SCENE 27: -
(Mchana wa siku kadhaa baada ya
sherehe ya Liliana, Liliana na binamu zake wanashuka katika gari ambalo ni mali
halali ya Liliana zawadi aliyopewa na mama yake wa kufikia siku ya kumbukizi ya
kuzaliwa kwake)
Anna:
wow...Binamu sikujua kuwa tunakuja mall…
Liliana
:( anacheka) sasa unajua kuwa
tumekuja …can we go?
Anna
na Bella: sure
(Wanacheka)
Liliana
:( anaongoza njia)
(Wakati wote wanaingia ndani,
wanapishana na Robert yule mwanaume waliokutana katika mgahawa siku ya sherehe
ya Liliana)
Robert
:( anamuona Liliana) hey mrembo mambo
Liliana
:( anasimama na kujaribu kuvuta
kumbukukumbu)
Robert:
tulionana kwenye mgahawa Fulani siku chache nyuma…mlikuwa na sherehe Fulani
sijui ilikuwa birthday ile?
Liliana:
ok nimekukumbuka…shikamoo?
Robert:
marahaba mrembo uko poa?
Liliana:
nipo poa za toka siku ile?
Robert:
ah Safi tu…naona mnaingia kuchukua viwili vitatu
Liliana:
ndio…
Robert:
haina shida…ila (anatoa simu yake)
ningepata namba yako ningefurahi sana
Liliana
:( anawaangalia binamu zake)
Anna
:( anampa ishara ya kukubali)
Liliana
:( anamtajia)
Robert
:( anaandika)
Liliana:
haya poa
Robert:
poa nitakutafuta...
Liliana:
sawa
Robert
:( anaondoka na kuelekea kwenye gari
lake)
Liliana
:( anamuangalia Sana)
Bella:
oh My God, he is so handsome
Liliana:
umempenda?
Bella:
ah wapi na bae wangu nimuachie nani?
Anna:
niachie Mimi
(Wanacheka)
Anna:
ila girls jokes apart, huyu baba mzuri
Liliana:
so?
Anna:
aha tunasema tu…maana anaonekana amekuzimikia kweli
Liliana:
oh, please ni mume wa mtu...
Bella;
umejuaje?
Liliana:
anaonekana tena ukute ana watoto wanaolingana na mimi n ahata kunizidi
Anna:
sio rahisi
Bella:
kwanini usimpe nafasi?
Liliana:
jamani hata hajanitokea
Anna:
atakutokea tena siku si nyingi
Liliana
:( anacheka) mna mambo nyie
Bella
:( anatabasamu) yaani
Liliana:
I mean ni mzee jamani
Anna:
age is just number my cousin
Liliana:
cuzo wewe?
Bella:
kabisa…akikutokea go for it girl
Liliana
:( anatikisa kichwa kidogo kisha anacheka)
mmenishinda tabia walahi (anacheka)
embu twendeni huko mnanishawishi vitu ambavyo mnajua kabisa kuwa mama hawezi
kukubali hata kidogo
Anna:
unamuongelea Aunt Bianca…wewe yule mzungu utaona tu anachopenda yeye ni kukuona
kuwa una raha na sio vinginevyo
Bella:
go for it baby…yaani natamani picha ianze hata sasa hivi
Anna:
yaani wewe hunishindi
Liliana
:( anatabasamu) yes…he is so cute na
hizo ndevu zake zenye mvi…amenivutia sana
(Wanacheka)
Bella:
go girl… (Anacheza kidogo)
Liliana:
yaani sijui ningekuwa wapi Kama nisingekuwa na nyie machizi wangu wa nguvu
(Wanacheka
huku wanaingia ndani maana muda wote walikuwa wamesimama nje)
0 Comments