MUNGU MKUU 25


 

SCENE 25: -

(Majira ya saa nane mchana wa siku hiyohiyo Jeremy yupo ofisini kwake anaonekana kuhangaika kupiga simu)

Anita :( anaingia alipo Jeremy) boss vipi? Mbona kama una kitu kinakusumbua?

Jeremy: simpati Miriam…sijui kwanini (anajaribu tena)

Anita :( anaguna) unaonekana yaani hujazoea kukaa masaa mengi bila kumpata my lady wako

Jeremy: exactly Anita yaani kuongea nae ni mfano wa dozi yaani asubuhi mchana na usiku bila kukosa

Anita: (anacheka)

Jeremy: wewe embu acha nipambane nimpate ananichanganya huyu jamani

(Simu haipatikani)

Jeremy: jamani huyu mtu yuko wapi?

Anita: hata TV hutaki kuangalia (anawasha runinga)

(Habari zilizotufikia hivi punde)

Jeremy: embu sogea tuone hiyo habari

Msoma habari: basi lililobeba wanafunzi wa chuo cha sheria limepinduka vibaya na kulipuka na kuua wanafunzi wote…

Jeremy :( anapiga kelele) Miriam… (Analia Sana) jamani mpenzi wangu…Miriam…Miriam wangu…Miriam No…No... No…no Miriam baby but why God why? (analia sana)

Anita: Mungu wangu (anazima runinga)

Jeremy: (anazimia)

Anita: boss…boss…boss (anatoka nje kuomba msaada) jamani naombeni msaada boss kazimia huku…

 (Watu wanakuja kumsaidia Jeremy)

Kaka 1: boss

(Upande wa familia ya kina Miriam, kama ilivyo kwa Jeremy nao wana wasiwasi juu ya Miriam)

Mary: mbona Miriam hana tabia ya kuacha kupiga simu tangu asubuhi hajatupigia simu kutuambia kama kafika au kakwama

Ken: yaani hata sijui jamani huyu mtoto

Ariana :( anajisemea moyoni) si afie huko (anafyonza)

Keddy: maskini mwanangu…sijui amepatwa na nini asipige simu

(Jirani mmoja anakuja)

Jirani: hodi jamani Habari za hapa jamani (anaonekana ana wasiwasi sana) hivi yule binti yenu mdogo si alikuwa anasafiri kwenye basi Fulani sijui walikuwa wanaenda kwenye masomo

Keddy: ndio kwani vipi?

Jirani: nimesikia kwenye habari kuwa basi limepinduka na kuua wanafunzi wote

Mary :( anapiga kelele) mwanangu (Analia Sana)

Keddy: mwanangu… (Analia Sana)

Ken :( anapata shinikizo la moyo) ah

Ariana: baba…baba (anamuwahi baba yake) Mungu wangu… (Anakimbilia chumbani kwa baba yake anachukua vidonge vyake vya presha) Mungu ananipenda…yaani sijafanya chochote Miriam kafa... (Anacheka) sasa kila kitu kitakuwa cha kwangu peke yangu (anarudi sebuleni) baba...Kunywa vidonge vyako baba (analeta maji ya kunywa) kunywa baba utulie baba yangu

Ken :( anakunywa) Asante mwanangu (anainuka kidogo) Ariana embu mpigie mdogo wako simu muulize yuko wapi mbona anachelewa kurudi nyumbani bwana…mwambie tunaogopa (anaanza kulia) mwanangu hawezi kuwa amekufa jamani… (Analia) hawezi kuwa amekufa jamani

Jirani: yaani baba Ariana yaani wamesema kuwa wanafunzi wote waliokuwepo wote wamekufa…yaani gari limelipuka...Na unavyoujua moto huwa hubakizi mtu yaani kwanza hapa watu wameshafika kuangalia miili ya watoto wao

Ken :( Kwa mkewe) twende mama Ariana…twende tukaangalie mwili wa Miriam wetu kama utakuwepo

Ariana: baba hali yako sio nzuri kwanini usitulie tu

Ken: niache Ariana nataka nikamuone mwanangu nataka kumuona Miriam wangu mwanangu...Niletee ufunguo wa gari haraka

Ariana :( anakimbia ndani kuuchukua ufunguo wa gari) huu hapa baba ila utaweza kuendesha acha niendeshe

Ken: sawa ila fanya haraka

(Familia nzima wanaelekea kwenye gari tayari kwa ajili ya kwenda eneo la tukio la ajali mbaya ya gari lililogharimu maisha ya wanafunzi)

Mary:(Analia sana) Miriam… (anajisemea moyoni) Mungu onekana baba yangu, onyesha ukuu wako mfalme wa Amani mwanangu hawezi kuwa amefariki tena kabla hajajua kuwa mimi ndo mama niliyemzaa (Analia)Mungu nakulilia leo Mungu wangu…namhitaji mwanangu Mungu wangu

Ariana :( anajisemea moyoni) mapigo Kama haya huwatokea wenye dhambi tu (anacheka moyoni) yeye aliniibia bwana Mungu kampa pigo… (Anaendelea kujisemea moyoni) sijafanya chochote ila Mungu ameshaniondolea pingamizi (anacheka moyoni)

Ken: Ariana bado hatujafika tu?

Ariana: baba tulia...

(Safari inaendelea na baada ya mwendo wa dakika kadhaa wanafika eneo la tukio)

Ariana: watu ni wengi

Ken :(bila kupoteza muda anatoka kwenye gari na kukimbilia ilipo miili ya wanafunzi) Miriam… (anamuona Jeremy) Jeremy...Shemeji yako (Analia)

Jeremy :( macho yamevimba kwasababu ya kulia sana) baba…

Ken: mbona uko hapa? baba kuna ndugu yako

Jeremy:(machozi yanamtoka kwa wingi) hapana baba…nimekuja kumtafuta Miriam

Ariana:(anaingilia) amekuja kumuona shemeji yake...

Ken: oh, una roho nzuri sana baba...

(Jeremy na Ariana wanaangaliana)

Ken: sasa hapa umemuona?

Jeremy:(bado machozi yanamtiririka) sijamuona baba

(Mary na Keddy wanakuja walipo)

Keddy: Jeremy...upo hapa baba

Jeremy :( Analia kwa uchungu)

Ken: mbona una uchungu sana Jeremy una shida gani?

Jeremy: sina shida baba…

Ariana: walikuwa wana mahusiano mazuri na shemeji yake naona ni mshtuko tu huo…

Jeremy:ni kweli baba ni mshtuko tu

Ken: oh sawa…mwanangu… (Anaangaliangalia) inamaana hawa ndo wanafunzi waliokuwepo?

Jeremy: inavyoonyesha

Ken: basi baba usilie bwana unajua umelia Sana ni wakati wako sasa kutulia kwani polisi wanasemaje?

Jeremy: hawajasema kitu…

Ken: dah

Keddy: labda twende mochwari sasa hapa hata hatumuoni Miriam

Mary :( Kwa keddy) dada tuendelee kumuangalia

Keddy: hayupo hapa …Miriam hayupo hapa angekuwepo tungemuona Mary

Mary :( Analia) Miriam uko wapi mwanangu…uko wapi mama?

Jeremy :( Analia kwa uchungu)

Ken :( Kwa Jeremy na Mary) mbona mnaonekana mna uchungu kuliko sisi?

Keddy: baba Ariana maswali gani hayo? Kila mtu anajua kuubeba uchungu wao…waache hiyo ndo jinsi wanavyobeba uchungu wao…

Ken:(anashusha pumzi) sawa haya twendeni huko mochwari

(Familia inaondoka kuelekea mochwari)

Post a Comment

0 Comments