SCENE 60:-
FINALE: -
BAADA YA MIEZI TISA: -
(Ni mchana mwingine mtulivu, maisha yanaonekana kuendelea vizuri, Angelina
ambae sasa ni mama mwenye nyumba ile ya kifahari anaonekana ni mama mjamzito
ambae anaweza kujifungua wakati wowote, anajikongoja taratibu kwenda jikoni)
Angelina: Esther mdogo wangu naomba chai yaani
nasikia tumbo linauma kweli (anaugulia)
Esther :( msichana
wa kazi) sawa dada…nikupashie maji pia?
Angelina: nimeshajimwagia maji si kuna hita
bafuni…wewe nipe chai (anasikia maumivu)
maamaaaaa...Esther muite shemeji yako…mpigie simu (anaanza kulia) naumia (anakaa
chini sakafuni)
Esther: dada nini tena?
Angelina: naumia, tumbo linauma sana…muite Rama…
Esther :( anakimbia)
kaka Rama…kaka Rama
Ramadhani: nini tena?
Esther: njoo dada anaumwa?
Ramadhani :( huku anakimbilia ndani) mpigie Ray
simu haraka
Esther :( anachukua
simu iliyopo getini na kupiga namba ya Raymond) shemeji…shemeji dada
anaumwa tumbo
Raymond: kafanyaje…nakuja sasa hivi (anakata simu kisha anatoka nje anapanda
gari na kuliondoa haraka)
(Upande wa kina Angelina)
Angelina: mama (anasugua
mapaja) inauma Sana…inauma Sana jamani acheni
Esther :( anakuja
akitokea nje) shemeji anakuja
Angelina: nyie hapana naomba twendeni atatukuta
hospitali jamani…twendeni tumkute kwanza hukohuko nyie hamjua tu maumivu
ninayoyapata
Esther: kaka Ramadhani, huu hapa ufunguo wa gari…tumpeleke
(Catherine, Edmond, Christina na Peter wanafika)
Christina: jamani Raymond kanipigia simu anasema
huyu kapata uchungu…sasa mbona mmesimama tu?
Angelina: nisaidieni jamani nakufaaaa
Catherine: kufa hufi Mimi mwenyewe niliipata freshi
miezi miwili iliyopita wewe usijali bwana utakuwa sawa
Christina: kabisa hata Mimi nilijipa moyo sasa hivi
Nina libaba langu akha mwenyewe sina shida
Peter: mnaongea Sana mwenzenu anaumwa Sana
Catherine: tunampa moyo
(Raymond anafika akiwa anaonekana amepaniki)
Edmond: embu tulia
Raymond :( Kwa
Angelina) mke wangu (anambeba na
kumpeleka kwenye gari) naelekea hospitali kwangu
(Edmond,
Catherine, Christina, Peter, Ramadhani na Esther wanapanda magari waliokuja
nayo na kumfuata Raymond nyuma.)
Raymond :( akiwa
anaendesha gari Kwa kasi Sana) basi mke wangu vumilia tunafika sasa hivi
hospitali
Angelina: Ray…fanya haraka
Raymond: najitahidi mke wangu
(Raymond anaendelea kuendesha gari Kwa kasi kubwa Sana na baada ya
mwendo kidogo hatimaye wanafika katika hospitali kubwa ya Raymond.)
Raymond :( anashuka
kwenye gari haraka anambeba mkewe kisha anaingia nae ndani) jamani nyie mpo
wapi…huyu chupa imeshapasuka
Nesi: jamani mke wa bosi chupa imeshapasuka
Angelina :(
anaishiwa nguvu)
Raymond: comeon baby…you can do it…jitahidi
mama…you can do it
(Madaktari, pamoja na manesi wanakuja na machela na kumbeba Angelina na
kumkimbiza katika wodi ya wazazi)
Daktari :( Kwa
Raymond) tulia dokta Leo acha tufanye wenyewe… (Anaondoka na kuelekea walipompeleka Angelina)
(Edmond, Catherine, peter, Christina, Esther na Ramadhani wanafika
aliposimama Raymond)
Edmond: vipi Mond?
Raymond: ameingia leba…
(Mr and Mrs Bembele nao wanafika)
Mr. Bembele: hamjambo
Wote: hatujambo shikamoo…
Mrs.Bembele: hamjambo?
Wote: hatujambo shikamoo
Mr & Mrs. Bembele: marahaba
Mrs.Bembele: vipi huyo anaendeleaje?
Raymond: ndo ameingia leba…chupa tayari
imeshapasuka
Mr. Bembele: huyo tayari keshaleta habari njema
(Wanacheka)
Raymond :(
anaonekana kuwa na wasiwasi sana, anazungukazunguka mara achungulie dirishani,
mara atake kuingia ndani ya chumba hicho)
(Upande wa Angelina kazi imeanza, anajitahidi kusukuma kwa nguvu zake
zote)
Daktari: shemeji jitahidi…
Angelina :( anajitahidi
kusukuma kwa nguvu na hatimaye anajifungua)
(Mmoja wa madaktari anatoka nje ya chumba hicho akiwa na furaha sana)
Daktari: hongereni Sana…shemeji amejifungua salama,
mapacha wa kike na wa kiume
Raymond :( anashangilia
kisha Analia kwa furaha sana)
Mr. Bembele: Asante Mungu…
Mrs.Bembele: Asante Mungu…mkwe kaniletea mke mwenza
na mume…loh kaniweza (anajikuta Analia
kwa furaha huku anamkumbatia mume na mwanae)
Christina :( anafurahi
pia)
Peter :( anafurahi)
Catherine: wow…mdogo wangu kawa mama wa watoto
wawili kwa mkupuo…
Edmond :( anamkumbatia
Raymond) hongera Sana Mond…umekuwa baba sasa uache kudeka
(Wanacheka)
Angelina :( akiwa
anasaidiwa na manesi anatoka nje ya chumba kile na kuelekea kwenye chumba cha
mapumziko)
Raymond :( anamkimbilia
mkewe na kumkumbatia) asante sana wife…asante mno mke wangu (anambusu mfululizo)
Angelina :(
sauti ya kuchoka) utaniangusha (anacheka)
Raymond: pole honey…
(Wote Kwa
pamoja wanaenda kumsindikiza Angelina mpaka kwenye kitanda cha mapumziko watoto
wake mapacha wanawekwa pembeni yake)
Mr. Bembele: hongera Sana binti yangu
Angelina :(
anatabasamu) Asante baba
Mrs.Bembele: wow…hongera Sana mama…Asante Kwa
kuniletea mke mwenza na mume, loh!!Wewe nae umeniweza
(Wote waliopo wanaangua kicheko)
Raymond :( anarekodi
tukio kwenye simu yake)
Christina: watoto wataitwa nani na nani?
(Raymond na Angelina wanaangaliana kisha wanacheka)
Raymond: wa kike ataitwa Angelica na wa Kiume
ataitwa Reynolds
Mr. Bembele: eeh mi nikajua mmoja ataitwa Glory na
mwingine Desmond…
Raymond: ah acha waitwe hivyo
Edmond: hayo majina mbona ya kizungu Sana tutakuwa
tunawaitaje?
Catherine:si Anje na Ray?
Peter :( anashangaa)
halafu watoto wanaitwa Kama wazazi wao ee
Raymond: Asante Peter Kwa kuwa wa kwanza kugundua
hilo…
Catherine: anje mama Anje, na Ray baba
Ray…wow…jamani
Mrs.Bembele: jamani inapendeza Sana hapo ukute
mlipanga hata kabla ya kuzaa hawa watoto wa siku hizi
Raymond na Angelina :( wanacheka)
Mrs.Bembele: Mama Angelina hajapewa habari hizi… (Anachukua simu kisha anampigia video call
mama Angelina)
(Simu inaita)
Mama Angelina :( anapokea) hello…
Mrs.Bembele: hongera Sana ndugu yangu Angelina
kajifungua
Mama Angelina :( anafurahi Sana) mtoto gani?
Mrs.Bembele: wa kike na wa kiume
Mama Angelina: mapacha?
Raymond :( anaingilia)
Raynolds na Angelica
Mama Angelina: Angelina na Raymond…? Jamani hayo si
majina yenu wewe na mkeo
Mrs.Bembele: nakwambia…
Mama Angelina: basi asanteni Sana nitakuja kuwaona
jamani
Mrs.Bembele: sawa mama (anakata simu)
Raymond: jamani selfieeee
(Wanakaa vizuri na kupiga picha ya pamoja)
Mr. Bembele :( anawabeba watoto wale mapacha)
Edmond nipige picha na wajukuu zangu
(Wafanyakazi
wa Raymond wa hospitali hiyo wanawavamia ndani)
Nesi: tunataka tupige picha
Glory: jamani hongereni…
Angelina :( anatabasamu)
Asante Sana
Pendo: watoto wanaitwa kina nani?
Edmond: Anje na Ray…
(Watu wanaendelea kufurahia pamoja wengine wanawabeba watoto huku Raymond
akijisemea myoni)
Raymond:hivi ndivyo maisha yangu yalivyogeuka
kuwa…maisha yangu yamekuwa ni ya furaha sana,nilichagua kuufuata moyo wangu
hata pale akili yangu ilipokataa kunipa ushirikiano…nilikutana na mke wangu Angelina
katika mazingira ya kawaida sana,siku moja mara baada ya kuchoka kazi za
nyumbani pamoja na kazi za ofisini,niliomba msaada kwa rafiki yangu kipenzi Edmond
wa kunitafutia msichana wa kazi,nae hakusita akanipatia msichana wa kazi…moyo
wangu uliripuka mara baada ya kumuona binti yule nafsi yangu haikujali kama ni binti wa hadhi ya chini au lah…niliupa moyo
wangu nafasi ya kumpenda,sikujali nani wala nani nilimpenda na leo hii nina furaha ya kwamba sikusita
kumpenda mke wangu , najiona ni mwanaume mwenye bahati sana kuwa na mwanamke
kama Angelina,mimi nay eye tulitofautiana matabaka lakini hiyo haikutuzuia kuwa
wamoja na leo mimi nay eye ni baba na mama wa watoto mapacha Raynolds na
Angelica.it was nice falling in love with my housegirl..She turned to be
perfect for me…forever I will be proud to tell everyone that I fell in love
with my housegirl…I love you Angelina,I love my kids,I love all my friends and
my parents
Angelina :( anamshika
bega mumewe) unawaza nini baba Ray…
Raymond :( anavuta
pumzi ndefu huku anaangalia watu wote waliopo hapo) love doesn’t ask
why…inatokea tu wakati wowote na katika mazingira yoyote…haichagua kabila,
dini, tabaka wala nini. Ikija inakuja na hatuna budi kupokea zawadi hiyo.
Nilikutana na mke wangu akiwa hana kitu chochote tabaka lake na langu vilikuwa
ni vitu viwili tofauti
Watu :( wanamsikiliza
Kwa makini)
Raymond: ilitokea tu…niliamua kuipokea zawadi hiyo
na leo hii imenipa furaha ya ajabu (anambusu
mkewe kwenye paji la uso) My Angelina, mama Angelica (anatabasamu)
Watu: wow… (Wanapiga
makofi)
Mr. Bembele: wow…overall, we are all happy…si ndio
jamani wote si tuna Amani?
Watu: ndio
Mr. Bembele: love is most beautiful thing…
Edmond: selfiiiiieeeee
(wote wanajipanga kupiga picha ya pamoja, wanaonekana kufurahi sana na
kila mmoja anaonekana hana kinyongo, kuna pongezi na Amani mahali hapo, watu wanatabasamu,
wanacheka kila kitu kipo safi.)
WRITTEN BY: MARYGLORY SEVERINE KIWANGO (VIDYA)
THE END
0 Comments