SCENE 24: -
BAADA YA MWEZI MMOJA: -
(Anna, Bella na Liliana wanashuka
kwenye gari wakitokea shuleni, wanaonekana wanafuraha sana na shauku yao ni
kumuona Bianca maana hawajamuona tangu asubuhi)
Liliana:(huku anaingia ndani akiwaongoza binamu zake)
mama
Bianca:(amekaa sebuleni akiwa na mjomba wake Liliana)
abeee
Liliana:(anamuona mjomba wake) mjomba…
Mjomba:
naam mwanangu
(Anna na Bella wanamkimbilia baba
yao)
Mjomba:
hamjambo jamani habari za shule?
(Watoto wote wanaitikia)
Anna:
habari za huko baba…umepona?
Mjomba:
ndio mwanangu nimepona…
Bella:
huko India pazuri baba
Mjomba:
pazuri eeh
Liliana:(anatabasamu huku anamuangalia Bianca)
Bianca:
nendeni mkabadilishe nguo mle mfanye kama mna homework
Anna
na Bella: sawa aunt
Liliana:
sawa mama
(Wanaenda chumbani kwa Liliana)
Mjomba:(anacheka kidogo) wanaonekana kufurahi
sana…
Bianca:
acha wafurahi ni watoto…mimi napenda sana watoto Mung utu hakunijalia mtoto…
Mjomba:
ipo siku moja atakupa
Bianca:(anatabasamu) emeshanipa na sio mmoja
watatu kabisa
Mjomba:
safi sana na yote ni kwasababu ya upendo wako na roho yako Mungu atakubariki
Zaidi na Zaidi
Bianca:
usijali kaka yangu… (anabadilisha mada)
embu niambie habari za huko?
Mjomba:
ah salama tu dada yangu matibabau yameenda vizuri na ninamshukuru Mungu
nimerudi salama
Bianca:
asante sana…sasa upumzike kidogo uanze tena kuchapa kazi uikoe familia yako si
unajua kuwa wewe ndo kichwa...mkeo hana hata akili vizuri
Mjomba:(anacheka huku anaangalia dirishani)
hatajwi huyo hapo
Bianca:
yaani una mke mtata(anaguna)
Shangazi:(anagonga mlango)
Msichana
wa kazi:(anafungua mlango)
Bianca:
karibu
Shangazi:(anaingia kwa shari)
Bianca:(anaguna) kumekucha
Mjomba:(kwa mke wake) vipi mwenzetu mbona
umeingia kama kuna ugomvi
Shangazi:
hapa ndo kwa mke wako? maana umetoka huko sijui India mbio mwanaume usivyokuwa
huna adabu…mpaka kwa mwanamke mwingine ndo mke wako?
(Bianca na mjomba wamekaa kimya
huku wanamuangalia tu)
Shangazi:(anacheka kidogo) au mna mahusiano?
Bianca:(anabaki mdomo wazi)
Shangazi:
niambie nimjue mke mwenzangu na nilijua tu sio bure tu…mara kakupeleka India
mara sijui nini mara kasomesha watoto wako mara kamlea huyo mtoto wa dada yako
yote hayo anayafanya kama nani? kama sio hawara ni nini? mnadhani mimi ni mtoto
mdogo sina akili au?
Mjomba:
wewe mwanamke wewe (anasikitika sana)
Shangazi:
wewe mwanamke nini? we huoni aibu sasa hivi una watoto ni wakubwa unakuwa na
mahawara nje utakufa mshenzi wewe
Mjomba:
kuwa na adabu mimi ni mumeo
Shangazi:(anafyonza) nenda zako huko
Mjomba:(kwa Bianca) dada nashukuru kwa misaada
yako yote dada yangu
Shangazi:
eti dada hamuoni hata haya watizame nyuso zao…(anafyonza)
Mjomba:
ila mimi siwezi kukaa na huyu mwanamke tena...Namuachia ile nyumba akae peke
yake naomba tu unisaidie nipate hata chumba na sebule niishi na wanangu kwa
Amani utakuwa unanikata kwenye mshahara
Bianca:
usijali kaka yangu utapata tu nyumba nzuri hao wanao ni wanangu pia ni jukumu
letu kuwalea
Shangazi
:( anapiga makofi kishari) kwanini
msiambiane ahamie kabisa humu?
Bianca:
sikiliza mama Anna…mumeo sio hawara yangu narudia tena kuwa misaada ninayotoa
ninatoa tu kibinadamu maana mimi sina watoto na Liliana aliniomba niwasaidie
kwa vyovyote vile umemtesa sana Liliana lakini hajawasahau wala kulipa kisasi
sasa badala ushukuru wewe unabwabwaja tu kama mwendawazimu
Shangazi:
sikuwaomba na wala sikumuomba huyo Liliana anifanyie chochote ni kiherehere
chake tu mjinga sana huyo
Bianca:(anafyonza) natamani nikutandike kibao
kimoja acha kumuita mwanangu mjinga unasikia wewe usidhani ni enzi hizo hana wa
kumtetea sasa hivi nipo mimi
Shangazi:(anabenjua midomo)
Mjomba:(kwa mkewe) embu ondoka nenda zako
Shangazi:
naenda na wanangu
Mjomba:
wanangu hawaondoki hapa eti kwenda wakaishi na wewe mwendawazimu
Shangazi:
kwahiyo kwa mantiki hiyo unataka kusemaje?
Mjomba:
tunakuhama...baki na nyumba yako
Shangazi:(anaonyesha kuchanganyikiwa) eti nini? Hivi
unasema kweli?
Mjomba:
umesikia vyema mama…siwezi kuishi na mwanamke mkorofi kama wewe nimetoka safari
hata unipokee vizuri kwa adabu umpe asante huyu dada katusaidia unamwambia
maneno mabaya
Shangazi:(anaanza kushuka) lakini mume wangu
jamani nisamehe unajua ni wivu tu na nimesikia kuwa unatembea na huyu mwanamke
ndo maana nimekasirika hata ingekuwa wewe umesikia hivyo ungejisikiaje?
(Mjomba na Bianca wamenyamaza
kimya)
Shangazi:
mume wangu sasa ukiondoka mimi nitakaa na nani?
Mjomba:na
huyo atakayeweza kukaa na wewe mimi hapana…
Shangazi:(anawaita watoto) Anna, Bella
Mjomba:
embu acha kelele embu heshimu miji ya watu wewe mwanamke jamani
(Anna na Bella wanakuja sebuleni)
Anna:
shikamoo mama
Shangazi:(anawashika mkono) twendeni nyumbani
wanangu
Bella:
tunafanya homework…
Shangazi:
mtafanyia nyumbani wanangu jamani
Mjomba:
hawa watoto naenda kuishi nao
Shangazi:
eti wanangu kati ya baba yenu na mimi mnataka kuishi na nani?
Watoto:(bila kusita) na baba
Shangazi:
jamani wanangu
Mjomba:
ondoka uende zako (kwa Bianca)
tunaomba tulale hapa leo
Bianca:
haina shida kaka
Shangazi:(anashikwa hasira sana, anaondoka zake)
(Watoto, mjomba pamoja na Bianca
wanabaki wanasikitika)
Bianca:
yaani asipoangalia akaendelea na hii tabia basi ana hali mbaya sana…atajikuta
anachanganyikiwa…
0 Comments