SCENE 25: -
BAADA YA MIAKA KUMI NA SITA: -
(Asubuhi nyingine njema, hali ya
hewa ni njema na ya kupendeza, jua ndo linaanza kuchomoza, binti mrembo
anafungua mapazia kuruhusu mwanga kuingia chumbani kwake, anatabasamu mara
baada ya kuona mwanga unaompa tumaini la siku mpya)
Binti
:( anakaa kitandani) oh napenda Sana
maisha yangu…
(Kuna mama ameenda umri anakuja
chumbani Kwa binti)
Mama:
Liliana…mwanangu
Binti:
abee mama yangu mpenzi…Madam Bianca
(Wanacheka)
Bianca:
umebadilika Sana mwanangu…yaani mtu akikuona hawezi kukukumbuka…
Liliana
:( anacheka)
Bianca:
happy 23rd birthday my love
Liliana:
thank you…mama (anamkumbatia)
Bianca
:( anamkumbatia pia) nakupenda binti
yangu umekuwa ukinipa Amani na furaha kubwa tangu siku ya kwanza nimekuona
mwanangu
Liliana:
Asante mama kwa kunilea vyema umenisomesha umenipenda nakupenda sana mama
Bianca
:( anacheka Sana) tumepatana
Liliana:
Sana…
Bianca
:( anashangaa) Liliana
Liliana
:( anaogopa) nini mama?
Bianca:
hujaoga, hujavaa na leo ni birthday yako una mambo mengi sana ya kufanya moja
ni kwenda chuo
Liliana:
NO…mama…No Leo siendi chuo I want to enjoy with you mama…
Bianca:
of course, ila mwenzio nimezeeka hata sijui kuenjoi
Liliana:
nani kakwambia umezeeka bado ni binti mrembo na wa kuvutia kama ulivyokuwa
miaka 16 iliyopita
Bianca:
unanipamba tu muone…kitoto kiongo hiki
Liliana
:( anacheka kidogo) acha nikaoge...Toka
nibadilishe nguo
Bianca:
hivi umesahau nilikuwa nakuogesha na mara zote ulipokuwa ukiugua nakuogesha
naukubwa wako
Liliana:
nakumbuka mama ila sasa mwenzio nimeshakuwa limama
Bianca:
hiloooo…umekuwa limama wapi hata boyfriend huna…toka hapa
Liliana:
mama sitaki boyfriend kwa sasa na unajua…unajua nilijaribu kuwa nae
akanidanganya kwahiyo sitaki tena...Nataka kuwa single kwanza kwa muda
Bianca:
wewe mimi nishazeeka nataka wajukuu…
Liliana:
mama mi bado mdogo bwana nitakuwa nae
Bianca:
okay…take your time usije ukasema mama alinishawishi…ila kumbuka wewe sio
teenager tena umeshavuka ule umri wa kuruka kutoka kwa huyu kwenda kwa huyu
sasa wewe umefikia umri wa kuchagua na kuwa serious
Liliana:(anatabasamu)
nakuelewa mama kwamba unataka mjukuu utampata
Bianca:
lini sasa?
Liliana:
soon…haya nenda nioge nije ninywe chai niwachukue Anna na Bella tukazurure
Bianca:
haya bwana…ngoja nitoke…(anatoka)
Liliana:(anaingia bafuni na kuanza kuoga, na baada ya
dakika kadhaa anamaliza kuoga anavaa kisha anapaka vipodozi kidogo kisha
anatoka kuelekea jikoni) yaani nina njaa...Mungu wangu
(Binamu zake na baadhi ya marafiki zake
wanapiga kelele)
Watu:
surprise…
Liliana
:( anageuka walipo watu wale) Oh My
God…nyie mmefanya hii kitu saa ngapi
Bianca:
wakati katoto kanakoroma sisi tulikuwa tunapamba kupika keki na kuandaa zawadi
Liliana:
jamani… (Anataka kulia) asanteni Sana
Anna
:( amekuwa binti mkubwa na umri wake ni
miaka 28) happy birthday cousin (anampa
zawadi)
Liliana
:( anapokea zawadi) thank you cousin
jamani... (Anamkumbatia)
Bella
:( amekuwa binti mkubwa umri miaka 25)
happy birthday binamu mjanja kuliko woteeeee (anampa zawadi)
Liliana
(anacheka huku anapokea zawadi)
Asante binamu mtata (anamkumbatia)
(Rafiki zake wanampa zawadi huku wafanyakazi wa
Bianca wakionekana kuwa na furaha juu ya siku hiyo yenye kawaida ya kusherekewa
kila mwaka)
Mpishi:
yaani madam anampenda Sana mwanae…
Mtunza
bustani: yaani Sana
Bianca
:( Kwa Liliana) my baby… (Anampa ufunguo wa gari) zawadi yako ya
birthday
Liliana:
wow…mama gari?
Bianca:
yeah mama gari
(Rafiki zake wanashangilia)
Bianca:
umefurahi?
Liliana:
saaaana mama…Asante Sana mama...Naomba nilione
Bianca:
sure…lipo nje…twendeni tukalione
(Liliana na rafiki pamoja na
binamu zake wanatoka nje kuliangalia gari hilo)
Liliana:
wow mama gari zuri Sana
Bianca:
umelipenda?
Liliana:
ndio mama
Bianca:
changamoto ni kwamba hujui kuendesha
(Wanacheka)
Liliana:(anaingia ndani ya gari)
(Rafiki zake wanampiga picha)
Bianca:
nakwambia mtoto wa Bianca anavyopenda kuonekana (anaguna kisha anacheka)
Liliana:(anaanza kudeka) jamani mama
Bianca:
sasa kwani uongo?
Anna:(kwa Bianca) aunt tunaweza kwenda kwenye
pati leo?
Bianca:
ya nani tena? leo kuna pati ya Liliana hapa jioni
Bella:(anamnong’oneza Bianca) tumemuandalia
pati aunt
Bianca:
hata mimi nimemuandalia pati jamani
Anna:
basi tukimaliza ya hapa
Bianca:
kwanini msifanye kesho bwana si huwa mnajua kuwa sipendi kuwaona mnadhurura
usiku
Anna:
basi sawa tutafanya kesho ila leo ndo ingenoga aunt maana ndo siku yake…
Bianca:
hata kesho itanoga sana tu bwana…baba yenu yuko wapi?
Anna:
yupo nyumbani yaani tangu mama amefariki hataki kutoka nje kujichanganya
Bianca:
maskini…mke ni mke tu pamoja na kwamba mama yenu alikuwa mkorofi ila baba yenu
alimpenda hivyohivyo
Bella:
Sana...
Bianca:
anyways tusiongelee masuala ya misiba Leo ni siku ya Liliana tuenjoi nataka
mkaangalie magauni yenu nimeweka chumbani kwa Liliana ndo mtavaa usiku au
mlitaka mvae vimini kama mnavyovaaga…halafu mbona hao wakwe hamniletei
(Anna na Bella wanacheka kisha
wanaingia ndani)
Bianca: hawajibu…watoto wa siku hizi
(anamuangalia Liliana ambae anaonekana
kufurahia zawadi yake ya gari) mwanangu kafurahi mwenyewe na hivi anapenda zawadi
(anatabasamu)
(Liliana
na rafiki zake bado wanaendelea kufurahia maisha kabla ya sherehe ya usiku)
0 Comments