SCENE 2:
(Dada Fulani amekaa kwenye chumba Fulani kinaonekana
kina Giza kiasi na haonekani vizuri kwa mantiki ya sura ila inajulikana kwamba
ni mwanamke)
Mwanamke:
Robert alinikosea ndo maana nikaona nimuue…asingefanya alichokifanya basi
nisingemuua na wala nisingepata wazo za kumuua kinyama hivyo… natumaini kuwa
huko alipo atakuwa ameona sababu ya mimi kumuua alinichezea na kuniacha solemba
na kunifanyia vitu vingi sana vibaya kwa jeuri ya pesa hiyo ndo adhabu yake,
ilinilazimu nilipize kisasi jamani sio kwa mambo ya ajabu aliyoamua kunifanyia
huyu mzee asiyekuwa na haya…nenda Robert…nenda hawara yangu…pole kwa wote
walioguswa na msiba huu.
(Mara inasikika kelele nje,
hatoki anaendelea kukaa kwenye chumba kile chenye Giza)
Polisi
:( wamesimama nje ya nyumba ile
iliyoungua na moto jana yake) jamani habari zenu
Majirani:
salama
Polisi:
naombeni wote mtoke nje kuna kitu hapa kimejitokeza juu ya mwili wa marehemu
(Majirani wote wanatoka nje kuja kusikiliza
wito)
Polisi:
mmetoka wote?
Liliana:(anakuwa wa mwisho kutoka) nilikuwa
nimebaki mimi tu(anatabasamu)
Polisi:
ulikuwa wapi?
Liliana:
nilikuwa naoga
Polisi:
sawa
Mama
Neema: hapa sasa tumetoka wote sasa
Polisi:
sawa… (anawaangalia majirani wote)
basi sawa…kwa mujibu wa taarifa ya hospitali marehemu bwana Robert hakufa kwa
ajali ya moto bali alichomwa kwanza visu ndipo akaungua
(Minong’ong’ono baina ya
majirani)
Polisi:
nani kati yenu alisikia au alishuhudia tukio hili
Mama
neema: mimi nikiwa mmoja wao…
Polisi:
uliona nini?
Mama
neema: moto tu
Polisi:
hukuona mtu…anaingia na kutoka?
Mama
neema: hapana hatukuona kabisa
Polisi:
jaribu kukumbuka
Mama
neema: hapana sikuona kabisa
Liliana:
jaribu kuvuta kumbukumbu unaweza ukakumbuka
Mama
neema :(kwa polisi) yaani sikumuona
kabisa labda kama wenzangu walimuona
Polisi
:( anawageukia wale wawili) hamkuona
kitu…
Majirani:
hapana
Polisi
:( anajikuna kichwa) dah!!Muuaji alitumia
akili Sana hakuingilia mlango wa mbele wala kutokea huko na pia ameharibu
ushahidi wote uliokuwa unatakiwa…amecheza karata vizuri sana
Mama
neema: yaani…ila hawezi kuwa ametokea mtaa wetu, Bw. Robert alikuwa ni mtu
mzuri sana alikuwa ni tajiri lakini aliishi na watu vizuri alitupenda sana na
kipindi cha sikukuu wote hapa majirani zake tulikuwa tunanufaika, hakika
alikuwa ni mtu wa watu sana hasahasa hapa kwetu wote hapa tulikuwa tunampenda
Liliana:
lakini usiusemee moyo ndugu yangu
Kijana:ni
kweli dada yangu unachosema ila kwa bw. Robert ambae amemuua (kimya kidogo) hawezi kuwa ametokea hapa mtaani,
wewe si umekuja juzi juzi tu…humjui vizuri bw. robert alikuwa ni mtu wa watu
sana
Polisi:
sawa…ila wanasema kikulacho ki nguoni mwako na rafiki yako wa karibu ndo adui
yako naungana na huyu binti mjamzito kwa kusema msiusemee moyo…hivyo basi…majirani
wote ndo mtakuwa ni watu wa kwanza kabisa kuondoka na mimi mpaka kituoni kwa
ajili ya kuangaliwa alama za vidole yaani finger prints maana kilikutwa kisu
eneo la tukio hivyo tutapima alama ya vidole kisha tutajua na jinsi mlivyo
pandeni kwenye gari hakuna mtu kutoroka hapa
(Bila wasiwasi majirani wote
wanapanda kwenye gari la polisi na kuelekea kituo cha polisi, wanapofika huko
haraka bila kupoteza muda wote wanapimwa alama za vidole vyao na kuamuliwa
wasubiri nje)
Polisi:
sawa naomba mnisubiri hapo nje nakuja baada ya muda
(Majirani wanatoka nje na
kusubiri kwenye viti, na baada ya sekunde kadhaa polisi anakuja)
Polisi:
kweli mlisema kweli kwamba Robert alikuwa ni watu wa mtu na hata siku moja
hawezi kuwa ameuawa na mmoja wa majirani zake…hiki kisu hakiendani na alama ya
vidole ya yoyote hapa…sasa ni jukumu letu sisi polisi kumtafuta muuaji na wala
hataenda bure
Mama
neema:si nilikuambia yaani muuaji ametoka mbali sana sijui wapi
Polisi:ni
kweli mama tumeamini maneno yako
(Wakati huo mke na watoto wa bw. Robert
wanafika kituoni hapo)
Lydia
:( mke wa Robert) jamani habari zenu
Wote:
salama…
Polisi:
na wewe ni…
Mama
neema:ni mke wa marehemu huyu anaishi Canada watoto wake wanafanya kazi huko
ndo wamemchukua
Liliana:
maskini pole dada yote ni kazi ya Mungu, mume wako anaonekana alikuwa ana
upendo sana na watu…watu wengi wanamlilia (anasikitika)
Lydia
:( anaanza kulia kwa uchungu sana)
Mume wangu tulitoka kuongea nae jana akaniambia kuwa amenikumbuka anataka aje
akae Canada amechoka kukaa peke yake huku…jana hiyohiyo nikapigiwa simu kuwa
mume wangu amekufa jamani (Analia sana)
Polisi:
pole sana mama, (anamsogezea kiti kisha
anamsaidia kukaa) jikaze mama
Lydia:
naomba polisi mfanye kazi yenu kuhakikisha kuwa muuaji wa mume wangu
anapatikana mapema Zaidi…nataka apatikane ili (anaongea kwa hasira) nimshuhudie kwa macho anavyonyongwa
Raphael
:( mmoja wa watoto wa marehemu)
habari zenu jamani...
Wote:
salama
Polisi:
wewe ndo mtoto au?
Raphael:
(kinyonge sana) ndio, naitwa
Raphael…kaka zangu watakuja baadae kidogo (anasikitika
sana) jamani baba yangu dah…alipanga kuja kukaa na sisi Canada leo hayupo tena
(Analia)
Majirani:
pole sana
Raphael:
(anafuta machozi) nashukuru sana na
Mungu ndo mpangaji wa yote…ila (anamuangalia
polisi) naomba haki itendeke nakutegemea sana…sisi tumeshakuwa watu wazima
ndio tuna wake zetu lakini tulikuwa tunamhitaji baba yetu
Polisi:
usijali tutafanya kila kitu mpaka haki itatendeka lazima tumpate muuaji
Liliana:
aisee…na alifanya kitu cha kinyama sana
Polisi:
sio kidogo
Liliana:
na alikuwa mwanamke au mwanaume?
Polisi:
haijajulikana…
Mama
Neema: yaani hakuna anayejua chchote
Polisi:
katumia akili nyingi Sana
Mama
Neema: sana
Polisi:
ila itakuwa ni mwanaume tu maana kama ni mwanamke asingeweza kupambana nae
hivyo
Mama
Neema: na Robert alikuwa yuko vizuri sana kimazoezi
Polisi:
nilikuwa namfahamu maana mara nyingi sana alikuwa anakuja kuwaona wafungwa
Mama
Neema: hakika tumepoteza jembe…
Kijana:
hakika
Liliana:
Mimi nilikuwa simjui…hata kidogo
Mama
Neema: sasa wewe unashinda unalala ungemjulia wapi?
Liliana:
ndo hivyo vitu vizuri huwa havidumu
Mama
Neema: kabisa
Polisi:
sasa nyie nendeni mkafanye mipango ya mazishi mwili wa Robert umeharibika sana
cha msingi tu n kwenda kumzika tu halafu sisi bado tunafanya uchunguzi tutakuwa
tunawapa taarifa ni wapi tumefikia sawa
Majirani
pamoja na familia ya marehemu: sawa
(Wanaondoka)
0 Comments