriam)
Ken:
yaani kila sehemu tumemuangalia hatujamuona…sio sehemu ya tukio wala mochwari…(Analia)sijui
nini kimemtokea huyu mtoto…sijui aliungua akabaki majivu (Analia sana) sielewi
Jeremy :(
Analia Sana)
Ariana
:( anajifanya kulia)
Keddy :(
Analia)
Mary :( Analia
Sana)
(Kwa
mbali wanasikia geti linafunguliwa)
Ken:
nani tena? Hatutaki wageni
Sauti :(
Kama ya Miriam) ma mdogo nifungulie
Mary:(anashangaa)
Miriam? (kwa wote) huyo ni Miriam? jamani nasikia sauti ya Miriam (anafuta
machozi) jamani Miriam…
Sauti:
da Ariana?
Ariana
:( anashangaa) Miriam?
Ken :(
ananyanyuka na kufungua mlango)
(Tazama
ni Miriam, kila mmoja aliyekuwepo hapo anapigwa na butwaa)
Jeremy :(
bila kutegemea anamkumbatia Miriam mbele ya wazazi) oh My God Miriam…Asante
Mungu
Mary: MUNGU
MKUU…haya ni maajabu yake
Ken:
ulikuwa wapi Miriam embu kaa
Miriam:
vipi kwani? (anaangalia nje) Vanessa, Naila njooni ndani
(Vanessa
na Naila wanaingia ndani)
Jeremy:
Naila...mlikuwa wapi nyie mmetutesa...
Miriam:
tulikuwa chuoni
Ken:
embu nihadithie mwanangu imekuwa vipi mpaka mpo hapa?
FLASHBACK
(Miriam
na Naila wanapanda kwenye basi)
Miriam:
yaani mimi unajua sijisikii kwenda hii trip
Naila:
najua kwanini hutaki itakuwa kwasababu ya Vanessa
Miriam:
wala sio utani haki ya Mungu yaani siwezi kabisa kwenda bila Vanessa na yeye
sasa nampigia simu unadhani hata anapokea sijui ana janga gani
Naila:
twende kwao
Miriam:
halafu gari litatusubiri utasema gari la baba zetu?
Naila :(
anacheka) wewe nae hata hivyo si hutaki kwenda trip kwanini tusiende kwa
kina Vanessa hii wikiendi nyumbani watajua tupo trip kumbe tupo mjini hapa hapa
Miriam
:( anacheka)
Naila:
twende zetu
Miriam:
let’s go
Naila :(
Kwa dereva) anko tuache hapa
Dereva:
kuna nini?
Miriam:
wewe tushushe tu
Dereva:
shukeni
(Wanashuka
kwenye basi)
Dereva
:( anawaona) naomba niwaambie kitu…yaani sisubiri ndege wa mtu hapa
Naila:
nyie nendeni tu
Dereva:
haya... (Anaondoa gari)
Miriam:
ngoja basi nimwambie hata da Ariana kuwa sijaenda tour
Naila:
tutawaambia tukifika kwa Vanessa
(Wanapanda
daladala)
BAADA
YA KAMA DAKIKA 15: -
(Naila
na Miriam wanafika nyumbani kwa kina Vanessa)
Vanessa :(
anawaona) karibuni nyie vimburu
Naila:
yaani ungejua hatujaenda tour kwa ajili yako wewe kimbulu mchanga
Vanessa:
Mimi si niliwaambia hamuwezi kwenda bila mimi, mimi nina vibe najua
kuchangamsha
Miriam:
halafu mbona hupokei simu?
Vanessa:
nilikuwa nafua nimefua nguo utasema sijui nini yaani sasa hivi ndo nimemaliza
kufua
Miriam:
naomba maji ya kunywa kwanza
Vanessa:
kaeni (anaelekea jikoni baada ya muda anarudi na glasi mbili za maji, moja
anampa Miriam na nyingine anampa Naila)
Vanessa:
sasa tupike halafu twende
Miriam:
wapi?
Vanessa:
kwenu…
Naila:
sisi tumekuja kukaa mpaka kesho jioni…
Vanessa:
be my guest
(Wanacheka)
Miriam:
tuonyeshe pa kuanzia…halafu muziki tafadhali
Vanessa:
una kichaa?
(Wanacheka
na kufurahi, wanawasha muziki wanaanza kucheza na kuenjoi)
SAA
NANE MCHANA: -
Miriam:
sasa tumekula tumeshiba time for TV
Naila:
weka ITV
Vanessa:
sasa ya nini?
Naila:
kuna marudio ya tamthilia ya wiki nzima
Vanessa:(anaweka)
(habari
zilizotufikia hivi punde)
Naila:
embu sikilizeni breaking news
Msoma habari:
habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa basi lililokuwa limebeba
wanafunzi wa chuo cha sheria waliokuwa wanaenda trip kwa ajili ya kujifunza
limepinduka vibaya na kulipuka na kuuwa watu wote waliokuwemo humo
Miriam:
My God…(anashangaa)Mungu ni Mkuu sana…MUNGU MKUU
Naila:
kabisa…duh na sisi tusingemuwaza Vanessa tulikuwa tunakufa eeh Mungu
Miriam:
twendeni chuo
(Wanatoka
na kwenda chuoni)
END
OF FLASHBACK
(Walipo
Miriam na familia yake)
Miriam:
ndo mambo yalikuwa hivyo
(Watu
wanashusha pumzi na kumtukuza Mungu)
Ken:
nina maswali…maana tulikuwa tumechanganyikiwa watu tumeshinda tunalia kama
wajinga shemeji yako amelia kama mjinga
Miriam:(anacheka)
Ken:
mbona simu yako ilikuwa haipatikani?
Miriam:
simu ilizima chaji sikuwa na chaja kwa bahati mbaya niliacha chaja nyumbani
Naila:
ila nakumbuka tulikuja sema mlikuwa hampo
Keddy:
ndio kuna kipindi tulienda eneo la tukio
Mary :( anamkumbatia
Miriam) namtukuza Mungu hata kwa hili leo amejidhihirishia ukuu wake,
nimefurahi kukuona mwanangu…(anambusu)nakupenda sana mama
Miriam:
asante ma mdogo, nakupenda pia ma mdogo(anatabasamu)
Jeremy:(anashusha
pumzi) naona mimi niende maadamu Miriam amesharudi nina Amani sasa
Ken:
haya baba…karibu tena (kwa Miriam) msindikize shemeji yako
Miriam:
sawa baba (anaongoza njia)
Jeremy:(anamfuata
nyuma)
(Wanafika
nje)
Jeremy:
I cried for you my love nilidhani nimekupoteza my queen
Miriam:
comeon baby nilikupigia simu kutumia namba ya Naila mara nyingi sana
Jeremy:
sikuiona…iam so sorry (anambusu mdomoni)
Miriam:
tupo nyumbani na unajua hilo
Jeremy:
iam so sorry
Ariana :(
anawachungulia kupitia dirisha la chumbani kwake) hawa washenzi bora hata Miriam
angekufa...ona wanavyojifanya kupendana
(Walipo
Jeremy na Miriam)
Jeremy:
I swear ningejiua, Kama ungekuwa ni mmoja wa wanafunzi waliokufa
Miriam :(
anamuangalia usoni)
Jeremy:
nini mbona unaniangalia hivyo?
Miriam:
macho yako yamevimba kweli
Jeremy:
nimelia, nimezimia yaani siku yangu imekuwa mbaya kweli…wazazi wangu wamesafiri
ila nimewaambia yaani wamechanganyikiwa ila nikitoka hapa nitawapigia…tutafanya
conference call nao
Miriam:
iam so sorry baby nimewasumbua
Jeremy:
it is okay (anatabasamu)
Miriam:
haya nenda tutaongea
Jeremy:
okay bye baby… (anaondoka)
0 Comments