SCENE 3: -
BAADA YA MIEZI SITA:
(Familia ya bw. Robert yaani mke na watoto
wake wapo kituo cha polisi wakifuatilia kesi ya mauaji ya mpendwa wao)
Gabriel
:( mmoja wa watoto wa bw. Robert)
mkuu huu ni mwezi wa sita tangu baba yetu auawe kikatili lakini bado hakuna
vitu vya maana ambavyo mmetupa Zaidi ya kusema kuwa mnaifanyia kazi, mnafanyia
kazi mpaka lini mkuu? Embu tupeni jibu la kueleweka bwana tumesubiri Sana
Polisi:
naomba tuendelee kuwa wapole tu, tutampata aliyefanya mauaji Yale na kuchoma
nyumba yenu, kuweni wapole tu…tutampata tu, kesi ngumu sana maana hakuacha
ushahidi mwingi
Raphael:
kila mara huwa mnatuambia hivyo…tumechoka Kama hamuwezi naomba tuite wapelelezi
toka nchi za wenzetu waje wafanye uchunguzi
Lydia
:( Analia) yaani mume wangu aliuawa
kikatili Sana na hakuna mtu anaehangaika na kifo chake nyinyi polisi hamfanyi
chochote kila tukija hadithi ni ile ile kuwa mtaifanyia kazi lakini kimya,
jamani tusaidieni tunataka kupata muafaka wa hili suala (anaanza kulia) au mnataka kesi ya mume wangu iishie njiani?
Michael:
(mtoto wa pili wa bw Robert) mama
acha kulia hapa cha msingi ni kutafuta wapelelezi kutoka nje naona hawa polisi
wameshindwa kufanya kazi yao
Polisi
:( anapata jazba) kijana chunga mdomo
wako, watu hatulali
Michael:
mbona hakuna jipya kila siku point ni ile ile? Bora tuite wapelelezi kutoka nje
Gabriel:
ndo maana yake dogo hapo maana huu ni mwezi wa sita na hakuna kilichofanyika
Zaidi ya hadithi…hii inamaanisha kuwa hamjui kufanya kazi zenu…
(Wakati huu anakuja mwanamke Fulani
haonekani kirahisi na amebeba mtoto mchanga anafika anaingia walipo familia ya bw.
Robert na polisi mwenye dhamana ya kusimamia kesi ya bwana Robert)
Polisi
:( Kwa jazba) wewe mama unataka nini?
Mwanamke
:( anaonekana kikamilifu na si mwingine
bali ni Liliana yuleyule mmoja wa majirani waliokuwa wanaishi karibu na nyumba
ya bw. Robert) nimekuja kujitoa mwenyewe maana nimeona mlishindwa
kunikamata
Polisi:
unamaanisha nini?
Liliana:
(Kwa upole Sana) nilimuua bw. Robert
(Wote waliopo hapo wanapigwa
butwaa)
Lydia:
wewe mtoto…kwanini ulifanya vile? Kwanini (Analia
Sana) ulimuua mume wangu alikufanya nini kibaya wewe mtoto…
Gabriel:
wewe dada…nini kilikufanya ufanye vile? Nini kilikupelekea kufanya yote hayo…?
Raphael:
sikutegemea na wala sikuwaza kuwa mmoja wa majirani zake wangemfanyia hivyo?
Polisi
:( anasikitika Sana) kwanini ulifanya
vile
Michael
:( anamsogelea) kwanini ulimuua baba
yangu na kuchoma nyumba yetu?
Liliana:(kwa utaratibu)hasira…huyu mtoto ni mtoto
wa bw.Robert…na pia alinidanganya hana mke wala watoto,aliniambia kuwa mke na
watoto wake wote walikufa kwenye ajali hivyo kabaki hana mtu na kwamba
ananipenda sana,kwa akili zangu za kitoto nilimuamini sana na nikajua nimepata
mwanaume wa maisha yangu alinidanganya aliponichoka akaniambia kuwa
ana mke na watoto…na anawapenda sana,alinitukana sana na kuniambia maneno ya kashfa…kitendo
kilichonipa hasira…sana na kikanipa hasira na kunifanya nifanye kitendo kile
haikuwa kwa nia mbaya ilikuwa ni hasira tu…alinisukuma kwa mambo mengi mengine
ni hadithi ndefu sana
Polisi:
pamoja na hayo usingemuua…
Liliana:
ningefanyaje? Aliniharibia maisha yangu na furaha yangu kwa asilimia
mia…namchukiaa sana
Polisi
:( kimya kidogo)
Liliana:
ningefanyaje? Ningekuja kwenu je mngenisaidia?
Lydia
:( Analia) lakini pamoja na hayo
usingemuua mume wangu…
Liliana:
ningefanyaje? na pia nilimuua kujikinga mimi na mwanangu maana sio mara moja
bali mara nyingi sana alituma watu waje waniue
Polisi:
sijui kwakweli kikubwa tu upo chini ya ulinzi…tukutane mahakamani binti
Liliana
:( kimya hasemi kitu)
Polisi
:( anatoka)
(Wote waliopo hapo hawana la
kusema Zaidi ya kukaa kimya na kuangalia chini huku kila mtu anawaza la kwake)
Gabriel:(anajikuta anasikitika sana) sijui ni nini
ila kwa niaba ya wadogo zangu na baba yangu napenda kukuomba msamaha kwa
maumivu yote ambayo baba yetu alikusababishia…msamehe sana na umuombee Mungu
amsamehe kwa yote aliyokufanyia…
Liliana
:( Analia sana)
Raphael:
hatujakifahamu kisa chote kilichokusababisha ufanye hivyo ilia naomba kwa hayo
machache uliyotuambia mi naomba nimuunge mkono kaka yangu na kuwaomba msamaha
wewe na mwanao kwa yote ambayo yamejitokeza
Michael:
msamehe baba yetu na umuombee apumzike kwa Amani
Lydia
:( Analia)
Polisi
:( anarudi yeye pamoja na askari mwenzake
huku wamebeba pingu)
Lydia:
si mngemuacha amlee mtoto wake hata mpaka akue kidogo, wewe ni wa kunyongwa tu
(kwa polisi) anyongwe huyu…muuaji
mkubwa huyu
Polisi:
mahakama itaamua na sio sio… (Kwa polisi
mwenzie) afande Marco mfunge pingu umpeleke rumande, (kwa Liliana) mlete mtoto
Liliana
:( anamshusha mtoto na kumpa polisi)
Polisi
:( anamkabidhi mtoto kwa Lydia)
Lydia
:( anampokea)
Afande
marko: sawa afande… (Anamfunga pingu kisha
anamchukua na kumpeleka rumande)
Polisi
:( anashusha pumzi) kitu mlichokitaka
kimetimia
Lydia:
ni kweli lakini…sijui kwanini pamoja na jazba yote mara baada ya kumuona muuaji
wa mume wangu na pamoja na kwamba ninamkumbuka sana mume wangu…ila baada ya
huyu binti kusema kwanini alimuua mume wangu sina hasira nae nimejikuta tu
namuonea huruma sana…
Polisi
:( anacheka kidogo) si umesema
anyongwe?
Lydia
:( anacheka kidogo) ni hasira tu
Gabriel:
kuna kitu kuhusu huyu dada ambacho watu wengi hawawezi kukijua kirahisi mpaka
akiseme yeye…
Lydia:
sijui ni nini
Gabriel:ni
hasira tu
Raphael:
kweli…hiyo hasira ilisababishwa na kitu Fulani…sijui ni nini lakini hiyo hasira
ilisababishwa na kitu kama depression…
Polisi:
yote kwa yote…aliua, na hatuwezi kulikalia kimya…
Michael:
hakuwa katika akili yake timamu…alisukumwa na kitu
Polisi:
aliua, iwe kwa makusudi au kwa kusukumwa…atahukumiwa…Lulu alipomuua Kanumba si
ilikuwa kwa bahati mbaya ila si alihukumiwa?
Raphael:
kwa kweli
Lydia:
sawa…tutamsikiliza Zaidi atuambie…kisa kizima kwa sasa turudi nyumbani
Polisi:
nyie nendeni tukutane mahakamani
Raphael:
mtoto bado mchanga Sana, unaonaje akachwa hapa akae na mama yake?
Gabriel:
yes, aachwe tu na mama yake maana atahitaji kunyonya na kadhalika
Polisi:
sawa (anaita mmoja wa maafande)
Afande
:( anakuja)
Polisi:
kuna mama amekamatwa sasa hivi hapa mpelekee mtoto wake
Raphael:(anaonekana kumhurumia sana Liliana)
maskini mwanae bado mdogo
Afande
:( anamchukua mtoto kisha anatoka nae
kuelekea rumande alipo Liliana)
Polisi:
ndo hivyo…yote maisha na hakuna ajuae kesho
Wote:
kabisa
Lydia:
sawa sisi…tunaenda
Polisi:
karibuni Sana
(Lydia
na wanae wanaondoka huku wamepoa tofauti na jinsi walivyokuja, wanapanda gari kisha
wanaondoka zao)
0 Comments