SCENE
27: -
BAADA
YA WIKI MOJA: -
(Majira
ya saa moja usiku, Ariana amesimama katika jumba Fulani ambalo linaonekana ni
bovu na wala halina mtu anayeishi humo, amesimama anaonekana kama ni mtu
anayesubiri kitu Fulani kwa hamu sana, baada ya kusimama kwa dakika kadhaa
hatimaye mtu aliyekuwa anamsubiri kwa hamu si mwingine ni Miriam)
Miriam:
dada yamekufika yapi mbona umeniita kwa haraka sana na mbona--- (anapashangaa)
mbona tupo hapa?
Ariana
:( anamuangalia kwa hasira mithili ya simba mwenye njaa anataka kumeza mtu
au kitu)
Miriam :(
anamshangaa) dada kuna tatizo?
Ariana:
lipo…au nikuambie kuwa yapo? Mengi tu
Miriam :(
anazidi kumshangaa) sikuelewi
Ariana:
tangu umekuja maishani mwangu nimekuwa sina hata Amani (anatembeatembea)
Miriam:
usiseme hivyo dada Mimi ni mdogo wako naanzaje kukukosesha amani?
Ariana
:( anacheka kwa kejeli) eti mdogo wangu…nani alikuambia kuwa mimi ni
dada yako (anacheka kwa dharau) wewe sio mtoto wa baba na mama yangu
Miriam
:( anapigwa butwaa) eti?
Ariana:
itika Miriam maana nimekuita…
Miriam:
unanidanganya…dada kwanini unanichukia hivyo (analengwa na machozi)
Ariana:
nakuchukia sio kidogo wewe Malaya…tangu wazazi wangu wamekuokota nje ya mlango
wetu…umekuwa ni kuzuizi cha furaha yangu wazazi wangu wamekuwa wakikupenda wewe
Zaidi ya mimi…haya nilipopata mchumba nae ukamchukua…
Miriam:
dada kuhusu Jeremy si tumeshamaliza? Wewe si ulisema huna pingamizi na
mahusiano yetu
Ariana:
wewe ni mshenzi, muuaji Malaya unayetafuta njia yoyote kuharibu furaha za watu...Upo
Kama mama yako
Miriam:
mama yangu ni nani kama mama yangu si mama yangu
Ariana:
mama yako ni Mary
Miriam:
ma mdogo Mary?
Ariana:
ndo hivyo
Miriam:
ulijuaje? na kwanini unaniambia hivyo leo?
Ariana:
mama yako ni fala kama wewe tu…aliniambia mwenyewe sasa sijui ili iweje? (Anacheka
kwa dharau)
Miriam
:( Analia) lakini dada Ariana...
Ariana:
bado najibu maswali yako...Umeniuliza kwanini nakuambia haya sababu wewe Leo
unaenda kufa mshenzi wewe
Miriam:
usinifanyie Mimi hivyo dada pamoja na kwamba umesema kuwa mimi sio mdogo wako
lakini tumekuwa pamoja tumelelewa kama ndugu kabisa dada sasa leo hii ukitaka
kuniua
Ariana:
utafanya nini?
Miriam:
sina cha kukufanya
Ariana
:( anapiga makofi mara mbili)
(Wanakuja
wanaume wawili walioshiba vizuri kwa lugha nyingine mabaunsa)
Ariana:
pigeni hii mbuzi mpaka muue sina hasara… (Anavuta kiti kisha anakaa)
Miriam :(
anamuangalia kwa huzuni) dada
Ariana: :(
anacheka) unaumia mwenyewe…unaogopa? (Anacheka kisha anakunja uso ghafla)
hata mimi naumiaga Zaidi na Zaidi nikikuona wewe na Jeremy
Miriam :(
Analia) dada jamani
Ariana
:( Kwa mabaunsa) pigeni huyo…
(Mabaunsa
wanachukua fimbo kubwa kila mmoja wao na kuanza kumpiga Miriam bila huruma)
Miriam
:( Analia) dada… (Anamuangalia Ariana usoni) dada…
Ariana:
nakuchukia Sana yaani kufa mshenzi wewe
Miriam:
dada …naumia (analia)
(Mabaunsa
wanaendelea kumpiga)
Miriam
:( anatoka damu puani)
(Simu
ya Miriam inaita)
Ariana:(anampokonya)
nani(anaangalia)eti king bae(anafyonza)huna hata haya… (kwa
baunsa mmoja) embu njoo…unaona hii simu ijibu…mjibu vibaya sana…mwambie
wewe ni mpenzi wa Miriam na hapa mlipo mnakula starehe asiwasumbue mwambie pia
unajua yeye ni sponsa amenunua gari na yupo mbioni kununua nyumba
Miriam
:( anasikitika Sana)
Ariana
:( Kwa baunsa) kaongelee kwenye utulivu
Baunsa
:( anaipokea simu huku anaelekea sehemu tulivu kidogo) hello? Nani?
Jeremy
:( anashangaa) wewe ni nani umeshika simu ya mke wangu?
Baunsa
:( anacheka kwa dharau) eti mke wako…huna hata haya wewe mshenzi...Miriam
ni mke wangu kaka oh nimekumbuka wewe ndo yule sponsa wake uliyemnunulia gari
na upo kwenye mchakato wa kumnunulia nyumba…oh My God sponsa tunashukuru kwa
upendo wako…haya kama hutojali jifunze kuheshimu wapenzi wa watu wewe kwa
Miriam ni sponsa tu
Jeremy:
Mimi sio sponsa braza wewe ndo sponsa kwa taarifa yako
Baunsa :(
anacheka kidogo) embu achana na mpenzi wangu wewe… (Anakata simu)
Jeremy:
hello
(Simu
imekatwa)
Jeremy
:( anapiga ukuta Kwa hasira) shit…damn this woman!!!!…Miriam ni wa
kunifanyia hivi mimi jamani…I hate her… (Anatupa simu pembeni Kwa hasira)
(Upande
walipo Ariana, mabaunsa na Miriam)
Ariana
:( kwa baunsa) umenipa raha sana...na mimi lazima nikupe raha baby...Twendeni
disco halafu baadae tutaenda kulala pamoja
Baunsa 1
:( anatabasamu) sawa boss...
Ariana:
ila nitafurahi na kuwapa wote raha mkimuua huyu mjinga
Miriam
:( amelegea hana hali nzuri)
Baunsa 2
:( anampiga)
Miriam
:( anazimia)
Ariana:
kafa…kafa (anashangilia) kafaaaaa… (Anaenda kumuangalia)
Miriam:
(ametulia)
Baunsa 1:
hajafa kazimia tu
Ariana
:( anachukua chupa ya maji anammiminia Miriam) amka wewe usijifanye umekufa
(kwa baunsa 1) baby umenifurahisha...Nipe mkanda wako mara moja
Baunsa 1
:( anavua mkanda na kumpa Ariana)
Ariana
:( anaupokea na kumnyongea Miriam kwa nguvu zake zote)
(Mabaunsa
wanampa moyo kwa kumshangilia)
Baunsa
1: ndo maana yake mama…fanya mambo mama
Ariana
:( anamnyonga mdogo wake kwa nguvu zake zote)
Miriam :(
anatapatapa Kama mtu aliyezama kwenye maji na kukosa pumzi)
Baunsa
2: uaa huyo hana adabu…uaaaaa
Ariana
:( anaendelea kumkaba)
Miriam
:( hatimaye anaishiwa nguvu na kutulia)
Ariana
:( ananyanyuka) Safi...Haya twendeni, atakuwa amekufa sasa
Baunsa
1: tukamzike...
Ariana:
tusihangaike…tuondoke
Baunsa
1: ulale pema peponi mrembo(anacheka)
(Wanaondoka na kumuacha Miriam akiwa hajitingishi)
0 Comments