SCENE 28: -
(Majira ya saa tatu usiku Liliana
yupo chumbani kwake anatazama tamthiliya huku anachati kwenye group ambalo yupo
yeye na binamu zake)
Liliana:(anacheka sana) yaani haya majinga (anacheka tena)
(Bianca anaingia)
Liliana:
oh mama…hujalala tu?
Bianca:
unajua mama kuwa siwezi kulala bila kukuona na kukubusu na kukutakia usiku
mwema mwanangu
Liliana:
najua mama kuwa huwezi kulala bila kuniona
Bianca:(anatabasamu) asante Liliana kwa kuja
katika maisha yangu mwanangu nimekuwa ni mtu mwenye furaha sana na zaidi nimekuwa
ni mtu mwenye bahati sana
Liliana:
mama, jamani wewe ndo nikushukuru mama yangu umenilea mimi na ndugu zangu kwa
miaka yote hii umenipa elimu nzuri kwakweli sina cha kukulipa…
Bianca:(anatabasamu kisha anamkumbatia)
Liliana:(anamkumbatia pia) asante mama, nina
bahati sana kukutana na wewe nakupenda mama
Bianca:
usijali mwanangu…
Liliana:(anatabasamu)
Bianca:
mbona unatabasamu sana?
Liliana:(anacheka) nothing mama
Bianca:
umepata boyfriend
Liliana:(anacheka kwa nguvu) of course not
mama…sijapata boyfriend
Bianca:
umri unaenda mwanangu
Liliana:
I know mama, ila sasa nataka kuwa sure
Bianca:is
there someone?
Liliana:
maybe yes, maybe no (anacheka sana)
Bianca:
you little girl (anacheka) meaning?
Liliana:
kuna mtu amenivutia ila yeye bado hajanionyesha dalili zozote za kutaka
mahusiano na mimi
Bianca:be
careful with your own heart my child usije ukasababisha majereha makubwa kwenye
moyo wako
Liliana:
yes mama
Bianca:
okay mimi nina usingizi sana…naomba nikalale wewe endelea na kuchat na mkwe
Liliana:no
mama nachati na cousins
Bianca:(anacheka sana kisha anambusu shavuni)
lala salama mwanangu
Liliana:
good night mama
Bianca:(anatoka chumbani humo)
Liliana:(anaendelea na kuchat)
(Wakati anaendelea na kuchati,
mara simu yake inaita anaipokea)
Liliana:
yes hello
Sauti
ya kiume: mrembo
Liliana:
nani?
Sauti:
Robert…umenipa namba yako asubuhi tulipokutana mall
Liliana:(anachezea nywele zake) oh okay
nambie…shikamoo
Robert:
marahaba mrembo vipi umelala?
Liliana:
hapana nipo tu ila ndo najiandaa nilale...
Robert:
oh, okay mrembo…hata mimi najiandaa nilale… (anashusha pumzi) labda samahani naomba uniambie nina mazunguzo
kidogo na wewe sijui nitakuona lini? kesho labda
Liliana:(bado anachezea nywele zake) mmmmmh mimi
nasoma kwahiyo ninakuwa busy sana mchana labda jioni
Robert:
perfect maana hata mimi ninapata muda jioni siku nzima ninafanya kazi nina
makampuni yangu mwenyewe sasa ninajikita sana na kazi ukizingatia sina familia
mimi nipo single
Liliana:
unasema kweli wewe huna familia?
Robert:
mke na watoto wangu walikufa wakati wanatoka safari, walipata ajali mbaya na
kupoteza maisha sasa nipo kwenye mchakato wa kupata mke na watoto wengine
Liliana:
maskini pole sana yaani dah…nimesikitika sana
Robert:
ndo hivyo kazi ya Mungu haina makossa
Liliana:
kabisa…basi sawa tutaonana kesho jioni
Robert:
sawa mrembo nikutakie usiku mwema
Liliana:na
kwako pia…
(Wanakata simu)
Liliana:
maskini anasikitisha imagine kupoteza mke na watoto kwa mpigo (anasikitika)pole yake sana… (anaamua kupiga simu kwa Anna) dada yule
baba kanipigia simu
Anna:
enhe!!
Liliana:
kaniambia kesho tuonane
Anna:
go girl…
(wanacheka kisha wanakata simu,
Liliana anajifunika shuka kisha analala)
0 Comments